LGE2024 Iringa: Lukuvi kutoa Tsh. 500,000 kwa kijiji kitakachoongoza kuandikisha wananchi Uchaguzi Serikali za Mitaa

LGE2024 Iringa: Lukuvi kutoa Tsh. 500,000 kwa kijiji kitakachoongoza kuandikisha wananchi Uchaguzi Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Cute Wife

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2023
Posts
1,906
Reaction score
5,000
Wakuu,

Tumefikia huku, watu tumekuwa wazito kushiriki kwenye shughuli za uchaguzi na siasa kwa ujumla mpaka ka hela kahusike!

===

Mbunge wa jimbo la Isimani ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) William Lukuvi ameahidi kutoa zawadi kwa vijiji vitatu vitakavyofanya vizuri katika zoezi la kujiandikisha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.

Kupata matukio yote ya mkoa huu soma: Yanayojiri kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa Mkoa wa Iringa

Lukuvi ametoa kauli hiyo leo 19/October/2024 akiwa ziarani jimboni Isimani ambapo ametumia ziara hiyo kuhamasisha wananchi wa jimbo la Isimani kujitokeza katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la wapiga kura litakalohitimishwa kesho October 20, 2024.

Amesema kuwa atafuatilia mwenendo wa zoezi hilo katika tarafa tatu za jimbo la Isimani na kutoa zawadi kwa vijiji vitakavyofanya vizuri ambapo cha kwanza kitapata Shilingi 500,000 cha pili shilingi 300,000 na cha tatu shilingi 200,000


Pia soma: Uzi Maalum wa Vibweka na Hekaheka za wanasiasa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
 
Back
Top Bottom