Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Inaripotiwa mamlaka za Iran zimewatia nguvuni maafisa zaidi ya 20 wa idara za ujasusi, usalama na jeshi wa nchi hiyo pamoja na wasaidizi wao wengi kufuatia tukio la hivi karibuni la kuuwawa kwa kiongozi wa Hamas, Ismail Haniyeh ndani ya ardhi yake alipofika kuhudhuria uapisho wa rais mteule wa Iran.
Japo Israel imewahi kufanya mauaji mbalimbali ya raia wa Iran wenye maslahi makubwa na taifa hilo mfano wanasayansi wafanyakazi wa miradi ya nuclear ya Iran na washauri mbalimbali wa kijeshi, tukio la hivi karibuni la kuuwawa kwa Haniyeh katika ardhi yake limewapa aibu kubwa zaidi kiasi cha baadhi ya watu kudai Israel hata ikitaka kumuondoa Ayatollah ni suala la kuamua wakati na mahali tu.
Bado ni gumzo kubwa jinsi gani Mossad ya Israel iliweza kumfikia na kumuua Haniyeh akiwa chini ya ulinzi mkali wa Islamic Revolutionary Guard Corps(IRGC). Kuna nadharia mbalimbali zikiwemo drone ndogo iliyorushwa kwa karibu au bomu lililotegeshwa chumbani kwake mapema kwa msaada wa agents wa Mossad ndani ya Idara za usalama za Iran.