TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

Wadau mimi sina mengi ya kusema ila tu nikitafakari haya mauaji na ukatili huu unaoendelea dhidi ya raia najikuta nakumbuka historia ya aliyekuwa kiongozi wa ujerumani Adolf Hitler na kuanza kujiuliza kama hata hapa bongo amepatikana mtu kama yeye.

Hakuna hatua inayochukuliwa kwa wahusika kanakwamba wanayoyafanya yana baraka zote kutoka juu.

Kwakweli inauma sana na penginei kadri siku zinavyozidi kwenda tutapata jibu la swali hili.

Hivi huwa tuakwenda misikitini na makanisani kama fashion tu?

Wataficha ukweli wa mambo haya mpaka lini?

Tusuburi kwani ni vigumu sana kuficha ukweli.

Ni vigumu pia kuamini kama kweli haya matendo yanatokea hapa bongo.

Heri mzungu kuliko mkoloni mweusi.

Unamuita boyfriend yenu Hitler ?
 
Aiseee watoto wapo wapi?
Iringa ndo wapo!
Wakati nimeenda iringa 1 alikuwa chuo,2 secondary ,wa mwisho alikuwa mdogo km Drs la 2 hivi.
Wale wawili wote I think watakua wanamalizia chuo

Sshv yule mdogo atakuwa secondary Kuna msamaria mwema alimchukua.
 
Mwwenyekiti na Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Iringa na mwandishi wa habari wa Channel 10 amepigwa risasi na polisi kwenye mkutano wa CHADEMA Mufindi.
---
Mwandishi wa habari wa Channel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chama chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisi na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo.

Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi.

Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa hawapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa kilitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa, Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo, ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini.

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa 'afande nimekufa' ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti.

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.

PIA SOMA
- Ripoti ya Kifo cha Mwangosi

Viongozi na Wanasiasa wengine waliowahi kupigwa risasi
VISA DHIDI YA WANAHABARI WENGINE WA TANZANIA:
Miaka 12 imepita na matukio yanazidi kuongezeka.
God have mercy.
 
Iringa ndo wapo!
Wakati nimeenda iringa 1 alikuwa chuo,2 secondary ,wa mwisho alikuwa mdogo km Drs la 2 hivi.
Wale wawili wote I think watakua wanamalizia chuo

Sshv yule mdogo atakuwa secondary Kuna msamaria mwema alimchukua.
🙏🙏🙏 God Bless them 🙏🙏🙏
 
Back
Top Bottom