Iringa: Idadi ya wanaume waliofanyiwa vitendo vya ukatili ikiwemo vipigo wilayani Mufindi imepungua

bongo dili

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2015
Posts
12,350
Reaction score
25,180
HABARI Idadi ya wanaume waliofanyiwa vitendo vya ukatili ikiwemo vipigo wilayani Mufindi mkoani Iringa, imepungua kutoka wanaume 811 mwezi Januari mwaka huu hadi kufikia wanaume 407 mwezi June.

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Dkt Linda Salekwa amesema kuwa hayo ni matokeo mazuri ya elimu inayoendelea kutolewa kwa wananchi jinsi ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia.

"Vipigo kwanaume vimepungua zaidi ya asilimia 50 imetoka 813 mpaka 407 lakini bado narudia kusema namba hii ni kubwa na tuna kazi ya kuhakikisha mimi na wewe tunazidi kupunguza," amesema DC huyo.

Chanzo: East Africa TV

==========

Maoni yangu:

Ujumbe toka chama cha wanaume wanaopigwa na wake zao nchini unawaasa wakina mama waache kuwapiga waume zao ikiwemo kuwafanyia ukatili wa jinsia yakiwemo maneno makali na machafu yanayochoma hisia na kupelekea wanaume kufa mapema kwa kushindwa kuyahimili.

Inayowafanya wawe wajane na kuishi maisha ya tabu mateso na watoto. Wanawake waache ukatili wa kijinsia wanazitesa bure familia wakiwa wao ndio wahanga wa madhara.

Ukimfanyia ukatili mwanaume ataikimbia nyumba na kwenda kuanza upya na mwanamke mwingine ampae amani na utulivu wanaoteseka ni watoto kukosa upendo wa baba.

Wanawake rejeeni kwenye misingi ya nafasi zenu kwenye ndoa nyie ni wasaidizi acheni kunyanyasa waume zenu kisa mnawalaumu michepuko eti kakukuchukulia mme,je unazikagua njia zako? Kazi ya mchepuko ni kuziba gap.Je unatosha Sio Kila mwanaume anao moyo wa kuvumilia maumivu.

Moyo wa mwanaume ni sawa na mkate. Utii ni Bora kuliko dhahabu,utii ni kwa faida yako mwanamke.
 
Wanawake wazidi kupewa elimu ndoa Sio uwanja wa mapigano na mashindano Bali ni kiwanda Cha amani na kuzalisha jamii yenye afya njema ya akili.
 
Childhood mates wa miaka ya 60-80 huwa hatuna kabisa mapenzi ya tamthilia za kifilipino ndiyomaana huwa tunaenjoy sana mapenzi na ndoa ingawa bila ya nguvu za kiroho (Mungu) ni sawa na kuufukuza upepo tu.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Hii ni hatari kwa huko shuleni walisomea kupigana.
Wapigwe tu kitendo cha mwanaume kuishi na kumtegemea mke wake hali ya kuwa mwanaume unao uwezo wa kupambana kutafuta unga ni upumbavu hiyo tabia wanayo wanaume wa iringa na mbaya na sumbawanga lazima wapigwe tu hakuna namna
 
Baba anaamka asubuhi anaenda kunywa pombe,mama anawaamsha watoto waende shule baadya hapo anashika njia ya kwenda shambani kurudi mpaka jioni. Akisharudi akatafute mboga na mahitaji mengine kwaajili ya mlo wa jioni.

Baba anavizia mchana anarudi nyumbani anauza mazao kwa bei chee ili akaendelee kunywa komoni na ulanzi,anazinywa pombe mpaka usiku.

Mama ameshawapikia watoto wamekula wanaenda kulala,usiku umeingia tayari baba anarudi home amelewa huku akitukana matusi makubwa makubwa na anaetukanwa si mwingine ni mkewe..'...fungua mlango'.

Mlango unafunguliwa anaulizwa kama alichota aidha maharage,njegere au mahindi kwasababu yeye ndyo ameshinda nyumbani. "Kwahyo unamaanisha mimi ndyo mwizi?.." matusi tena mke anatukanwa mpaka watoto wanaskia.

mpaka hapo kwanini mwanaume wa aina hyo asipigwe?
 
Wapigwe tu kitendo cha mwanaume kuishi na kumtegemea mke wake hali ya kuwa mwanaume unao uwezo wa kupambana kutafuta unga ni upumbavu hiyo tabia wanayo wanaume wa iringa na mbaya na sumbawanga lazima wapigwe tu hakuna namna
Wanaume wa dodoma pia bila kusahau singida pia wanayo.
 
Ujumbe toka chama cha wanaume wanaopigwa na wake zao nchini unawaasa wakina mama waache kuwapiga waume zao ikiwemo kuwafanyia ukatili wa jinsia yakiwemo maneno makali na machafu yanayochoma hisia na kupelekea wanaume kufa mapema kwa kushindwa kuyahimili.
Hivi dunia ya leo mtu mwenye akili timamu unang'ng'ania mwanamke usiyeheshimiana wala kuthaminiana naye wa kazi gani?!
 
Wengi wao ni kwa sababu wanaogopa watoto wasiumie
 
Childhood mates wa miaka ya 60-80 huwa hatuna kabisa mapenzi ya tamthilia za kifilipino ndiyomaana huwa tunaenjoy sana mapenzi na ndoa ingawa bila ya nguvu za kiroho (Mungu) ni sawa na kuufukuza upepo tu.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Wapigwe tu kitendo cha mwanaume kuishi na kumtegemea mke wake hali ya kuwa mwanaume unao uwezo wa kupambana kutafuta unga ni upumbavu hiyo tabia wanayo wanaume wa iringa na mbaya na sumbawanga lazima wapigwe tu hakuna namna
Sio wote wanalishwa na wanaawake
 
Hivi kweli mwanaume unapigwa na mkeo hadi unaenda kushtaki, hakuna mwanaume hapo.
 
HABARI Idadi ya wanaume waliofanyiwa vitendo vya ukatili ikiwemo vipigo wilayani Mufindi mkoani Iringa, imepungua kutoka wanaume 811 mwezi Januari mwaka huu hadi kufikia wanaume 407 mwezi June.

Mkuu wa wilaya ya Mufindi Dkt Linda Salekwa amesema kuwa hayo ni matokeo mazuri ya elimu inayoendelea kutolewa kwa wananchi jinsi ya kukabiliana na ukatili wa kijinsia.

"Vipigo kwanaume vimepungua zaidi ya asilimia 50 imetoka 813 mpaka 407 lakini bado narudia kusema namba hii ni kubwa na tuna kazi ya kuhakikisha mimi na wewe tunazidi kupunguza," amesema DC huyo.

Chanzo: East Africa TV

==========

Maoni yangu:

Ujumbe toka chama cha wanaume wanaopigwa na wake zao nchini unawaasa wakina mama waache kuwapiga waume zao ikiwemo kuwafanyia ukatili wa jinsia yakiwemo maneno makali na machafu yanayochoma hisia na kupelekea wanaume kufa mapema kwa kushindwa kuyahimili.

Inayowafanya wawe wajane na kuishi maisha ya tabu mateso na watoto. Wanawake waache ukatili wa kijinsia wanazitesa bure familia wakiwa wao ndio wahanga wa madhara.

Ukimfanyia ukatili mwanaume ataikimbia nyumba na kwenda kuanza upya na mwanamke mwingine ampae amani na utulivu wanaoteseka ni watoto kukosa upendo wa baba.

Wanawake rejeeni kwenye misingi ya nafasi zenu kwenye ndoa nyie ni wasaidizi acheni kunyanyasa waume zenu kisa mnawalaumu michepuko eti kakukuchukulia mme,je unazikagua njia zako? Kazi ya mchepuko ni kuziba gap.Je unatosha Sio Kila mwanaume anao moyo wa kuvumilia maumivu.

Moyo wa mwanaume ni sawa na mkate. Utii ni Bora kuliko dhahabu,utii ni kwa faida yako mwanamke.
Mi huwa naona kama ni mzaha mwanaume kunyukwa na mkewe na bila aibu kutoka hadharani na kuanza kulialia!
Hivi haya mambo ni kweli yapo au huwa tunalishwa siasa za maji taka?
 
Kwani ujawahi ona wanaume wanazikimbia nyumba zao unadhani kwa sababu gani kama sio manyanyaso na vipigo.
Wahanga ni wanaume wasomi,walioshika dini,waliolelewa familia zenye maadili, wanaume wapole na wastaarabu haya makundi yanateseka sana kwenye ndoa, kiasili wanawake wanapenda mwanaume dikteta mbabe mwenye sauti ndani ya nyumba wengine ngumi jiwe anajua akikuletea dakika sifuri anatoka damu.
Wanaume wengi hawasemi kuhusu ukatili wanaofanyiwa.
Ukitaka kuzijua Siri za ndani ulizia madada wa kazi wanajua Kila kitu na hata ukitaka kuoa
 
Dah!
 
Though wanawake wana midomo sana, ila kuna mambo yanafurahisha sana...
 
Back
Top Bottom