Uchaguzi 2020 Iringa: Mgombea Urais wa chama cha ADC, Queen Sendiga adai kupigwa makofi na watu wasiojulikana na kuvunjiwa kioo cha gari lake

Angekuwa kapigwa Lissu basi humu pangekuwa hapotoshi ila huyo mama anaambiwa et anatumika na ccm hivyo watu hawajali,Lissu aliisema ACT si chama cha upinzani bali ni chama ambacho kinatumika na serikali kuharibu upinzani ila et sasa Lissu anamuunga mkono mgombea wa ACT na anataka ACT imuunge mkono yeye mgombea wa chadema.

MiMi ndio maana naona kabisa hata huyu Chadema akishika dola hatokuwa na utofauti na ccm,maana mambo yao ni yaleyale tu.
 
MGOMBEA urais wa chama cha ADC, Queen Sendiga adai kupigwa makofi na watu wasiojulikana na kuvunjiwa kioo cha gari lake akiwa katika maeneo ya stendi kuu ya zamani ya Manispaa ya Iringa kuendelea na mikutano yake ya hadhara ya kampeni .

Akizungumza mara baada ya tukio hilo leo mgombea huyo alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 10 jioni wakati akielekea katika viwanja vya Stendi kuu ya zamani ya mabasi yaendayo mikoani eneo ambalo pia chama cha mapinduzi (CCM) walikuwa na mkutano wa kampeni za mgombea wa udiwani kata ya Kitanzini Miyomboni .

Alisema kuwa jana kwa mujibu wa ratiba alikuwa ana mikutano yake ya kampeni katika mkoa wa Iringa katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa na asubuhi baada ya kuwasili Iringa alikutana na matangazo ya mgombea udiwani na ndipo alipotoa taarifa tume ya taifa ya uchaguzi kulalamikia suala hilo

" Mimi kabla ya kuwasilisha malalamiko mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi Bwana Mahela kuelezea vurugu ambazo nimekutana nazo jimbo la Iringa mjini niliendelea na ratiba zangu za kampeni za kuzunguka mitaano kama sokono na maeneo mengine kuomba kura japo tayari mgombea wangu wa nafasi ya ubunge jimbo la Iringa mjini Daud Masasi ambae pia ni kamishina wa ADC mkoa wa Iringa aliwasilisha malalamiko hayo kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini" alisema

Kuwa ameshangazwa na kusikitishwa na tukio la vijana kuvamia gari lake la matangazo na kuvunja kioo cha mbele cha gari hilo na wengine kumzingira na kumpiga makofi yeye wakati akihoji sababu ya gari lake kuvunjwa kioo wakati akielekea eneo hilo katika mkutano.

Hata hivyo alisema kuwa katika vurugu hizo gari la matangazo na vijana waliokuwepo katika gari hilo ndio ambao wameshambuliwa sana na yeye wameishia kumsukuma na kumzaba makofi wakati wa mvutano huo .

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alisema hajapata taarifa hizo zaidi ya kusikia kutoka kwa mwandishi hivyo anafuatilia
Haya matukio yamekua mengi mnoo
 
Swali: Mpaka kupigwa makofi, je hakuwa na walinzi? Mtu apenye ampige makofi asikamatwe na walinzi? Muangalie sana huyu binti anatafuta "kiki" kwa niaba ya CCM
Kwa hiyo una watuhumu walinzi kuwa hawajulikani ama waliacha lindo lao!?
 
Hutu tu vyama ni kichefu chefu tu hawa ndo hutumika kuangamiza wapinzani kamati ya maadili!! Hovyo sana hawa
Mfumo wa siasa zetu umeruhusu uwepo wao hivyo wana haki ya kufanya kampeni kulingana na ratiba na si vinginevyo. Haya ya kuvunja vioo vya magari na kushambuliwa kwa kupigwa ni vitendo vya kihuni, kijinga na kishamba mno katika karne hii. Kwa bahati mbaya wanaojihusisha na uvunjifu huu wa amani wanajulikana ni wafuasi wa chama gani . Kila lenye mwanzo halikosi mwisho.
 
MGOMBEA urais wa chama cha ADC, Queen Sendiga adai kupigwa makofi na watu wasiojulikana na kuvunjiwa kioo cha gari lake akiwa katika maeneo ya stendi kuu ya zamani ya Manispaa ya Iringa kuendelea na mikutano yake ya hadhara ya kampeni .

Akizungumza mara baada ya tukio hilo leo mgombea huyo alisema kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 10 jioni wakati akielekea katika viwanja vya Stendi kuu ya zamani ya mabasi yaendayo mikoani eneo ambalo pia chama cha mapinduzi (CCM) walikuwa na mkutano wa kampeni za mgombea wa udiwani kata ya Kitanzini Miyomboni .

Alisema kuwa jana kwa mujibu wa ratiba alikuwa ana mikutano yake ya kampeni katika mkoa wa Iringa katika halmashauri ya Manispaa ya Iringa na asubuhi baada ya kuwasili Iringa alikutana na matangazo ya mgombea udiwani na ndipo alipotoa taarifa tume ya taifa ya uchaguzi kulalamikia suala hilo

" Mimi kabla ya kuwasilisha malalamiko mkurugenzi wa tume ya Taifa ya uchaguzi Bwana Mahela kuelezea vurugu ambazo nimekutana nazo jimbo la Iringa mjini niliendelea na ratiba zangu za kampeni za kuzunguka mitaano kama sokono na maeneo mengine kuomba kura japo tayari mgombea wangu wa nafasi ya ubunge jimbo la Iringa mjini Daud Masasi ambae pia ni kamishina wa ADC mkoa wa Iringa aliwasilisha malalamiko hayo kwa msimamizi wa uchaguzi jimbo la Iringa mjini" alisema

Kuwa ameshangazwa na kusikitishwa na tukio la vijana kuvamia gari lake la matangazo na kuvunja kioo cha mbele cha gari hilo na wengine kumzingira na kumpiga makofi yeye wakati akihoji sababu ya gari lake kuvunjwa kioo wakati akielekea eneo hilo katika mkutano.

Hata hivyo alisema kuwa katika vurugu hizo gari la matangazo na vijana waliokuwepo katika gari hilo ndio ambao wameshambuliwa sana na yeye wameishia kumsukuma na kumzaba makofi wakati wa mvutano huo .

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Juma Bwire alipotafutwa na mwandishi wa habari hizi kwa njia ya simu alisema hajapata taarifa hizo zaidi ya kusikia kutoka kwa mwandishi hivyo anafuatilia
Hongera Queen Sendiga kuteuliwa RC.
Pasco
 
Back
Top Bottom