P53,
hapana mkuu sikukuweka nafasi moja na JK hata kidogo isipokuwa nilidhani mwenzangu unalo jibu zuri kuliko la JK..
Mkuu, hata mimi nimejiuliza swali hilo baada tu ya kumsikiliza Kikwete..Sikuwa na jibu kwa sababu sijasikia wala sijaona kitu kikifanyika ambacho kinatuandaa sisi watanzania kupambana na hali mbaya ya uchumi duniani..
Na hasa ukisoma Thread ya:- Stimulus Package for Tanzania? A case against -Utaona kwamba ndio kwanza hapa JF tunalijadili na hatuna jibu kwani nchi yetu inahitaji stimulus kila siku ya maisha yake..Hatuna kitu kinachozalisha kiasi kwamba kikianguka tutaanguka kiuchumi kwani tayari tumekwisha anguka..
Utajibu nini mkuu ndio maana nikasema Kikwete amejiuma uma kwa sababu hafiria kitu gani kafanya.. hakuona ndani..Hakuna alichofanya zaidi ya U - Vasco Da Gama na kajibu hivyo..
Point being, we have done nothing ktk kujiandaa wala kufikiria kujiandaa, hivyo hakuna jibu hapo na hakuna mtu Tanzania nzima anayeweza kujibu swali ambalo hatuna mkakati wowote dhidi ya hali mbaya ya Kiuchumi duniani labda huyo msanii Mkapa..