Halafu eti hela zinaenda kujenga sanamu ya mtu! Nyingine zinatumika kununulia Benzi la Rais Mstaafu, nyingine zinaenda kuwajengea Marais hao hao Wastaafu mahekalu ya kuishi!!
Yaani mtu amehudumu katika nafasi ya ubunge, uwaziri na baadae Urais kwa miaka lukuki, analipwa mafao ya 80% kila mwezi, halafu bado ananunuliwa gari, anajengewa nyumba ya kifahari na bado haitoshi, anajengewa mpaka sanamu!
Hakika Tanzania inahitaji Katiba Mpya haraka iwezekanavyo! Kuna mambo yanaleta sana maudhi.