Irani na Israeli wana Undugu usioyumba, Makombora 300 ya Irani naona kama ni Propaganda

Bush Dokta

JF-Expert Member
Joined
Apr 11, 2023
Posts
24,831
Reaction score
45,154
Nimewaza Vita ya Irani na Israeli na Kituko cha Mizinga 300 kutoleta Athari Kwenye Ardhi ya Israeli.

Inawezekanaje Siraha hevy za moto zaidi ya 300? Sio kwamba Irani na Israel wana lao moja?

Hawa Wayahudi na Waajemi wan Undugu wa Kiroho Tangu zamani.

Nikurudishe nyuma kidogo.

Mambo mema ambayo Irani (Waajemi) waliwatendea Wayahudi hapo zamani za kale.

1. Wayahudi walipokuwa wametekwa ndani ya Babeli chini ya Nebkadineza na baadae Mwanaye Belshaza walipata nafuu ya Utumwa kwa Mfalme Koreshi Mwajemi kuiangusha Babeli.

2. Baada ya Koreshi alishika madaraka Mfalme wa Uajemi King Darius( Dario) huyu Mwamba aliandika nyaraka Ikulu akaifadhi ikieleza kuwa baada ya kipindi cha miaka fulani wayahudi waachiwe warudi kwao Yesrusalem kuujenga mji wao uliobomorewa na Nebkadneza miaka 600BC.

3. Tukio lingine ni lile la Mfalme Dario kuwaua Mawaziri na Baraza loote la maliwali alipogundua kuwa walimdanganya kwamba Daniel alikuwa Mhaini asiyetii sheria za Uajemi ambazo zilikuwa Infaliable( yaani hazitenguki). Maliwali walikula kibano cha kufa mtu wao na watoto wao na wake zao wakatupwa kwenye shimbo la Simba zikawasasambua asibaki hata mmoja. Wakati huo Daniel akiwa ndiye Waziri Mkuu Uajemi( imagine Mkimbizi tu)

4. Baada ya Mfalme Dario aliingia Ahasuero, huyu Mwamba alikuta nakala ya Barua iliyoandikwa na kuagiza Wayahudi waruhusiwe kurudi kwao na akatekeleza. Ahasuero akampa barua ya Ruhusa Ezra akiwa na wenzake akina Yoshua, Hagai Nabii, Modekai, Delaya na Zerubabeli wakaenda kuanza ujenzi. Kitu kikubwa ktk Ruhusa hii ni kwamba Ahasuero aliagiza maliwali waliokuwa pande za Siria na Jordani na ng'ambo ya Mto(West Bank) wahakikishe Waisraeli hawasumbuliwi. Soma Kitabu cha Ezra, 1,2 hadi sura ya 6. Mfalme anaagiza ikiwa watapungukia basi wakuu wa mikoa inayozunguka israeli wahakikishe wanachukua sehemu ya Kodi wawahudumie wayahudi wasipate tabu.

5. Kule Jordan wakajitokeza wabishi akina Sanbalati, Tobia, Geshem Mwarabu kutaka kuleta bugudha na kejeli wakadhibitiwa na Waajemi.

6. Baada ya Ahasuero alifata Mfalme Atashasta kipindi cha Nabii Nehemia, mwendo ukawa ule ule. Katika mwaka wa 20 wa kutawala kwake Atashasta Kamanda wa Jeshi na Intelijensia Hamani akazinyaka taarifa kwamba Kuna Wayahudi hawataki kuitii serikali na mamlaka ya Uajemi( kosa la uhaini). Waliotuhumiwa ni akina Modekai na wayahudi woote(wakimbizi). Kwa kujipendekeza Kamanda Hamani akapanga kuwaua wayahudi wote akianza kumtundika Juu ya Mti Modekai ili washenzi wengine wajifunze. Lahaulaa! Kibao kikageuka Hamani akatundikwa Yeye na Wayahudi hawakufanywa kitu. Walaka uliotolewa kwa maliwali wote na wakuu wa mikoa ukafutwa na wayahudi wasibudhudhiwe.

7. Basi Nehemia na kina Zerubabeli wakafunga msafara wa pili( second importation) wa kurudi kwao wakapewa ulinzi na pesa kutoka kwa Mfalme wa Uajemi.
Kwa hiyo kwa nyakati zote za uhai wa Israeli na Uajemi hawa watu wamekuwa ndugu. Sio undugu wa kikabila bali wa kiroho.

Unaposikia Kuna Mizinga na drone za kibabe 300 zimepiga na hakuna madhara yoyote yaliyotokea usishangae ktk Ulimwengu huu wa Propaganda.
 
Acheni kuandika vitu msivyovijua, hiyo Israel iliyopo sasa pale mashariki ya kati sio Israel iliyokuwepo hapo kale ilioandikwa katika vitabu vya dini kama Biblia na Quran.

Israel iliyopo sasa ni sinagogi la shetani au khazarian Tribe.

Hao wanaojiita waisrael waliopo mashariki ya kati ni mazayuni yanayoandaa mazingira ya mpinga kristo wakishirikiana uingereza(6), marekani(6) na hao mazayuni(6) wenyewe waliopo sasa hapo mashariki ya kati.

Tafuta historia ya khazarian Tribe (Ashkenazi Jews) utaelewa hasa chanzo chao na mission zao hapa duniani.
 
Umeeleza historia za bc na ac, zilizopendwa.
Taifa la Israel hadi sasa limeshapigana na kila nchi zinazoizunguka. Ameshapigana na wairan zaidi ya mara 3. Kila baada ya miaka 4 lazima atwangane na jiran yake. Jana hata jiran mmoja wanayependana nae, kwasababu muisrael anajiamini yeye ndiye taifa teule na muhimu kuliko yeyote duniani. Kama kupigana na Iran, kitawaka tu. Sio Iran pekee, bali nnchi zote zinazoizunguka Israel patachimbika.

Ushahidi List of wars involving Israel - Wikipedia
 
Shida yako unajaribu kuchambua siasa za kimataifa kwa kutumia kitabu cha kale. Mbaya zaidi icho kitabu wenzako hata kukiamini hawakiamini. Izo kombora za iran kutokua na madhara ni kitu ambacho kimeshatolewa ufafanuzi. Iran wenyewe hawakutaka izo kombora zilete madhara makubwa ili israel isipate sababu ya kujibu tena mashambulizi yani iran ilitaka vita iishie hapa. Kila mmoja awe kampiga mwenzie kofi 1( israel kupiga ubalozi wa iran na iran kalipiza kwa kurusha makombora kwa israel)
 
Acha kuandika Hisia zako.
 
Nimejaribu kuconnect dot tu
 
Unaandika vitu usivyovifahamu dogo. Unakaa sana vijiweni kusikiliza porojo.
 
Shida yako unajaribu kuchambua siasa za kimataifa kwa kutumia kitabu cha kale. Mbaya zaidi icho kitabu wenzako hata kukiamini hawakiamini. Izo kombora za iran kutokua na madhara ni kitu ambacho kimeshatolewa ufafanuzi. Iran wenyewe hawakutaka izo kombora zilete madhara makubwa ili israel isipate sababu ya kujibu tena mashambulizi yani iran ilitaka vita iishie hapa. Kila mmoja awe kampiga mwenzie kofi 1( israel kupiga ubalozi wa iran na iran kalipiza kwa kurusha makombora kwa israel)

Hapa nimekulewa Iran wame behave kiutu uzima. Ile ya tema mate tumpige....
 
Msichok8elewa nimkuwa Iran kafikishabujumbe.

Missiles za engine za honda xilikua ni decoy tu za kuwatia hasara mazayuni, missile zilizotakiwa zipige zimepiga na hakuna aliyeweza kuzizuwia.
 
Kumbuka pia Ni Iran iliyoamuru wayahudi wote wauwawe. Enzi za Malkia Ester. Na waliwahi kuandika waraka hairuhusiwi kujenga chochote israel enzi hizo (Yuda) ikiwa ni magofu.
Waajemi Ndio hao walitaka kuwaua kwa Amiri ya Amiri Jeshi Hamani. Mfalme wa wakati huo Atashasta akasikiliza Hoja za Ester akapiga Marufuku walaka uliotolewa kila Mkoa kwa ajili ya kutekeleza.
 
Msichok8elewa nimkuwa Iran kafikishabujumbe.

Missiles za engine za honda xilikua ni decoy tu za kuwatia hasara mazayuni, missile zilizotakiwa zipige zimepiga na hakuna aliyeweza kuzizuwia.
Iran sio waarabu wenzako lakini. Ni hilo tu.
 
Waajemi Ndio hao walitaka kuwaua kwa Amiri ya Amiri Jeshi Hamani. Mfalme wa wakati huo Atashasta akasikiliza Hoja za Ester akapiga Marufuku walaka uliotolewa kila Mkoa kwa ajili ya kutekeleza.
Hakukuwa na urafiki. Iran ilikuwa ni watawala na Wayahudi walikuwa ni watumwa na vibarua wao tu ambao kwa kauli moja wanaweza kufutwa wote
 
Back
Top Bottom