TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

Sir Leem

JF-Expert Member
Joined
Mar 14, 2008
Posts
584
Reaction score
125
Mwwenyekiti na Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Iringa na mwandishi wa habari wa Channel 10 amepigwa risasi na polisi kwenye mkutano wa CHADEMA Mufindi.
---
Mwandishi wa habari wa Channel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chama chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisi na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo.

Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi.

Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa kilitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa, Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo, ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini.

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa 'afande nimekufa' ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti.

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.

PIA SOMA
- Ripoti ya Kifo cha Mwangosi

Viongozi na Wanasiasa wengine waliowahi kupigwa risasi
VISA DHIDI YA WANAHABARI WENGINE WA TANZANIA:
 
Namjua kwa jina anaitwa Ndugu DAUDI MWANGOSI, hali yake ikoje na nini kimetokea?
 
Mwwenyekiti na chama cha waansishi wa habari mkoa wa iringa na mwandishi wa habari wa chanel 10 amepigwa risasi na polisi kwenye mkutano wa chadema mufindi

Can you believe the source?
 
Ni kama kuna thread moja iliandika jambo hili kama taarifa kuwa litatokea hili. Pole wafiwa na R.I.P mwandishi wa habari. Tusubiri polisi kulikanisha hili utasikia " rimarehemu rinepigwa na kitu chenye ncha kari". wapii.
 
Maisha ya watanzania - statistics!
 
Duh nimeumia sana taarifa hizi si njema sana wala si za kupuuzia
 
Huu mkakati ya serikali kupitia polisi ni MKAKATI HATARI. ITS WHAT WE CALL BAD POLITICS!
 
Ni kama kuna thread moja iliandika jambo hili kama taarifa kuwa litatokea hili. Pole wafiwa na R.I.P mwandishi wa habari. Tusubiri polisi kulikanisha hili utasikia " rimarehemu rinepigwa na kitu chenye ncha kari". wapii.

Thead hiyo ilikuwa na kichwa POLISI WANAJIPANGA KUUWA KWENYE MKUTANO WA CDM MUFINDI.
 
Sasa nimeamini wamepania kuimaliza cdm! Na hawataweza!
 
RPC atasema polisi hawatumii risasi za moto. Polisi itaunda tume kuchunguza. Polisi itatangaza yenyewe kama waliomuuwa nu CDM! Kila kitu wao!

Hata daktari atakayechunguza polisi ndiyo watatangaza matokeo!

By the way serikali ina jibu gani kwamba leo hii CCM wanafanya mkutano wao lakini CDM hapana.
 
Ni kama kuna thread moja iliandika jambo hili kama taarifa kuwa litatokea hili. Pole wafiwa na R.I.P mwandishi wa habari. Tusubiri polisi kulikanisha hili utasikia " rimarehemu rinepigwa na kitu chenye ncha kari". wapii.
is soo sad,huo uzi nanadhani upo na umeandikwa POLISI WAJIANDAA KUUA IRINGA
 
Haya! Walilia posho wa Nape jibuni hilo, msianze kuzungusha kama haziwatoshi vile!
 
Ni kama kuna thread moja iliandika jambo hili kama taarifa kuwa litatokea hili. Pole wafiwa na R.I.P mwandishi wa habari. Tusubiri polisi kulikanisha hili utasikia " rimarehemu rinepigwa na kitu chenye ncha kari". wapii.
Samahani kama sikuelewa, habari ni kuwa amepigwa risasi au ameuawa kwa kupigwa risasi? Tuache utani, yote si mema, lakini tafadhali tusiandike maneno mazito kama hayo wakati hatujapata taarifa zaidi za hali yake. Sina neno lolote mkuu Royals, ila naomba kabla hatujajua kilichotokea kwa dhati tusikimbilie kuandika R.I.P! Mkuu marejesho ameuliza Vipi hali yake? Naomba mwenye habari zaidi atupatie.
 
Amefariki dunia Daudi Mwangosi RIP my friend my brother Daudi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…