Iringa: Mkuu wa Wilaya apiga marufuku vijana kushinda vijiweni

Iringa: Mkuu wa Wilaya apiga marufuku vijana kushinda vijiweni

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Serikali ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa imewataka vijana kupitia mradi wa Youth Agency Mufindi (YAM) kuunda vikundi vya kiuchumi ili kunufaika na mikopo isiyo na riba toka Halmashauri badala ya kukaa vijiweni bila kazi.

Rai hiyo ilitolewa jana Machi 9, 2022 na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Saad Mtambule wakati akizungumza na vijana 100 wanaotoka kwenye mazingira magumu Kata za Ihanu, Luhunga na Mdabulo wanaoendelea na mafunzo ya Afya ya Akili kwenye Ukumbi wa Yatima Igoda.

Mtambule aliwataka vijana hao kuunda vikundi na wale wenye ulemavu kuungana hata wawili ama mmoja kuomba mkopo.

Alisema Serikali ya Wilaya haitapenda kuona vijana wakizagaa mtaani ama kushinda vijiweni bila kazi na kuwa watakaokamatwa watafikishwa mbele ya vyombo vya sheria ili wafungwe gerezani wakafundishwe kufanya kazi huko.

Akielezea Kuhusu mafunzo hayo aliwataka vijana waliobahatika kuzingatia masomo hayo na kutokukatishwa tamaa na changamoto wanazokumbana nazo bali wajipe moyo na kuamini kuwa wakati wao wa kuinuka ni sasa hivyo hawana budi kukabiliana na changamoto hizo.

Aidha, aliwataka kutumia fursa hiyo ya mafunzo vizuri kwani serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu imejipanga vyema kuwainua na kuwasaidia wahitaji wote kutokana na kutenga fedha nyingi katika Halmashauri zao hivyo wanachotakiwa kufanya ni kujitambua.

Aliongeza kuwa baada ya kupata mafunzo hayo jambo la msingi ni kuyatekeleza kwani utekelezaji wao utapunguza mazingira ya vitendo vya uhalifu na ukatili wa kijinsia katika jamii zao huku akiwataka kuwatumia viongozi wao wakati wanapohitaji msaada

Mkuu wa Wilaya Iringa.jpg

Wakizungumzia baada ya mafunzo hayo wanufaika hao walisema wamejipanga vyema katika kuyapokea mafunzo kwani wanaamini ndoto zao za muda mrefu zitatimia lakini pia wataweza kumudu maisha yao pamoja na kuzikabili changamoto za maisha kwa ujumla.

Mwezeshaji wa mafunzo hayo, Dkt. Heriel Mfangavo alisema mafunzo hayo yamejikita katika kuwasaidia vijana namna ya kujitegemea katika nyanja zote ili waweze kujikwamua katika changamoto wanazozipitia lakini pia kujiinua kiuchumi kwa kufanya shuguli mbalimbali za ujasiriamali.

Dkt Mfangavo aliongeza kuwa vijana ambao wanastahili kukaa kwenye makundi baada ya mafunzo hayo wananufaika kwa kupata mikopo kutoka katika bajeti za halmashauri ambayo itawasaidia katika kuendeleza biashara zao lakini pia vijana ambao ni walemavu wanapewa kipaumbele cha kuweza kukopeshwa au kuingizwa kwenye fursa za ajira rasmi.

Meneja wa mradi wa YAM, Zilpa Mgeni alisema mradi huo unaendeshwa kwa ushirikiano na serikali na hivyo wanaishukuru serikali kwa kuonyesha ushirikiano wa hali ya juu na mradi wao ambao kiujumla una msaada mkubwa sana kwa vijana.

Pia aliiomba serikali kuzidi kutoa ushirikiano hasa kwa kusaidia kupatikana kwa mikopo hiyo ili wanufaika hao wapate mitaji na kuweza kujiendeleza kimaendeleo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi na Diwani wa Kata ya Luhunga, Festo Mgina aliwataka vijana hao kusikiliza vyema mafunzo hayo huku akiwaahidi kuwa pamoja na kuwahakikishia kupata mikopo baada ya mafunzo yao kutokana na serikali kujipanga vyema katika kuwasaidia wahitaji.

Chanzo: Matukio Daima blog
 
Mkuu wa wilaya ni moja ya nafasi ambazo wapowapo tu ofisini hawana kazi maana hana maamuzi hata ya fungu lolote pale halmashauri kwa ufupi ofisi yake ni kijiwe tu kama vijiwe vingine ndio maana ofisi za wakuu wa wilaya hawana ratiba ya kazi hufanya kazi kwa matukio
 
Kamati ya ulinzi na usalama anayoongoza DC pale hatakiwi kuwepo maana hana jeshi au kikosi chochote mambo ya usalama akiwepo DSO , OCD, TAKUKURU, Mkuu wa magereza, Mshauri wa mgambo kwa niaba ya jeshi la wananchi, kamati ya usalama ya madiwani, Mkuu wa uhamiaji, mkuu wa zimamoto, na mkuu wa uhifadhi wilaya hao wanatosha kabisa kwenye hiyo kamati DC au mkuu wa wilaya ni cheo ambacho hakitakiwi kuwepo maana hana kazi
 
Kwa mfano kwenye hiyo YAM aliyoenda DC alitakiwa aende Afisa Maendeleo ya jamii ambaye pia ni mtaalamu wa maendeleo aongee na vijana masuala ya kijamii na maendeleo
 
Back
Top Bottom