Iran yazuia uingizaji wa chanjo ya Corona kutoka Marekani na Uingereza kwa kutokuwa na imani na mataifa hayo

Iran yazuia uingizaji wa chanjo ya Corona kutoka Marekani na Uingereza kwa kutokuwa na imani na mataifa hayo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Kiongozi Mkuu wa Iran Ayatollah Ali Khamenei amepiga marufuku uingizaji wa chanjo ya Covid-19 kutoka kampuni ya Pfizer ya Marekani na mshirika wake BionTech, sambamba na chanjo ya Uingereza ya Astrazeneca kwa kile alichokitaja kama kukosa imani na mataifa ya Magharibi.

Katika hotuba kupitia vyombo vya habari Khamenei amesema Iran haitoagiza chanjo za Marekani na Uingereza akiashiria idadi ya vifo vinavyoendelea kusajiliwa katika mataifa hayo.

Aidha kiongozi huyo amedai kwamba mara nyingine mataifa hayo yamekuwa yakitaka kufanya majaribio ya chanjo zao kwa watu wa mataifa mengine akiijumuisha pia na Ufaransa.

Kiongozi huyo amekubali kuingizwa kwa chanjo kutoka mataifa mengine salama na anaendelea kuunga mkono juhudi za Iran kutengezeneza chanjo yake ambayo tayari inafanyiwa majaribio tangu mwezi Disemba na inatarajiwa kuanza kuuzwa kufikia majira ya machipuko.
 
Ayatollah anazuia raia wake wasipate chanjo sababu yeye hajaumwa.

Kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa.
 
Kwa hili nakubaliana na Iran ukizingatia wanavyopenda kushupaza shingo dhidi ya Marekani lazima waogope kila kitu kinachotoka Ulaya, ila sasa na wenyewe ni vilaza makajamba kama sisi Waafrika hawana uwezo wa kubuni chanjo yao, hivyo lazima wakubali sindano iingie la sivyo wataangamia.

Sisi huku tumezoea kubakwa, tuapokea tu chochote kile maana hatujawahi na hatuna uwezo huo wa kubuni chochote, hata simu zinazotumika kwenye ikulu zetu huwa za kununuliwa kutoka nje, yaani mazungumzo yote ya wakuu wa nchi zetu yanaweza yakadukuliwa kiulaini tu.
 
Ayatollah anazuia raia wake wasipate chanjo sababu yeye hajaumwa.

Kweli aliyeshiba hamjui mwenye njaa.
Hawaja wazuia raia wao kupata chanzo bali kutokana na migogoro waliyo kuwa nayo hawataki kutumia chanzo ya kutoka UK na USA.

Ila nilicho sikia wao wataitumia iliyo tengenezwa URUSI.
 
Back
Top Bottom