Iringa: Adaiwa kumbaka mjamzito na kumsababishia umauti

Iringa: Adaiwa kumbaka mjamzito na kumsababishia umauti

hii ndio aina ya watanzania ambayo wanaharakati wa chadem wanataka wasiuawe na polisi mahakama ifanye kazi yake.

polisi ina kazi nyingi.
 
Jeshi la Polisi mkoani Iringa linamshikilia mkazi wa Manispaa, Mohamed Njali, kwa tuhuma za kumdhalilisha kijinsia mama mjamzito, Atka Kivenule na kumsababishia kifo chake.

Tukio hilo limetokea Jumamosi usiku mtaa wa Maweni, kata ya Kitazini/Myomboni ambapo mtuhumiwa huyo alivamia nyumbani kwa Adeline Kileo, saa 5 usiku.

Kamanda wa Polisi mkoani humo, Allan Bukumbi, alikiri kutokea kwa tukio hilo na wanaendelea na uchunguzi ili kujua sababu za mauaji hayo.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa, Alfred Mwakalebela amethibitisha kupokea mwili wa mwanamke anayedaiwa kubakwa hadi kufariki akiwa na ujauzito wa wiki 10.

“Inasemekana alikuwa amelala ndani akavamiwa na mtu na katika uchunguzi tumegundua alivunjwa koromeo tulikuta michubuko inaonekana mbakaji alikuwa akimnyonga shingo ili atimize azma yake,’ alisema Mwakalebela.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi amethibitisha kutokea tukio hilo na kwamba, uchunguzi zaidi unaendelea.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Mohamed Moyo alisema mtuhumiwa amekamatwa na kuwa Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi kwa hatua zaidi.

Moyo alisema hajafurahishwa na matukio ya ukatili yanayoendelea mkoani hapo na kusema inahitajika nguvu ya pamoja kati ya Serikali, wananchi na wadau mbalimbali katika kupiga vita matendo hayo ya udhalilishaji wa kijinsia.
“Tunawaomba viongozi wa dini waendelee kuzungumza na waumini wao, kubwa zaidi wajue kumtanguliza Mungu, wabunge wawe na ajenda ya kudumu ya kukemea masuala ya udhalilishaji, ubakaji, mauaji na kuondokana na imani za kishirikina kwamba wakibaka au kuua watapata utajiri,” alisema Moyo.

Kwa upande wake, Balozi wa mtaa wa Maweni, Yasin Kisogwe alisema aliletewa taarifa hizo za kusikitisha kuwa amevamiwa katika nyumba yake na mkewe kubakwa hadi kufa.

“Kwa kushirikiana na jeshi la polisi, tulikwenda nyumba ya mtuhumiwa na alikamatwa na kuwekwa chini ya ulinzi na kuanza kufanya upekuzi nyumbani kwake na ilipatikana simu ya marehemu,” alisema.

Akizungumza kwa majonzi, mume wa marehemu, Adeline Kileo alisema siku ya tukio mke wake alitoka kazini kutokana na hali yake ya ujauzito alimuomba mumewe amsaidie kupika.

Alisema baada ya kumaliza kula yeye na kaka yake walirudi dukani kuendelea na biashara kisha wakaenda kuangalia “pambano la ngumi la Mandonga.”

Alisema wakiwa katika mgahawa wanaangalia pambano mtuhumiwa alimfuata na kumwambia “mkeo ni mzuri sana, jirani ana shepu hatari.”

Kileo alisema, baada ya kusikia anazungumza maneno hayo, “sikuyapenda nikampoteza na kuendelea kuangalia ngumi mimi na wenzangu.”

Alisema, baada ya kutoka kuangalia pambano la ngumi, alishangaa kukuta milango ya nyumba yake ipo wazi na kuingia ndani hakuamini macho yake alipomwona mkewe akiwa amelala kitandani kifudifudi akiwa uchi wa mnyama.

“Nikamuita mtoto hakuitika, sikumpata sehemu yeyote, ndipo tukaamua kumchukua mke wangu kumpeleka hospitali ya jirani ambapo tuliambiwa ameshafariki” alisema.

“Alikuwa ni mjamzito wa miezi miwili, naliomba Jeshi la Polisi litusaidie kupata haki na kutoa adhabu kali kwa watuhumiwa wa matukio haya ili yasiendelee kwa familia nyingine au watu wengine kufanyiwa,” alisema.

Chanzo: Mwananchi
 
Inasikitisha sana, sheria ifuate mkondo wake...
 
Dah jamaa anajuta asingeenda angalia ngumi, angemwitia hata mwizi wampopoe mawe wakati anamkimbiza
 
Jeshi la Polisi Mkoani Iringa linamshikilia Mohamed Mwanjali mkazi wa Mtaa wa Kitanzini kwa tuhuma za kumbaka Mama mjamzito na kumsababishia umauti.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Maweni Kata ya Kitanzini Yassin Kisogole amesema Mwanamke huyo alitendewa ukatili huo usiku wa kuamkia September 25,2022 wakati Mumewe akiwa Mtaa wa jirani alipokwenda kushuhudia pambano la ndondi la Mandonga vs Abeid kisha la Twaha Kiduku vs Abdo kupitia TV.

Shemeji wa Marehemu aitwaye Prosper Kileo amesema Mume huyo aliporudi nyumbani baada kuangalia pambano la ngumi alipofika mlangoni alikuta mlango upo wazi wakati akiingia ndani alimuona Mtuhumiwa akitoka katika moja ya chumba na kukimbia ndipo alipojaribu kumkimbiza bila mafanikio.

Alipoingia ndani alimkuta Mtoto wa Marehemu mwenye umri wa miaka mitano ambaye alimmsimulia kwa kumwambia "Baba alikuja Mtu hapa akamziba Mama mdomo akamuangusha chini"

Baada ya taarifa hizo Mume huyo wa Marehemu alienda kutoa taarifa Polisi, taarifa za awali zinadai Mtuhumiwa alikuwa na ugomvi na Marehemu kutokana na kumripoti katika mamlaka za usalama kwa tabia za wizi, Mtuhumiwa amekamatwa na Polisi nyumbani kwake ambako amekutwa na baadhi ya vitu vya Marehemu ikiwamo simu ya mkononi na nguo (suti) ambazo alizichukua mara baada ya kutekeleza tukio hilo.

Source: Millard Ayo
Mohamed Mwanjali mkazi wa Mtaa wa Kitanzini kwa tuhuma za kumbaka Mama mjamzito na kumsababishia umauti.

Cc adriz Mlolongo Dalmine Accumen Mo
 
Alieua ni huyo hapo hapa iringa wanamwita muddy MT kiufup huyu dogo ni jambazi na kibaya zaid askar wanamjua kuwa ni mwizi lakn akikamatwa anatoka,huyu dogo yuko vizur kimazoez weng waliobiwa na huyu dogo haswa wanafunz wa vyuo wanaoenda club wanameng yakusimulia ana ngumi jiwe na anaruka vichwa kama mshale,huyu alikua akimlawiti dogo mmoja wa kitanzin ikatokea huyo dogo mama ake anatembea na askar mama mtu kujua mwanae analawitiwa akaenda kushtaki dogo akawekwa ndani mwez haujaisha akarud mtaa,aliwah kumbaka mdada wa guest dada alipoanza kupiga kelele akamkaba dada akamminya makende jamaa akamwachia dada akakimbia jamaa akamkatia denge uzur dada aliwah kufika geti la guest anayofanyia ile anaingia tu akala tofali la kichwa akazimia jamaa akasepa,kiufupi dogo alishindikana na eneo analotokea(kitanzini) ni eneo korofi kihistoria mana majambazi,wehu,mabondia wanapatkana huko,bangi,unga,mirungi...serikal ya mtaa inamjua kama ni mwizi,polis wanamjua pia lakn alikua hakai ndani muda anatoka licha ya uhalifu aliokua anaufanya lilikua ni suala la muda tu
Well explained
Alitakiwa apigwe chuma afe,
Tatiz mahakama zetu zinawalea sana wapuuz kama hawa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alieua ni huyo hapo hapa iringa wanamwita muddy MT kiufup huyu dogo ni jambazi na kibaya zaid askar wanamjua kuwa ni mwizi lakn akikamatwa anatoka,huyu dogo yuko vizur kimazoez weng waliobiwa na huyu dogo haswa wanafunz wa vyuo wanaoenda club wanameng yakusimulia ana ngumi jiwe na anaruka vichwa kama mshale,huyu alikua akimlawiti dogo mmoja wa kitanzin ikatokea huyo dogo mama ake anatembea na askar mama mtu kujua mwanae analawitiwa akaenda kushtaki dogo akawekwa ndani mwez haujaisha akarud mtaa,aliwah kumbaka mdada wa guest dada alipoanza kupiga kelele akamkaba dada akamminya makende jamaa akamwachia dada akakimbia jamaa akamkatia denge uzur dada aliwah kufika geti la guest anayofanyia ile anaingia tu akala tofali la kichwa akazimia jamaa akasepa,kiufupi dogo alishindikana na eneo analotokea(kitanzini) ni eneo korofi kihistoria mana majambazi,wehu,mabondia wanapatkana huko,bangi,unga,mirungi...serikal ya mtaa inamjua kama ni mwizi,polis wanamjua pia lakn alikua hakai ndani muda anatoka licha ya uhalifu aliokua anaufanya lilikua ni suala la muda tu
Polisi wa huko waige ule utaratibu wa huku Dar, piga shaba tu mbwa hao
 
Watani zangu wahehe mmekutwa na nini?

Yani mmeanza kuwa kama wanaume wa dar?[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]

Huyu mbwege mmoja ndio akiwekwa ndani, baada ya mwezi anatoka na mnamuangalia!!!!!!

Mmekua wapuuzi sana,
watu kama hawa ata kaburi huwa hakuna,
Ila mbinguni anakuwa amefika
 
Back
Top Bottom