Iringa: Wanne wadaiwa kufariki Dunia mgodini kwa kufukiwa na kifusi

Boran Jakutay

Senior Member
Joined
Apr 8, 2023
Posts
110
Reaction score
259
Watu wanne ambao ni wachimba madini, wamefariki kwa kufukiwa na kifusi cha mchanga katika eneo la machimbo ya madini ya dhahabu yaliyopo Kijiji cha Igomaa wilayani Mufindi mkoani Iringa, huku wengine watatu wakijeruhiwa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi, amethibitisha kutokea kwa vifo hivyo na kusema chanzo cha tukio hilo ni kutokana na mvua nyingi zinazoendelea kunyesha mkoani Iringa.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, ACP Allan Bukumbi amesema “Majina ya wanaodaiwa kufariki hayajapatikana kwa usahihi lakini tunafuatilia taarfa kupitia kwa Maafisa Madini kujua kama mgodi huo una leseni na wachimbaji wana kibali.


CHANZO: East Africa TV
 
Migodini ukiskia wamekufa wanne ujue hapo huenda ni zaid ya kumi wamekufa, taarifa huwa inapunguzwa makali shughuli ziendelee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…