Irone Dome - Uchawi wa mu-Israeli

Irone Dome - Uchawi wa mu-Israeli

Hezbollah yupo far more advanced kuliko Hamas
Hezbollah, Hamas wote wanapata backup toka Iran. Hezbollah wapo vizuri. Hamas walitegemea Nework tannel kama ngao, lakini naona kwa sasa Hamas wanakimbilia mashuleni na mahospitalini kujiokoa. Tunnel network ishazibitiwa tayari.

Vita ni mbaya sana, lakini Israel ni lazima afanye sasa - na kama akishidwa kuliangamiza kundi la HAMAS pale Gaza basi asahau milele.
 
Ukweli wa IDF kuhusu mashambulizi katika Hosptali kuu Gaza - Al-Shifa

Msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) Libby Weiss amekanusha kuwa vikosi vya IDF vinalenga raia huko Gaza, na anasema Hamas wanaendesha shughuli zao kutoka maeneo kama hospitali kwa ajili ya kijikinga (Shelter).

"Tunajua kabisa kwamba Hamas inatumia maeneo haya ya kiraia," aliambia kipindi cha Wikiendi cha BBC World Service hapo awali. "Tunajua hilo kwa uhakika. Tumetoa habari muhimu ambayo inazungumza hivyo."

Wizara ya afya inayoendeshwa na Hamas imeishutumu IDF kwa "kuzingira" hospitali ya Al-Shifa, ambayo ni eneo kubwa zaidi la matibabu huko Gaza. Alipoulizwa kuhusu operesheni katika eneo hilo, Weiss alisema: "IDF hailengi hospitali ya Shifa. Tunajibu moto unaozinduliwa na Hamas karibu na hospitali hiyo."

Weiss aliongeza kuwa Israel "inatumia rasilimali kubwa" ili kuepusha vifo vya raia, akirudia kusema kwamba "sio walengwa wetu"
 
Ata sioni cha kusifia hapo,kama Makombora yameundwa tu na kikundi cha watu ambao ujuzi wao ,nguvu kazi na financial resources ni haba yanawasumbua hivyo.
Je makombora ambayo yatakuwa yemeundwa na Nchi itakuwaje??
Israel si chochote si lolote. Ni propaganda tu.kama Israel inazo hizi sifa,kwa nn marekani anahangaika kutwa kucha anapeleka siraha Israel?
 
Mfumo wa ulizi wa Israel ni 55% kwa sofiscated weapons, kwa local made weapons uko 88% bado hapo hauwezi kutoa matokeo 100%, isreal kupewa nafasi ya 18 duniani kwa jeshi bora is over rated.
Ukiachana na Iron dome wana mfumo mwingine unaoitwa Arrow 3.

Halafu wana ule mpya unaitwa Iron Beam.
 
JF,

Kuwekeza kwenye elimu na uvumbuzi ni kitu muhimu sana kwa Taifa lolote lile, leo hii katika mifumo dhabiti duniani ya kutunguaji makombola kama utayataja basi huwezi kuiacha The Irone Dome ya wa Israel. Mfumo huu imesaidia sana kuyatungua makombola zaidi ya 5,000 yaliyotumwa ndani ya sekunde 20 na HAMAS siku ya uvamizi. Usahihi wa Irone Done ni zaidi ya asilimia 90. Kama yangetua yote basi leo Israel haingekuwepo kwenye uso wa Dunia hii, yangekuwa ni majivu.

Ulinzi wa Anga: Irone Dome imeundwa kwa sehemu kuu tatu: Gundua, Amua, Zima
Mfumo wa ulinzi wa anga una vipengele vitatu muhimu. Kwanza, kuna rada za kugundua, kutambua na kufuatilia makombora yanayoingia. Upeo wa rada hizi hutofautiana. Rada ya Iron Dome inafanya kazi kwa umbali wa maili 2.5 hadi 43.5 (km 4 hadi 70), kulingana na mtengenezaji wake Raytheon. Mara tu kitu kimegunduliwa na rada, lazima ichunguzwe ili kubaini ikiwa ni tishio. Taarifa kama vile mwelekeo na kasi hutumika kufanya uamuzi huu.

Ikiwa kitu kitathibitishwa kama tishio, waendeshaji wa Iron Dome wanaendelea kufuatilia kitu kwa rada. Kasi ya kombora inatofautiana sana, lakini ikichukulia kasi ya uwakilishi ya futi 3,280 kwa sekunde (km 1/s), mfumo wa ulinzi una angalau dakika moja kujibu shambulio.

Sehemu kuu ya pili ya mfumo wa ulinzi wa anga ni kituo cha udhibiti wa vita (battle control center). Kipengele hiki huamua njia inayofaa ya kuhusisha tishio lililothibitishwa. Inatumia taarifa ya rada inayoendelea kusasishwa ili kubaini jibu mwafaka katika suala la mahali pa kurusha makombora ya vipokea sauti na ngapi ya kurusha dhidi ya kombora linaloingia.

Sehemu kuu ya tatu ni kombora la kuingilia yenyewe (interceptor). Kwa Iron Dome, ni kombora la ajabu lenye vihisi joto. Vihisi hivi hutoa masasisho ya ndani ya ndege kwa kipokezi, kikiiruhusu kuelekea na kukaribia tishio. Kinasaji hutumia fuse ya ukaribu iliyowashwa na rada ndogo ili kulipuka karibu na kombora linaloingia ili isilazimike kuligonga moja kwa moja ili kulizima.





View attachment 2808407
Iron Dome,ipo kisaikolojia zaidi ya kivitendo,ntafafanua,ninaposema kisaikolojia nina maanisha serikali ya Israel imeweka mitambo ya kudengua makombora ya adui,unaoitwa Iron Dome ili kuwa Hadaa wananchi wake kwamba wako salama serikali inawajali kwa kuwalinda dhidi ya makombora ya adui,lakini kiuhalisia mtambo huo ulizidiwa uwezo Hamas walipo fire makombora 5000 hewani ndani ya dakika chache.
Kwa faida ya msomaji,wakati wa vita ya pili ya dunia (WW2),Serikali ya uingereza iliamua kujenga vizuizi vya mablock makubwa ya sementi ufukweni,kama yale unayoyaona kwenye barabara za mabasi ya mwendo kasi,halafu wakautangazia umma kwamba mablock hayo yanaweza kuzuia vifaru vya adui vitakavyoshushwa kwenye meli visiingie mjini,lengo haswa la serikali hiyo ilikuwa ni kuwateka wananchi wake kisaikolojia kuwa wako salama.
 
Dunia ielewe kwamba HAMAS bado wapo GAZA na wanaendelea kupigana na majeshi ya Israel, Hao jamaa wakishashambulia wanakwenda kujificha kwenye kambi za UN, Makanisani, Misitikini, Mahospitalini.

Hii vita ya namna hii ni ngumu sana, ukiwa na roho ndogo huwezi kupigana sababu HAMAS inatumia watu kama kinga.
Sasa IDF inaendeleza kushambulia popote ambapo wapiganaji hawa wapo bila kujali adhali za kibinadamu zinakazoteka.

More than 60 mosques ‘destroyed’ across Gaza​


According to the Wafa news agency, an Israeli aircraft bombed the al-Salam Mosque in the Sabra neighbourhood of Gaza City in the northern part of the besieged territory.
The destruction of al-Salam Mosque raised to more than 60 the total number of mosques destroyed by Israeli forces since October 7, the report said.
Places of worship qualify for protection as a cultural property under international humanitarian law.
 
kama Makombora yameundwa tu na kikundi cha watu ambao ujuzi wao ,nguvu kazi na financial resources ni haba yanawasumbua hivyo.
Je makombora ambayo yatakuwa yemeundwa na Nchi itakuwaje??

Hamas wanatumia silaha zinazopenyezwa yoka nchi muhisani ambayo mara nyingi huwa ni Iran...
 
Una hoja mkuu, mfano wapambane na Hezbollah (total war) yenye makombora 150,000 tena mengi ni 'precious guided missiles', hizo Iron dome lazima zizidiwe tu na miji yao mingi itaharibiwa.

Kiufupi hamna bado mfumo wa ulinzi ulio 100% 'perfect'.

T14 Armata
Hawana Irone dome moja kwa nchi nzima, zipo installed kadhaa na zinafanya kazi wa usahihi. Ukiwa na mfumo wa ulinzi ambao unadhibiti walau 60% ya kakombola basi wewe upo salama.

Fikiri, what if makombola yote 5,000 yangetua Israel siku ya uvamizi ingekuwaje kama si uimara wa mfumo huu.
 
Kwa namna waparestina wanavyopukutika aisee wanajuta kushangilia mauaji ya Wayahudi live kwenye TV zao siku ya mashambulizi October 7.

Kila nyumba, kanisa, msikiti, hospitali ambayo ina network ya underground tunnel inashughulikiwa kikamilifu na wayahudi. Underground tunnel zenye urefu wa zaidi ya km 500 zilizojengwa kwa zaidi ya miaka 20 sasa hivi imefaa vifusi, entry na exit points zote zaidi ya 1000 zishafumuliwa, kifupi imebakia historia.

Hawa wayahudi wana uzoefu na vita hizi, vinginevyo tungesikia wote walioingia ndani ya Gaza wanapukutika.
 
Technology yao is not appropriate au proportionate, hiyo ni poor military planning and badgeting kwa njia hiyo huwezi kusustain vita kwa mda mrefu, kama Urusi anavo fanya, huwezi kudungua drone ya $ 100 kwa kutumia kobora linalo rushwa na ndege ya F 16, its military foolishness and extravagant, ni sawa sawa kuwinda na kuua mbu na Ak 47......kwa hiyo Isreal hajajianda kwa vita ya mda mrefu watafilisika tu.

Ita depend na uchumi wa nchi husika ukoje. Kuna chi zina financial muscles hiko kitu si gharama kwao.
israel wasingeza kutumia mfumo kama hawawezi ku afford gharama zake
 
Baada ya IDF kutoa ushahidi wa wazi wazi kwamba hosptali ya al-Shifa inatumika na magaidi wa HAMAS, leo msaka mkali umefanyika chumba kwa chumba korido kwa korido huku watu wakiambiwa watokee kwenye milango ambayo imefungwa vifaa maalum vya detection.

Inaonekama magaidi hawa wanatumia hospital kama centre zao kijeshi (Commanding points)

Vita bado ni mbichi, ila waparestina kwa kweli wanajuta mno kuwakaribisha hawa HAMAS.
 
Netanyahu atoa msimamo mkali, Hatma ya HAMAS shakani.

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesisitiza lengo lake la kuwaondoa Hamas ameyasema hayo alipotembelea kambi ya mafunzo ya jeshi ya Zikim karibu na Gaza.

"Hakuna sehemu katika Gaza ambayo hatutafikia, hakuna maficho, kimbilio, au makazi ya wauaji wa Hamas," Netanyahu alisema, katika taarifa iliyochapishwa kwenye X.

"Tutafika, tutaondoa Hamas, na tutawarudisha mateka. Malengo haya mawili ni matakatifu… Jana, nilizungumza na Rais Biden tena. Hatafanya kazi bila kuchoka. Tutaondoa Hamas, kupata ushindi, na kuwarudisha mateka,” aliongeza.

Wanajeshi wa Israel kwa sasa wanavamia hospitali ya al-Shifa baada ya kudai kuwa boma hilo limeunganishwa na "miundombinu ya Hamas."
 
Back
Top Bottom