Iringa: Adaiwa kumbaka mjamzito na kumsababishia umauti

Iringa: Adaiwa kumbaka mjamzito na kumsababishia umauti

0897

Member
Joined
Feb 25, 2022
Posts
39
Reaction score
92
Jeshi la Polisi Mkoani Iringa linamshikilia Mohamed Mwanjali mkazi wa Mtaa wa Kitanzini kwa tuhuma za kumbaka Mama mjamzito na kumsababishia umauti.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Maweni Kata ya Kitanzini Yassin Kisogole amesema Mwanamke huyo alitendewa ukatili huo usiku wa kuamkia September 25,2022 wakati Mumewe akiwa Mtaa wa jirani alipokwenda kushuhudia pambano la ndondi la Mandonga vs Abeid kisha la Twaha Kiduku vs Abdo kupitia TV.

Shemeji wa Marehemu aitwaye Prosper Kileo amesema Mume huyo aliporudi nyumbani baada kuangalia pambano la ngumi alipofika mlangoni alikuta mlango upo wazi wakati akiingia ndani alimuona Mtuhumiwa akitoka katika moja ya chumba na kukimbia ndipo alipojaribu kumkimbiza bila mafanikio.

Alipoingia ndani alimkuta Mtoto wa Marehemu mwenye umri wa miaka mitano ambaye alimmsimulia kwa kumwambia "Baba alikuja Mtu hapa akamziba Mama mdomo akamuangusha chini"

Baada ya taarifa hizo Mume huyo wa Marehemu alienda kutoa taarifa Polisi, taarifa za awali zinadai Mtuhumiwa alikuwa na ugomvi na Marehemu kutokana na kumripoti katika mamlaka za usalama kwa tabia za wizi, Mtuhumiwa amekamatwa na Polisi nyumbani kwake ambako amekutwa na baadhi ya vitu vya Marehemu ikiwamo simu ya mkononi na nguo (suti) ambazo alizichukua mara baada ya kutekeleza tukio hilo.

Source: Millard Ayo
 
Daah aiseee mambo yamekua mengi. Jela zinajaa wangemgeuza panyaroad na kummaliza hapo hapo walipomkamata
 
Mtuhumiwa alikuwa na ugomvi na Marehemu kutokana na kumripoti katika mamlaka za usalama kwa tabia za wizi, Mtuhumiwa amekamatwa na Polisi nyumbani kwake
Sasa angalia hapa mtu km huyu akipelekewa chuma cha Moto kwenye ubongo watu wataanza kulalamika hapa unaona unyama aliofucha huyu kiumbe?

Kuna mjinga mmoja ataanza kumtetea kwamba hivi na hivi na vile eeeenhe wakipigwa na manati ya mzungu mnaanza kupiga kelele hamuoni huyu mpuuzi ameshashindikana huyu ni wa kutembezewa chuma tu akapumzike akipelekwa mahakamani anapigwa miezi 6 baada ya hapo yupo uraiani tena anabaka mama mjamzito mwingine anajua atakamatwa atapelekwà jela mda ukiisha atatoka atakuja kubaka tena hio ndio routine yake suluhu ni kumpumzisha kwa kumpelekea chuma akajielezee huko mbele ya Safari sio kumchekea

Pigwa chuma watu wote wenye tabia km hizi waishe wapigwe tu na manati ya mzungu wote waishe

Pole sana marehemu
Starehe kwa amani..
 
Alieua ni huyo hapo hapa iringa wanamwita muddy MT kiufup huyu dogo ni jambazi na kibaya zaid askar wanamjua kuwa ni mwizi lakn akikamatwa anatoka,huyu dogo yuko vizur kimazoez weng waliobiwa na huyu dogo haswa wanafunz wa vyuo wanaoenda club wanameng yakusimulia ana ngumi jiwe na anaruka vichwa kama mshale,huyu alikua akimlawiti dogo mmoja wa kitanzin ikatokea huyo dogo mama ake anatembea na askar mama mtu kujua mwanae analawitiwa akaenda kushtaki dogo akawekwa ndani mwez haujaisha akarud mtaa,aliwah kumbaka mdada wa guest dada alipoanza kupiga kelele akamkaba dada akamminya makende jamaa akamwachia dada akakimbia jamaa akamkatia denge uzur dada aliwah kufika geti la guest anayofanyia ile anaingia tu akala tofali la kichwa akazimia jamaa akasepa,kiufupi dogo alishindikana na eneo analotokea(kitanzini) ni eneo korofi kihistoria mana majambazi,wehu,mabondia wanapatkana huko,bangi,unga,mirungi...serikal ya mtaa inamjua kama ni mwizi,polis wanamjua pia lakn alikua hakai ndani muda anatoka licha ya uhalifu aliokua anaufanya lilikua ni suala la muda tu
 
Attachments

  • FB_IMG_1664293444792.jpg
    FB_IMG_1664293444792.jpg
    14.1 KB · Views: 17
  • FB_IMG_1664293259484.jpg
    FB_IMG_1664293259484.jpg
    36.7 KB · Views: 17
Kifo ni halali yake.hafai kuendelea kupumua alipaswa hadi sasa atangulie ahera...amechelewa.
 
aisee inafikirisha kwa kweli mbona matukio ya hivi yamekuwa mengi
 
Kifo ni halali yake.hafai kuendelea kupumua alipaswa hadi sasa atangulie ahera...amechelewa.
Hapana kumuua ni kumpunguzia adhabu, achomekwe vyuma vyuma kila kwenye mfupa...usiku asipewe blanketi, vyuma vikipata baridi atakuwa analia kila usiku mpaka uzee wake
 
Alieua ni huyo hapo hapa iringa wanamwita muddy MT kiufup huyu dogo ni jambazi na kibaya zaid askar wanamjua kuwa ni mwizi lakn akikamatwa anatoka,huyu dogo yuko vizur kimazoez weng waliobiwa na huyu dogo haswa wanafunz wa vyuo wanaoenda club wanameng yakusimulia ana ngumi jiwe na anaruka vichwa kama mshale,huyu alikua akimlawiti dogo mmoja wa kitanzin ikatokea huyo dogo mama ake anatembea na askar mama mtu kujua mwanae analawitiwa akaenda kushtaki dogo akawekwa ndani mwez haujaisha akarud mtaa,aliwah kumbaka mdada wa guest dada alipoanza kupiga kelele akamkaba dada akamminya makende jamaa akamwachia dada akakimbia jamaa akamkatia denge uzur dada aliwah kufika geti la guest anayofanyia ile anaingia tu akala tofali la kichwa akazimia jamaa akasepa,kiufupi dogo alishindikana na eneo analotokea(kitanzini) ni eneo korofi kihistoria mana majambazi,wehu,mabondia wanapatkana huko,bangi,unga,mirungi...serikal ya mtaa inamjua kama ni mwizi,polis wanamjua pia lakn alikua hakai ndani muda anatoka licha ya uhalifu aliokua anaufanya lilikua ni suala la muda tu
Yaani kambegu kadogo haka kanasumbua iringa yote? Duh...
 
Back
Top Bottom