Is Diamond Platnumz good as he is au kuna mengine?? Mbinu za kutoboa kimataifa.

Ndio sababu ya Kiba kuto kutoa video ya nagharamia???
Sababu kumbe unataka na inaweza isitoke kabisaa yani labda letter 2016 director kagoma nayo umeridhika au bado??
 
Sijaridhika, mi ninachotaka ni video ya nagharamia sio mambo ya director yamekwenda yamerudi hayana ishu... Nadhani ni wakati muafaka wa kufanya maamuzi magumu, kutimua mameneja wooote maana hakuna la maana wanalofanya au we unaonaje mkuu? Weka mahaba pembeni, muheshimu msanii wako utaona anachofanya ni kinyume na anachostahili...!!
 
Huyu ndo walewale unaowasema vichwa mizigo kazi kuwaza majungu.....aisee nenda.mirembe....
 
Et mara waganha, mara freemason, mara ccm......hivi hao waganga wasanii wengine hawawaoni? Na nenda kaangalie viewer wa diamond kam utakuta ccm tupu bu th? way we wenyew unaesema koz yupo ccm umeangalia n'a unamsapoti je n'a w? ni ccm? Au wasanii wengine si ccm? Hapo vha msingi ni kujituma, mungu, wakati huu mziki kibiashara zaidi n'a Ye anacheza n'a soko, so soko laziki ni watu, anagharamia kazi kwa kuziandaa n'a kupromote ndani n'a nje, so unategemeaje w? kam Ali kiba anatoa nyimbo kam zamani nyimbo mwka huu vid?o mwakan, nani atamsapoti akati watu wanataka hivi Ye anafanya vile....tuwasapoti wasanii wetu kA yeyote anaetoa nyimbo nzuri n'a tusishabikie tu.....DIAMOND ANA JUHUDI N'A KAZI...KUNA MDA ANAFAIL VITU VYAKE LAKIN HAKATI TAMAA ANATAFUTA NJIA NYINGINE..
 
Sijaridhika, mi ninachotaka ni video ya nagharamia sio mambo ya director yamekwenda yamerudi hayana ishu... Nadhani ni wakati muafaka wa kufanya maamuzi magumu, kutimua mameneja wooote maana hakuna la maana wanalofanya au we unaonaje mkuu? Weka mahaba pembeni, muheshimu msanii wako utaona anachofanya ni kinyume na anachostahili...!!
Unaijua kwanza management ya ali kiba ?? Tuanze hapo
 
Et mara waganha, mara freemason, mara ccm......hivi hao waganga wasanii wengine hawawaoni? Na nenda kaangalie viewer wa diamond kam utakuta ccm tupu bu th? way we wenyew unaesema koz yupo ccm umeangalia n'a unamsapoti je n'a w? ni ccm? Au wasanii wengine si ccm? Hapo vha msingi ni kujituma, mungu, wakati huu mziki kibiashara zaidi n'a Ye anacheza n'a soko, so soko laziki ni watu, anagharamia kazi kwa kuziandaa n'a kupromote ndani n'a nje, so unategemeaje w? kam Ali kiba anatoa nyimbo kam zamani nyimbo mwka huu vid?o mwakan, nani atamsapoti akati watu wanataka hivi Ye anafanya vile....tuwasapoti wasanii wetu kA yeyote anaetoa nyimbo nzuri n'a tusishabikie tu.....DIAMOND ANA JUHUDI N'A KAZI...KUNA MDA ANAFAIL VITU VYAKE LAKIN HAKATI TAMAA ANATAFUTA NJIA NYINGINE..

Wanatapatapa mkuu
wamezoeleka hao
 
Naomba kwanza nianze kwa kudeclare interest, Mimi ni fan wa Diamond!

Ni fan wa Diamond si kwa sababu huwa napenda mziki wake at first place, Big NOOOOO! Nimejikuta nakuwa fan wa huyu jamaa kwa sababu mimi ni muumini wa Uzalendo ,ambao unanifanya niwe na shauku kubwa ya kuona jina la Tanzania linang'aaa zaid na zaid katika anga la kimataifa.

Napenda nyimbo zake ndiyo lakin si kwa uwingi na level ya kulinganisha navyo penda nyimbo za TID,Ben Paul,Marlow,Belle, Jux,Barnaba, Ibrah, Mangwair (RIP),MB Dog,Christian Bella na wengine wengi

Lakini mwisho wa siku najikuta tu nakubali kuwa He is the best, na ndo King wa hii industry na hii industry haikuwah pata mtu kama yeye (Mr Nice records considered well)

At the same time, Najisikia vibaya pale ambapo Wajasiriamali wabunifu wa Mfano Kenya na Rwanda, wanang'aa zaid katika international spot light kuliko vijana wetu wabunifu wa kitanzania ambao nao wana products nzuri tu, na start ups zao zinakick zaid kuliko hata hao ( Tembelea KINU na BUNI uone vijana hawa)

Najisikia vibaya napoona These big NGOs na other international firms vyeo vingi vya juu ,vinashikiliwa na watu kuitoka nje, same kwa big hotels na chochote kile chenye harufu ya ukimataifa basi sura ya Mbongo huwa ni ya kutafta sana, ukiipata inakuwa bado ina binywa, wakati tuna wasomi wetu wengi sana ambao wanauwezo mzuri sana.

Huku kujisikia vibaya hakuishii hapo tu, kunaenda kwenye michezo,Movie,had kwenye kuuza utalii wetu wa ndani. Na ndo hapo napopata conclusion kuwa pengine tatizo letu wabongo si ubora wa bidhaa, au ubora wa kazi, au Kujituma katika kutengenza kazi nzuri,au Elimu na Maarifa au uzuri wa vipaji, HAPANA, Hivyo vyote tunavyo vingi, na tumejaliwa sana . Tatizo Pengine ni kuwa WATANZANIA SIYO WAZURI SANA KATIKA KUUZA KAZI ZETU,KATIKA KUJIBRAND NA KATIKA KUTANGAZA UBORA WETU.

Ndo maana Marehem Kanumba, japo siyo kwamba alikuwa ni bora kuliko JB na Richie Richie ( According to my sister & My wife ) ambao ni wadau wakubwa wa Bongo Movie lakin aliweza kuanza kupenya na akafanikiwa kuiweka industry ya movie mahali fulani.

Swali ni kuwa is Diamond platnumz really that good??, Kwa sasa yeye ndo msanii bora Africa( MTV Emma),Akitoa wimbo hauwi tena topic ya kujadiliwa Jamii forums tu,tena kwa thread moja kama wasanii wengine, au XXL au FNL tu, inakuwa topic duniani huku mitandao top ya Naigeria,SA,na Kenya. (Watu wenye viburi barani Afrika) ikiongoza kumjadili, huku Vituo kama MTV base,Trace etc vikiback up huku Instagram na Youtube vikisimama kwa muda kidogo kwa views na comments.

Mfano:- ametoa wimbo tar 11 December kwa channel mbili tofaut you tube, moja ina view laki tano na kitu, na ningine yenye English subtitle ina viewers laki nne kasoro (had muda huu napoandika hii post) wakati huo huo Belle 9 alietoa wimbo wiki moja kabla yake, viewers hawajafika hata elf arobain, huku Jux alietoa siku moja kabla yake akiwa na viewers elfu therathin na kitu, Kaka angu Kala jeremiah pia nae kaachia kichupa chake bora kabisa tangu aanze mziki siku hyo hyo lakin viewrs bado hata elfu therathin ( Had muda huu napoandika hii post)

Swali je , kuna mbinu gani nyingine ambazo Diamond anatumia kutangaza mziki wake, ili na wasanii wengine waige? maana kazi zao ni nzuri tu, na wengi wanafanya vyema sana (Hongera kwa Navy Kenzo,Weusi na Vannesa,jIDE na The legend himself AY-Pioneer wa kupeleka mzik wa Tz Nje.

Sitaki kuamin kwamba ni msanii bora kuliko wote wali wahi tokea ndo maana amekuwa na record ambazo hazijawahi tokea, sitaki kuamin kwamba ni bahati, kwamba sijui ananyota kali kuliko wengine, sitaki kuamini , sitaki kuamini, Nachodhani ni mbinu fulani ya kibiashara ambayo wengine hawajaijua, au hawaujui, na hata wafanyabiashara na wafanyakazi wengi sisi tunaojaribu kupenya katika masoko ya kimataifa ni wakati sasa wa walau kujifunza vitu vichache vilivyowork kwa huyu jamaa na kuangalia namna ya kuviapply katika field zetu, iwe ni katika Employment,Business,Entertainment etc etc.

So Thread hii itumike kwa wadau mbalimbali kutoa mawazo yao, unadhani ni mbinu gani, au ni njia zipi zimemfanya Diamond kupenya katika international markets, ili Wasanii wengine na hata watu wa field nyingine waweze kucopy ili tuzid kupenya kimataifa zaid na zaid.

Wasanii wengi wanatoa video kali sasa hiv, na video nyingi zinapata access kwenye international media, lakin bado hawajapenya, so ina maana kuna kitu zaid ya kuwa na video kali, Collabo ??? wasanii wengi tu washafanya collabo za kimataifa lakin still hawakufika alipo fika Diamond, so Ni kitu gan kingine ambacho hatukijui?? Ni kama kwenye soko la ajira mtu akwambie uwe na PHd au Masters ya kitu fulani ndo upate kazi mahali fulani lakin still unakuta bado wabongo wenye hizo qualification wanapuliza, ina maana kuna code fulan bado hawajaibinya sawa sawa, so ni code gani hiyo???

Karibuni!!!

Mkuu uzi mzima sijaona neno ALI KIBA

inamaana KIBA hafanyi poa kabisa au vile uko mtaa wa pili?

kiukweli hizi mbio zishamshinda KIBA fans wanampa psychological suffering
 
Unaijua kwanza management ya ali kiba ?? Tuanze hapo

Hilo swali kila siku unauliza utafikiri kuna jipya wanalofanya.. Yupo chini ya Rockstar, na Keko anataka kuwapiga chini amelalamika wamemkwamisha mambo mengi, so hawezi kuendelea nao...!!
 
Namshauri kiba ajiunge kwa akina HARMONIZE BABY-AIYOLA atoka veery fastest.
 
Tatizo mashabiki wake mkuu hawatakubali hata kidogo, wanaichukulia poa WCB afu wanamuangalia kwa mbali harmonize yuleeeee anatoboa kimataifa
 
Hilo swali kila siku unauliza utafikiri kuna jipya wanalofanya.. Yupo chini ya Rockstar, na Keko anataka kuwapiga chini amelalamika wamemkwamisha mambo mengi, so hawezi kuendelea nao...!!
Kumbe unajua kila kitu sasa unauliza tena pigia mstari
 
Muuza sembe

ushabiki samtaimz unakufanya uwe kipofu.Kwahyo unataka kuniambia kuuza sembe ndo kumemfanya apate matuzo yote yale,na zile youtube views je,vipi lile nyomi la burundi na kongo miaka kadhaa iliyopita,kama ingekuwa ni sembe tu bas wauza unga wote bongo wangekuwa masupastaa maana wanapesa nyingi kuliko yeye.Mafanikio ya daimond ni kutokana na work ethic yake
 
Mimi navyofahamu watanzania ni wavivu na wanapenda kuridhika sana, mfano vijana wengi wanaohitimu vyuo Tanzania hua hawanaga mawazo ya kufanya kazi nje ya Tanzania wao wanachojua ni TRA,NSSF,BOT,CRDB etc....wakati kuna taasisi nyingi sana za kutest bahati yako...kwenye anga za kimataifa...hata mtu akiajiriwa hua hana mawazo mapya i.e kuanzisha kampuni inayotoa huduma nzuri juu ya kitu fulani unakuta mtu ana experience ya miaka 15 lakini bado muajiriwa tu watu hawana malengo na kutamani kuacha kitu kitakachofaidisha vizazi vyao vya mbeleni i.e. wanigeria wao mtu yupo radhi kuacha ajira na aanzishe biashara endelevu mfano kwenye sekta ya mafuta na gesi kampuni nyingi sana ni za wazawa

kwwnye swala la ubunifu wabongo wengi hawana ubunifu mfano huko kinu,binu, au tume ya sayansi ukienda mara nyingi vijana wengi wanachofanya ni kuchati facebook ubunifu kwa maana mtu hawezi waza kutoa kitu ambacho kitasaidia wengi au kitakacho kua kinatumika na wengi, au ambacho lazima mtu akitumie wakifanikiwa hapo aaah lazima wafike mbali mtu hawezi fikiria kunzisha kitu chenye malengo ya kua na coverage nchi nzima

kwenye mziki wasanii wengi wameendekeza starehe, mziki wa sasa hivi ni hela, hela kwenye video hela kwenye kujibrand pia, mfano chid benz alikua juu sana kama angewekeza kwenye kutengeneza nyimbo nzuri ambazo ziko stock zenye mashairi yenye kuweza kuwashika mashabiki yani mziki wa sasa hivi unahitaji angalau uwe na nyimbo 12 za kuachia kila baada ya miezi 3 au 4 kwa mwaka ili watu wasikusahau na ili uweze kufanya shooo...na pia diamond hua anafanya promo kwenye mambo yake skendo nini na nini zile zote hela zinatumika ndo mana jamaa anastay current mwisho wa siku pia inabidi uwe na management nzuri yenye kukupa support kwenye mziki....kuwekeza kwenye mziki kwa kua na studio, kufanya kazi vizuri bila kua na wasi wasi wa kutokua na nyimbo ya kutoa au kukosa hela za kufanyia video na kutoendekeza starehe...daaah nimetumia simu samahani kama haitakua inatokea vizur...

mkuu hapo kwenye vijana kujiongeza kwenye international jobs nimekuelewa sana na mi ni mmoja wa chasers wa hzo mavitu sema nna less acces na support,,vp naeza kukuchek ukaniongezea mwanga?
 
Mkuu nakubaliana nawe kwa baadhi ya point za msingi ulizozianisha hapa, na nyingine sikubalin aiseee,

Kuna watu wasanii wanajituma na wana kazi nzuri, kuna vijana hao hapo buni na kinu wana bidhaa nzur tu, na sio kwamba wana chat tu FB kama unavyosema but, hawatoki ktk mainstream kama wenzao wa Kenya na Rwanda
 
ushabiki samtaimz unakufanya uwe kipofu.Kwahyo unataka kuniambia kuuza sembe ndo kumemfanya apate matuzo yote yale,na zile youtube views je,vipi lile nyomi la burundi na kongo miaka kadhaa iliyopita,kama ingekuwa ni sembe tu bas wauza unga wote bongo wangekuwa masupastaa maana wanapesa nyingi kuliko yeye.Mafanikio ya daimond ni kutokana na work ethic yake
Unamjua dallas ??
 
mkuu hapo kwenye vijana kujiongeza kwenye international jobs nimekuelewa sana na mi ni mmoja wa chasers wa hzo mavitu sema nna less acces na support,,vp naeza kukuchek ukaniongezea mwanga?
Mimi ukinicheki nitakupa websites tu za kua unaangalia vitu vinavyohusiana na kozi ulizozisomea mkuu
 
Back
Top Bottom