0ozg Tz
JF-Expert Member
- Feb 28, 2016
- 4,155
- 11,168
Hata sijui mkuuPumziko la nani hilo
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Hata sijui mkuuPumziko la nani hilo
Chadema tuache vurugu,hadi akina mama mnawapiga?Kapigwa na nani?
Chadema tuache vurugu.CCM wana hofu hadi na wagombea hewa!
Kamanda asiyechoka kutoka CCM hi![emoji2772][emoji2772][emoji2772][emoji16]Chadema tuache vurugu.
Wewe, huyo ni raisi mtarajiwa. Heshima kwake mkuu.Huyo mgombea n pisi Kali,napenda anavyosuka simple (twende kilioni)
Teh teh [emoji23][emoji23][emoji23]Wanasiasa wanakuwa kama wasanii wanatafuta kiki akiona hasikiki anatafuta kiki za kujulikana
Hivi kumbe huwa wanapewa ulinzi na serikaliKwani wale walinzi wanaopewa na serikali waliokuwa wapi?
Haya matukio yamekua mengi mnooMGOMBEA urais wa chama cha ADC, Queen Sendiga adai kupigwa makofi na watu wasiojulikana na kuvunjiwa kioo cha gari lake akiwa katika maeneo ya stendi kuu ya zamani ya Manispaa ya Iringa kuendelea na mikutano yake ya hadhara ya kampeni .
Akizungumza mara baada ya tukio hilo leo mgombea huyo alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 10 jioni wakati akielekea katika viwanja vya Stendi kuu ya zamani ya mabasi yaendayo mikoani eneo ambalo pia chama cha mapinduzi (CCM) walikuwa na mkutano wa kampeni za mgombea wa udiwani kata ya Kitanzini Miyomboni .
Alisema kuwa jana kwa mujibu wa ratiba alikuwa ana mikutano yake ya kampeni katika mkoa wa Iringa katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa na asubuhi baada ya kuwasili Iringa alikutana na matangazo ya mgombea udiwani na ndipo alipotoa taarifa tume ya taifa ya uchaguzi kulalamikia suala hilo
" Mimi kabla ya kuwasilisha malalamiko mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi Bwana Mahela kuelezea vurugu ambazo nimekutana nazo jimbo la Iringa mjini niliendelea na ratiba zangu za kampeni za kuzunguka mitaano kama sokono na maeneo mengine kuomba kura japo tayari mgombea wangu wa nafasi ya ubunge jimbo la Iringa mjini Daud Masasi ambae pia ni kamishina wa ADC mkoa wa Iringa aliwasilisha malalamiko hayo kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini" alisema
Kuwa ameshangazwa na kusikitishwa na tukio la vijana kuvamia gari lake la matangazo na kuvunja kioo cha mbele cha gari hilo na wengine kumzingira na kumpiga makofi yeye wakati akihoji sababu ya gari lake kuvunjwa kioo wakati akielekea eneo hilo katika mkutano.
Hata hivyo alisema kuwa katika vurugu hizo gari la matangazo na vijana waliokuwepo katika gari hilo ndio ambao wameshambuliwa sana na yeye wameishia kumsukuma na kumzaba makofi wakati wa mvutano huo .
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alisema hajapata taarifa hizo zaidi ya kusikia kutoka kwa mwandishi hivyo anafuatilia
Naomba tuheshimiane.Kamanda asiyechoka kutoka CCM hi![emoji2772][emoji2772][emoji2772][emoji16]
Kwenye nyanja za ujasusi mtu kama wewe anaejifanya kuwa ni chadema wakati ni mamluki dhaifu kutoka CCM huwa anaitwa pandikiziNaomba tuheshimiane.
Mimi ni kamanda ninaetumia akili, sio pandikizi.Kwenye nyanja za ujasusi mtu kama wewe anaejifanya kuwa ni chadema wakati ni mamluki dhaifu kutoka CCM huwa anaitwa pandikizi
Wewe ni pandikizi dhaifu kutoka hapo Lumumba kwa sababu tulikugundua mapema sanaMimi ni kamanda ninaetumia akili, sio pandikizi.
Wewe hutumii akili,nipo ufipa hapa nafanya analysisi jinsi tu avyoshindwa.Wewe ni pandikizi dhaifu kutoka hapo Lumumba kwa sababu tulikugundua mapema sana
Kwa hiyo una watuhumu walinzi kuwa hawajulikani ama waliacha lindo lao!?Swali: Mpaka kupigwa makofi, je hakuwa na walinzi? Mtu apenye ampige makofi asikamatwe na walinzi? Muangalie sana huyu binti anatafuta "kiki" kwa niaba ya CCM
Mfumo wa siasa zetu umeruhusu uwepo wao hivyo wana haki ya kufanya kampeni kulingana na ratiba na si vinginevyo. Haya ya kuvunja vioo vya magari na kushambuliwa kwa kupigwa ni vitendo vya kihuni, kijinga na kishamba mno katika karne hii. Kwa bahati mbaya wanaojihusisha na uvunjifu huu wa amani wanajulikana ni wafuasi wa chama gani . Kila lenye mwanzo halikosi mwisho.Hutu tu vyama ni kichefu chefu tu hawa ndo hutumika kuangamiza wapinzani kamati ya maadili!! Hovyo sana hawa
Hongera Queen Sendiga kuteuliwa RC.MGOMBEA urais wa chama cha ADC, Queen Sendiga adai kupigwa makofi na watu wasiojulikana na kuvunjiwa kioo cha gari lake akiwa katika maeneo ya stendi kuu ya zamani ya Manispaa ya Iringa kuendelea na mikutano yake ya hadhara ya kampeni .