Iran yatoa Onyo kwa nchi yoyote ya Kiarabu itakayoruhusu Israel na Marekani kutumia anga au ardhi yake kushambulia Iran itaadhibiwa vikali

Iran yatoa Onyo kwa nchi yoyote ya Kiarabu itakayoruhusu Israel na Marekani kutumia anga au ardhi yake kushambulia Iran itaadhibiwa vikali

Multiple times

Silazimish ila ni fact tu, tambo nyingi bad track record
Unalazimisha huna fact mkuu.
Nauliza maswali mawili tu mkuu.
1) Kwanini Saudi Arabia iliondoa majeshi Yemeni!??
2)Kwanini Saudi Arabia iliomba negotiation za kumaliza Yemeni war!?
Je madhara hayakufanya kazi kama unavyodai!?
 
Iran imetoa ONYO kuwa nchi yeyote ya kiarabu itakayosaidia Israel na marekani kuishambulia basi itakumbana na matatizo makubwa.

Iran imechukua msimamo mkali dhidi ya majirani zake baada ya kutoa onyo kali kuhusu ushirikiano wowote na Israel kwa ajili ya operesheni za kijeshi.

Msimamo huu mkali ni sehemu ya mkakati wa Iran kuzuia nchi za kiarabu kushirikiana Israel. Maafisa wa Iran wamesisitiza umuhimu wa "umoja wa kikanda" kukabiliana na kile wanachokiona kama tishio kutoka Israel, huku wakieleza pia umuhimu wa kudumisha utulivu huko Mashariki ya Kati

Soma pia: Israel kuishambulia Iran leo usiku, Marekani yaja juu

Onyo hilo halihusishi tu matumizi ya anga, lakini pia Iran inafuatilia kwa karibu uwezekano wa ushirikiano wa vituo vya kijeshi vya Marekani vilivyoko katika eneo la Gulf

Kwa mujibu wa vyanzo vya kidiplomasia, msimamo wa Iran uliwekwa wazi wakati wa mkutano wa hivi karibuni huko Doha.

Ujumbe ulikuwa wazi: taifa lolote la Gulf States litakaloruhusu anga yake au vituo vyake vya kijeshi kutumika kwa operesheni dhidi ya Iran litakabiliwa na kisasi.

Tehran inachukulia vitendo hivyo kama uamuzi wa pamoja wa mataifa yote ya Gulf, jambo ambalo linaweza kupanua wigo wa majibu yake.

Kazi kwako Saudi Arabia na vibaraka wengine wa marekani hapo Middle East .

Wanalingia 👇👇

View: https://www.instagram.com/p/DA7qKXKKUyr/?igsh=NWJtNmhoYXNjdGd1
 
Tusubiri maoni kutoka kwa walokole wa uswahilini wanaosali kwenye yale makanisa mabati na viti vya baa, maana wale huwaelezi kitu kuhusu taifa teule
Taifa la Israel ni Taifa la Mungu!! Ukilibariki unabarikiwa na ukililaani unalaaniwa!! Marekani na Uingereza wanaufahamu vizuri ukweli huu!! Hii haina maana kuwa Israel hawana makosa la hasha!! Wakifanya makosa Mungu mwenyewe anawaadhibu!! Hakuna Taifa duniani lililopokea baraka kama Taifa la israel. Lakini kwa upande mwingine historia inaonesha Taifa la Israel limepita kwenye adhabu kubwa sana kutoka kwa Mungu!!
Huwezi kupigana na Taifa la Israel ukafanikiwa!!

Waulize Misri na Yordani na Syria!! Watakuambia hicho kitaifa kione hivyo hivyo!!
 
Iran ina Hypersonic Missiles ambazo hata Marekani hana kwa sasa (bado yuko kwenye majaribio)!! Ndiyo maana Marekani haitaki kabisa Israel ijibu mapigo kwa Iran maana mzee mzima atajikuta meli zake zinazamishwa!! Hypersonic missiles hazidunguliwi na air defense yoyote kwa sasa!! Mzee mzima atajikuta analazimika kutumia mabomu ya nyuklia!! maana hatakubali kuadhirika!!
 
Iran washukru Marekan kwa kumuua Sadam Hussein, vinginevyo kauri hizi za Iran kuzigeuza nchi za kiarabu kama wanawake wanao sitahili kuolewa na Iran isingekuwepo.
Sasa mkuu Saddam angekuwepo si ange ungana na iran?, maana alikua keshajua kuwa USA sio mtu wa kuaminika ata kidogo, raisi wa Syria kama angekuwa kajipendekeza Kwa USA, saizi washa mla kichwa kitambo lakini Russia na iran wana mpa support mpaka leo yupo, hapo lipo la kujifunza
 
Iran wana chuki sana na Saudi Arabia

Maneno mengi hapo ana mlenga saud tu
Iran wengi ni washia na utawala wa Saudi Arabia ni Wasuni.

Yemen yatawaliwa na wasuni wanowakandamiza washia ambao wengi ni Wahuthi na ndo vita kati ya serikali ya Yemen na wahuthi ambapo Saudi Arabia amekuwa akitumia ndege za kivita anozinunua kutoka Marekani kudondosha makombora huko Sanaa.

Hizbollah ni washia ila ulitengenezwa mtandao wa eneo lote na washia wakiongozwa na Iran ili nae ajilinde. Hivyo Syria hadi Iraq kote penye Washia kuna kundi la jihadi na ndiko Isreali wapo watupa mabomu miezi yote hii.

Israeli nae ni Proxy kwa mmarekani akilinda maslahi ya Marekani katika Eneo la Mashariki ya Kati.

Ni kama alivyo Zelensky kwa NATO na Marekani ni Proxy wao akipigana na Russia. NATO na Marekani wataka eneo zaidi la Ukraine ili waweze miliki ardhi yenye madini na maliasili ya kutosha na isiwe Russia peke yake, lazima tugawane.

Hivyo kwa Iran na Saudi Arabia utaelewa ugomvi wao umelalia wapi.
 
Taifa la Israel ni Taifa la Mungu!! Ukilibariki unabarikiwa na ukililaani unalaaniwa!! Marekani na Uingereza wanaufahamu vizuri ukweli huu!! Hii haina maana kuwa Israel hawana makosa la hasha!! Wakifanya makosa Mungu mwenyewe anawaadhibu!! Hakuna Taifa duniani lililopokea baraka kama Taifa la israel. Lakini kwa upande mwingine historia inaonesha Taifa la Israel limepita kwenye adhabu kubwa sana kutoka kwa Mungu!!
Huwezi kupigana na Taifa la Israel ukafanikiwa!!

Waulize Misri na Yordani na Syria!! Watakuambia hicho kitaifa kione hivyo hivyo!!
Huu upuuzi mtupu umeandika hapa,,, bila shaka wewe itakuwa unasali kwa mwamposa,,, hao misri na yordani unaowasema unadhani walipigana na Israel?? Israel kivuli tu pale kulikuwa na mkono wa marekani na uingereza ambao ni miungu wa Israel. Poor mind eti ukiibariki Israel na ww utabarikiwa
 
Sasa mkuu Saddam angekuwepo si ange ungana na iran?, maana alikua keshajua kuwa USA sio mtu wa kuaminika ata kidogo, raisi wa Syria kama angekuwa kajipendekeza Kwa USA, saizi washa mla kichwa kitambo lakini Russia na iran wana mpa support mpaka leo yupo, hapo lipo la kujifunza

Kumbuka Iraqi na Iran walichapatana kwa muda wa miaka 8 tena vita yenyewe ilikuwa inapiganwa ndani ya nchi ya Iran yenyewe katika maeneo yaliyokuwa yametekwa na Iraq kungekuwa na maelewano hapo Iran ingemsaidia kwanza Sadam Hussein asipigwe na Marekani na kuuawa kwa kunyongwa.
 
Back
Top Bottom