Tumefikia huku, watu tumekuwa wazito kushiriki kwenye shughuli za uchaguzi na siasa kwa ujumla mpaka ka hela kahusike!
===
Mbunge wa jimbo la Isimani ambaye pia ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) William Lukuvi ameahidi kutoa zawadi kwa vijiji vitatu vitakavyofanya vizuri katika zoezi la kujiandikisha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa.
Lukuvi ametoa kauli hiyo leo 19/October/2024 akiwa ziarani jimboni Isimani ambapo ametumia ziara hiyo kuhamasisha wananchi wa jimbo la Isimani kujitokeza katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la wapiga kura litakalohitimishwa kesho October 20, 2024.
Amesema kuwa atafuatilia mwenendo wa zoezi hilo katika tarafa tatu za jimbo la Isimani na kutoa zawadi kwa vijiji vitakavyofanya vizuri ambapo cha kwanza kitapata Shilingi 500,000 cha pili shilingi 300,000 na cha tatu shilingi 200,000