Is our president serious?

kiranga, i think that was a joke! Sidhani kama kikwete alimaanisha kuwa amempatia aisha zawadi ya tanzanite. If anything, alimaanisha kuwa isha should buy some before leaving the country. Ndivyo nilivyoelewa.

katika mkutano wowote lazima kuwe jokes kidogo to easy the tension
 
mkuu kiranga,


mi mwenyewe nilivosikia hilo la kunyosha mikono nikasema eh! Hivi haka 'katoto' kanaweza kuwaaambia watu wazima wanyoshe mikono ki hivi, hata kama ni kwenye mkutano?

alivyosema watu wanyooshe mikono ni kuchangamsha kikao wewe vipi,
hapo ni kazini hamna mambo ya haka katoto

content matters and not age
 
I guess even Bob Gendolf did not understand the question. She rephrased the question by asking what are you doing different to encourage investors. Did you hear Bob talking about commercial courts etc and how no one would bring their cash to invest in Tanzania if their assetts are not safeguarded. All these is having right policies. He even went emphasizing on Land property rights, ports and thats where he held kikwete on Task. If you live in Tanzania and you follow up on the investment procedures, you will understand my emphasis on adequate policies. One of the biggest complains by TIC is our investment policies. No investor with their right mind would want to invest in such level of inefficiency. Take a look at the Dar port utaona wht I suggest reforming our own policies and look at what is not working. Actually this is a time for Africa to sell itself to private sectors, thats why revisiting our policies is importantso I am sorry you do not seem to agree with what I am saying. I am done and there is no way I can convince you otherwise.

Sorry mimi nimechemsha, how about you giving us your take on the question?
 
Tazama ndugu Mkapa akiongea kwa ufanisi zaidi ya mh JK bila kigugumizi.
Tazama kuanzia 0:32:32

[ame=http://www.youtube.com/watch?v=R8CF4EoXjD0]YouTube - Davos Annual Meeting 2005 - Funding the War on Poverty[/ame]

Tazama pia kuanzia 0:52:00 uone jinsi Bi Sharon Stone alivyoanzisha harambee ya chap chap kwa ajili ya Neti za Mkapa. In 3 mins she raised 100,000 USD.
 
alivyosema watu wanyooshe mikono ni kuchangamsha kikao wewe vipi,
hapo ni kazini hamna mambo ya haka katoto

content matters and not age


Mkuu Semilog,,

content sawa, lakini na context je?

nadhani utakuwa umesoma michango ya wenzangu waliyotoa kuhusu umuhimu wa kuwa na one foreign policy na collective responsibility....kama hapo unaona mkullo kauchuna JK kanyoosha mkono...tayari ni embarrassment, mwandishi alitakiwa ajue kuwa swali hilo sio muafaka kwa hadhira ile!

kuna namna nyingi za kuchangamsha kikao sio lazima kunyosha mikono...hayo mambo ni ya kwenye semina zetu hizi (nasikia Pinda kazikataza)
 
The president looked more interested to the facilitator(the lady) yaani anaoffer Tanzanite stone sijui ya ujazo gani so cheaply!! other than any one else, ndo maana nasema hata CCM watusaidie kwa kumuheshimu Mwl.JKN wamwambie ukweli Rais Kikwete kwamba kipindi alichotumikia watanzania kinatosha!! upeo wake na tafsiri yake ya mambo ni mdogo ndo maana ukizungumzia Richomond au Dowans au mkutano kama huu haoni umuhimu wa kujua anasema nini, na wakati gani !!!!kama ktk huu mkutano hapa hata Mkapa angeshinda (pamoja ni mwizi kama kweli yanayosemwa maana wanamtandao waliwamwita Dr. Salimu mwarabu wa Oman!!) hivi unaulizwa wakati wa criss utafanyaje wewe unajeka.!!! na huyu ni baba wa nchi , Mungu ibariki Tanzania!! soma Biblia kuhusu Joseph alivyoitwa mtu wa maana wakati wa criss ya Misri ,Ukosefu wa chakula
 
alivyosema watu wanyooshe mikono ni kuchangamsha kikao wewe vipi,
hapo ni kazini hamna mambo ya haka katoto

content matters and not age

Huyo dada aliuliza lile swali kutokana na maelezo ambayo Jeffrey Sachs alikwishayatoa kwenye mkutano huo. Hivyo alikuwa anauliza kama wanakubaliana na mawazo ya Jeffrey Sachs. Na hapo utaona Kikwete anakubaliana na Mkullo hakubaliani (kwa kunyoosha mikono). Kwa hiyo halikuwa swali la policy formulation bali lilikuwa swali la kuweka uwanja tayari kwa ajili ya majadiliano na mazungumzo.
 
we didn't throughly grill our president during the campaign. we should have known how poor a communicator he is.

i know CCM hawapendi wazo la midahalo ya wagombea kiti cha rais [hata ndani ya chama chao pasipo kupambanisha wapinzani], sababu kubwa ya kuchukia huo utaratibu ni kutaka tuongozwe na dumb candidates kama huyu anayeishia kubabaisha mbele ya macho ya walimwengu.

nakubali kukosolewa, lakini kwa rais kama huyu tunadanganyana kudhani nchi inapiga hatua za kutosha kwenda mbele.shukran kwa aliyetuwekea link

naamini kuwa kujibu maswali peke yake siyo sifa za rais anayeongoza vizuri nchi yake, lakini huyu wetu bomu!!
 

Kine ulichosema ni kweli kabisa. Nakumbuka wakati wa kampeni ni gazeti la Annur peke yake ambalo lilitoa katuni ya JK akikimbia mdahalo na kipanya wa Annur akisema kaka unakimbia mdahalo kuongoza nchi siyo mchezo. Kwa hiyo mdahalo ni muhimu. Lakini suala la muhimu ni kuwa na demokrasia pana zaidi katika vyama. Hawa wagombea wa CCM na vyama vingine walichaguana kwenye mikutano yao mikuu na wala hawakupigiwa kura na wanachama wote. Ingekuwa vizuri wangepita kwenye matawi wakajieleza na wakapigiwa kura na kwenye mkutano mkuu inakuwa kumtangaza aliyeshinda na kisha kumkabidhi kwa Umma. Kitu cha pili ni kwamba waandishi wetu ni washabiki mno wa watu. Kama 2005 waandishi wangeacha ushabiki, basi tungempa wakati mwafaka rais kujiandaa kwa mambo makubwa zaidi. Rais Kikwete alishabikiwa mno na hivyo ni kama alidekezwa na media yetu. Matokeo yake anatuangusha kila anapohojiwa na vyombo vya nje
 

Mkodoleaji,

Hili ni swali la kumuuliza mtu mmoja mmoja, si swali la kuwauliza watu mkutano mzima wanyooshe mikono, halafu mtu kama Prof. Sachs anaweza kulijibu swali hili bila controversy kwa sababu yeye ni academic, kina Kikwete wao ni representative wa nchi kwa hiyo kama wanaulizwa swali hili basi iwe in a one on one session, sasa Tanzania tuna foreign policy moja tu, iweje Waziri wa Fedha na rais watofautiane? Ina maana kuna mmoja hapo hafuati foreign policy.Hili ni swali na kuuliza mtu mmoja mmoja likafuatiwa na maelezo, si swali la kuuliza ukumbi mzima na kuwafanya watu kama watoto wa darasa la kwanza. Ki itifaki huyu dada alichemka kuuliza swali sensitive la foreign policy, ambalo lilihitaji jibu refu sio tu la whether Washington still leads, but why and how the answer is what it is.
 

Kiranga mimi siyo mtaalam wa itifaki kwa hiyo siwezi kukupinga sana. Lakini kama mtaalam wa mijadala niliangalia kiupande wa mjadala zaidi siyo kiitifaki. Na ndiyo maana nasema yule dada alitupa lile swali kuchokoza ukumbi katika majadiliano. Sasa kama lile swali lilikuwa liendane na sera za nje hilo nadhani si sahihi. Kwa sababu Prof. Sachs alikuwa ametoa maada ambayo ilionyesha utawala wa Marekani umeishiwa nguvu ya kuongoza dunia. Sasa yule dada alikuwa anataka watu waongee kuanzia hapo na nadhani aliona hiyo ingesaidia kuchokonoa mawazo mbalimbali. Angeweza kuuliza swali lolote lile kwa mfano wangapi wanaamini kuwa Afrika ni Maskini?. Kuhusu itifaki sidhani pale ilikuwa itifaki ya kwamba wale ni wakubwa wasiulizwe maswali, mbona waliulizwa na wengine wakawasema wenzao.
 
Tatizo yule dada anauliza maswali kama Larry King, anautoa mpira huku anaupeleka huku, which is fine.Lakini kuna maswali mengine yanahitaji mtu ayajibu one on one na kuyatolea maelezo.

Sasa kama sisi tungekuwa na serious press basi hiki kikao kilikuwa na headlines kibao.

"Kikwete hafanyi chochote tofauti dhidi ya janga la uchumi"

"Mkullo na Kikwete watofautiana kuhusu Washington"

Not exactly the picture of governmental unity and collective responsibility.
 
Wakati sisi tunatolea mate "stimulus plan" kutoka nje, wengine wanasema "trade, not aid"

6. Africa, Business Destination - 10 Ideas Changing the World Right Now - TIME

 

Hapo tuko wote mkuu. Lakini media yetu si unaijua ya washabiki. Na usisahau ni media ambayo ilitumika kumpamba Kikwete kwa miaka 10 yote. Na nadhani akina Salva na Ulimwengu wanastahili kubeba lawama kubwa kwa nchi hii kupata kiongozi embarrasing kama JK. Maana ukipitia Rai za miaka ya nyuma, zilikuwa ziko makini kuichambua serikali lakini wakimfagilia Kikwete. Wengi hatukujua kumbe jamaa wako tayari mifukoni. Leo tumeona Salva akibebwa na mzee. Kwa hiyo hakuna mhariri au mmiliki (hata Mengi ambaye siku zote hujifanya anapamba na ufisadi huku akimsifia Kikwete aliyeingia ikulu kwa pesa za ufisadi) ambaye angetoa hivyo vichwa vya habari
 
Kilandu,
With due respect, I will rephraise the question... Mr. Kikwete, what is your Country doing differently in the wake of financial crisis!

Sasa mkuu hapa jibu lako liko nje kabisa ya swali na ndicho alichojaribu Kikwete kujibu kwa mapana zaidi lakini Bi. Aisha akamkata kauli..
Mkuu tunazungumzia Tanzania IMEFANYA NINI tofauti na policies zilizopo ili kukabiriana na hali mbaya ya Uchumi Duniani.. We have done nothing and to be truthfuly we can do nothing kwa sababu Tanzania na nchi zote maskini ni mabehewa yanayovutwa na kichwa -Nchi tajiri..
Sasa ukitazama Torisim, kupunguza taxes ni ujinga kabisa unless hufahamu nini kinachotokea - Dunia ipo in recession mkuu wangu, watu wanapoteza kazi, mahotel hata huiku nje yanapunguza wafanyakazi mengine yanafungwa...hakuna watalii kwa sababu ni wakati mgumu sana watu hawatumii fedha zao, na hasa wanaogopa matumizi yasiyokuwa ya lazima - Utalii ni mojawapo ya matumizi yasiyokuwa ya lazima!..

Hata hivyo binafsi nachofahamu mimi, Kikwete angeweza kabisa kutumia vita ya Ufisadi kuwa moja ya maangalizi ya hali hii mbaya ya kiuchumi kulingana na mazingira yetu..Lakini ukweli ni kwamba vita ya wahujumu Uchumi imeanza KABLA ya crisis hii na ukweli uatabakia kwamba hakuna kitu nchi maskini zinachoweza kufanya!..Pili hatuwezi kuingilia mashirika ya nje ktk utendaji kazi wake kwani mali hizo hazitengenezwi nchini, ajira yetu ni ktk services ya vitu kama simu, matangazo na kuuza bidhaa toka nje!..Tatu migodi yetu inamilikiwa na mashirika ya nje wenye mkataba hivyo ni wao wanao control kila kitu...Hivyo basi serikali yetu inategemea wageni na jibu litatokana na hali toka nje...Tanzania ni sokoni kwenye wanunuzi wanakokuja wageni kuuza au kuchuma mali..

Nitarudia kusema hivi.. Kikwete ALICHEMSHA na kujiuma uma kwa sababu hakuwa na jibu pia inajulikana muungwana ni domo zito, nimeona mahojiano yake mengi tu kuwa sii mzuri ktk kujieleza kama kina Mkapa...Na imemchukua hadi swali hilo liliporudiwa dakika ya 39 ndipo alipojieleza vizuri kuwa all we can do is to talk about it!..ndicho anachokifanya kila mwezi...to be aware of what is happening around us...
Kifupi ni kwamba sikuona hata mtu mmoja aliyejibu swali hilo zaidi ya kuongelea watakachoweza kufanya sio walichokifanya na kibaya zaidi ni kwamba hakuna nchi hata moja yenye mkakati mezani acha mbali wamefanya nini!..
 

Mkandara,

Sawa kabisa, na aliweza kusema hivyo baada ya kuwasikiliza wenzake waliomfuatia walivyojibu, especially yule waziri wa South Africa.
 

...na ndicho alichojaribu Kikwete kujibu kwa mapana zaidi lakini Bi. Aisha akamkata kauli..

Pamoja na mengi mengine yalosemwa na kina Kiranga, hilo na kumkata kata kauli Rais mwenyeji wa mkutano mimi sikulipenda hata kidogo.

Nimemuandikia barua dada Isha kupitia CNN Africa kumwambia hilo, pamoja na swala la kuchukua zaidi ya saa nzima ya Rais. Nimemweleza pia swala la kushindwa kufuata itifaki wakati anafunga mkutano.

Mwisho nimemkumbusha kwamba alitakiwa ajaribu kulinda heshima ya Rais aliyefanya hisani ya kukubali kuja kwenye majadiliano ya wazi na viongozi walio chini yake, mawaziri wastaafu, watu wa NGOs ambao hawaongelei serikali yeyote, wote wako pale wanaulizwa swali lile lile. Kusipokuwa na moderation makini ya maswali gani yanaulizwa matokeo yake ndio waziri na Rais wanatofautiana au waziri wa Africa Kusini anaejua kupinda pinda lugha anafanya Rais wa nchi aonekane hajiwezi.

Nilisahau tu kumwambia kuhusu kile kinguo alicho underdress pale mbele ya forum ya wakuu wa nchi na mawaziri. Sijui nimwandikie tena? Kama siku hizi hakuna kina Nyerere wa kukataa kupelekeshwa pelekeshwa na Wamagharibi basi wananchi tutasema, tumeshaamka. Yani binti alitudharau dharau tu pale!
 

Attachments



Kuhani
On right touch mkuu una nini na huyu mrembo aha ahha ahahha ha
 
[/I]

Kwi kwi kwi kwii kwii wenzio kile kivazi ndiyo kilifanya tuangalie ule mdahalo kwa muda wote (on right touch, no offense intended)
 
[/COLOR][/I]

Kwi kwi kwi kwii kwii wenzio kile kivazi ndiyo kilifanya tuangalie ule mdahalo kwa muda wote (on right touch, no offense intended)


sema pia kilichangia kwa namna moja kuhongwa mawe yetu ya thamani.....alitega watu pale!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…