Irene Uwoya awachamba watangazaji wa xxl na mashabiki wanaomfuatilia

Irene Uwoya awachamba watangazaji wa xxl na mashabiki wanaomfuatilia

Lord Diplock MR

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2015
Posts
1,393
Reaction score
3,237
Siku ya leo clouds FM kwenye show yao ya xxl walikuwa na mahojiano na Dogo Janja na katika mahojiano waligusia ndoa ya Dogo Janja na Irene Uwoya katika madai yao watangazaji Adam Mchomvu na Dozen walidai Irene Uwoya amemwacha Dogo Janja na hivi sasa yupo Dubai.

Ili kuwathibitishia kuwa bado wapo pamoja Dogo Janja aliamua kumpigia Irene Uwoya live wakiwa on air na kumpa aongee na akina Adam Mchomvu na Dozen kitendo hicho kilimkasirisha Uwoya aliyewavaa watangazaji hao kwa kuwaambia wafanye mambo yao na kwamba wao na Dogo Janja wapo pamoja. Uwoya amesema kwamba yeye kutokwenda na Dogo Janja Dubai ni kutokana na Dogo Janja kuwa na ratiba zake.

Uwoya ambaye kwasasa yupo nchini toka juzi, akiongea kama mtu aliyekasirika aliwataka watangazaji hao pamoja na mashabiki kufanya mambo yao kwa aibu Adam Mchomvu akajibu akijikongoja "tunafanya mambo yetu kwani lazima tuongee hewani?"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
bado mnao huo muda wa kusikiliza radio kumbe
 
Back
Top Bottom