Is Feisal Salum ''Feitoto'' overrated?

Is Feisal Salum ''Feitoto'' overrated?

Covid-19

Senior Member
Joined
Mar 2, 2020
Posts
162
Reaction score
364
Habari wanajukwaa?

Leo kwenye pita pita zangu mitandaoni nimekutana na hiyo mada instagram iliyoandikwa na mchambuzi wa michezo pale Azam tv anaitwa Alikamwe, ameandika mengi kuthibitisha statement yake kwamba Feitoto ni overated kwa mpira wetu hapa Tanzania.

Binafsi sikupendezwa na matumizi ya neno '' Overrated '' kwa nafasi yake kama mchambuzi kwani ni wazi anamkatisha tamaa kijana yule ambae kwa muono wangu kiwango chake kimekua kikipanda siku baada ya siku. Unawezaje kutumia takwimu za mechi moja kuthibitisha mchezaji ni overated? Hii si sawa kwa maendeleo ya vijana hawa.

Karibuni kwa michango yenu juu ya kauli hizi za wachambuzi wetu ambao mara kwa mara wamekua wakitumia akaunti zao vibaya kuandika mambo yasiyofaa kwenye mpira wetu.

Screenshot_20200910-002220_Instagram.jpeg
Screenshot_20200910-002139_Instagram.jpeg
Screenshot_20200910-002147_Instagram.jpeg
Screenshot_20200910-002155_Instagram.jpeg
Screenshot_20200910-002202_Instagram.jpeg
 

Attachments

  • Screenshot_20200909-232334_Instagram.jpeg
    Screenshot_20200909-232334_Instagram.jpeg
    64.4 KB · Views: 2
Ndio ubaya wa waswahili mnataka msifiwe tu! Mkiambiwa ukweli mnahusisha ukweli na roho mbaya

Binafsi nimejitahidi kuangalia kwa kila aina ya jicho lakini Feisal ameshindwa kunithibutishia ninachokiskia kuhusu yeye huku mtaani

Dogo ni overrated
 
Gift mauya ni bora kuliko huyo mpemba.Kuna yule mwingne anaitwa ndemla yuko pale mikiani,wanamsifia kwa kupga mashuti lakni yote yanaenda nje.
Kwani lazma ufanye comparison, itoshe tu kusema mpemba ni Overrated kwa leo

Ila siku nyingine tutadili na huyo anayepiga mashuti ya nje.... [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
. Leo tukae kwa Overrated kwanza
 
Kwani lazma ufanye comparison, itoshe tu kusema mpemba ni Overrated kwa leo

Ila siku nyingine tutadili na huyo anayepiga mashuti ya nje.... [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
. Leo tukae kwa Overrated kwanza
hahaahaa,utopolo na mikia huwa mnawakuza sana wachezaji wenu kupitiliza
 
Yaani mchezaji hujamuona hata mechi moja unasema Overrated!!

Kweny ile wiki yenu si ndo alipiga shuti mpira haujafika hata golini? .. mi sijawahi ona striker asiye na nguvu ya miguu kama huyo
 
All in all, Fei Toto ni fundi. Akiufanyia kazi huo ushauri, atafika mbali. Ni kweli kadogo bado kana umayai mayai! Kakiongeza stamina ya mwili wake, pumzi ya kutosha, akili ya kushambulia zaidi kuliko kutoa pasi za kusifiwa na mashabiki, akirudisha yale mashuti yake ya kushtukiza, hakika tutakafukuza ili kakajaribu bahati yake nje ya nchi.
 
Kwa kifup hana madhara....ila inatokana na position anayochezeshwa.
 
Back
Top Bottom