Is our president serious?

Is our president serious?

Foreign affairs minister for 10yrs!! I rest my case.
 
afadhali umesema uwe corrected! nasema Kikwete ni mpiga ngoma za mdundiko , kwa taarifa yako, naweza nikakutajia ordinary people katika jamii yetu, ambao wangeweza kujibu swali vizuri, swali kujibu ni rahisi kama ni hicho kitu concern yako ya kila siku.

Kama umeendelea kuangalia mjadala huu, kuna Bob Geldof ( angalia dakika ya 15:48-16:00 Uone wanaume) anamponda Kikwete Live kuwa anaenda bandarini ANASEMA ANAJUA MAJINA YA WEZI HAWATAJI! HUKU WANAKULA FEDHA ZA UMMA! Kikwete ni 0 , zero I mean sifuri, au kwa msisitizo yai

Tena sifuri yenye masikio.

Lakini mwakani ni uchaguzi. Na tutamchagua huyu huyu kwa matumaini ya kuiboresha Tanzania, kiuchumi, kisiasa, kijamii na kadhalika.

Wabongo bwana! Hatuishiwi vituko.
 
Kichwa cha habari kingekuwa "mdahalo wamtoa nishai mkuu".
It's funny how a simple question can make dumb dumb, dumber.

Alibakia kujilamba, sasa huo mda wote anavyokwenda nje,anawaelezaga nini?

Anaendaga kuona majiji ya majuu, kujaribu kupata vidosho wa kizungu na kuomba misaada, sidhani kama huwa ana zaidi ya hilo
 
Tena sifuri yenye masikio.

Lakini mwakani ni uchaguzi. Na tutamchagua huyu huyu kwa matumaini ya kuiboresha Tanzania, kiuchumi, kisiasa, kijamii na kadhalika.

Wabongo bwana! Hatuishiwi vituko.

Yaaani, alishasema ya namna hiyo mengi tu
(1) Nawajua wanaouza madawa ya kulevya, saaana tuliishia kumpoteza mrembo wa bunge, Da Amina Chifupa
(2) Nawajua wanaohusika na rushwa bandarini, majina ninayo nitakuletea uwafukuze kazi
(3) Rweyemamu as a mouth piece, tunajua Balali alipo, tukimtaka tutamuita, aliishia kufa kifo chenye utata kuliko vyote siku za karibuni

Hivi mnajua GPA yake ya UDSM ya uchumi!!! na kwamba utashi wake kama human being ukiwekwa katika mizani ya 1 to 10 ata score ngapi?

Hatuna mtu pale jamani, basi tu kumbe nchi yaweza kujiendea bila kuwa na Rais..kwa Tanzania
 
Duuh wazee heshima kwenu.
Anyway Bob ameongea kitu ambacho Mr. Presidaaa alipaswa kukifanya wakati mwingine huwa nawaza hv tumelogwa sie!!!??. Presidaa na serikali inavyo elekea, hawana kabisaaa program yeyote maalum kwa ajili ya hii kraisis tunapelekwa tu.
Msenegali sijui kasemaje maana kifaransa mie madudu, bondeni at least kuna feeeling wanayo na wanajarib ku absorb lost jobs ktk ujenzi wa miundo mbinu.
Kazi ipo watz.
 
Wakuu,
Kikwete amechemsha kwa sababu hakuna alofanya wala hajui afanye nini na hii yoite inategemea na ELIMU tuliyopewa.. Kila kitu tunategemea mzungu aje kutufanyia na Kikwete amedhihirisha wazi kwamba Tanzania bado kabisa inaihitaji IMF kutupangia mikakati hata kama ni ya kutumaliza...
By the way, Kipapi kimesimama!..huyu Aisha mbongo au? haaa haa haa!

Mkandara acha kusingizia elimu tunayopata. Sisi kwa elimu hii hii tunayopata tumegundua jamaa kachemsha na wala siyo wazungu waliotuambia. Kwa nini Kikwete kachemsha ni kwamba hakai ofisini, hasomi na inawezekana hata mipango mikakati ya nchi haisomi. Siyo hilo tu, mwaka 2006 akihojiwa na waandishi wa habari wa bongo kuhusu NGOs kutumia vibaya fedha wanazopewa, unajua alijibuje? Alisema hilo ni tatizo na hiyo inatokana kuwa hakuna sheria ya kuzibana NGOs Tanzania. Na hiyo haikuwa sahihi kwa sababu sheria ya NGOs ilipitishwa 2001 na NGOs kibao zilipinga mpaka wengine wakatishwa kuandamana wakisema wanaingiliwa. Sasa angekuwa ni mtu anayesoma na kufuatilia mambo kwa umakini angeitaja hiyo sheria na pia angezungumzia wapi anaona pana mapungufu. Huna haja ya kumtetea sana. JK ni Rais, lakini tungependa afanye homework na hii ni pamoja na kupitia machapishi na kazi za watu walio chini yake.

Yule dada kamuuliza swali zuri ambalo pia lingekuwa ni opportunity ya kujimarket kama Tanzania. Hebu fikiria ile nafasi angepewa Kagame, Kibaki au Museveni ingekuwaje? Kweli kwenye miti mingi hakuna wajenzi
 
My Question is
If we are continuing to do the same, where are we going to endup. This is not acceptable I mean we must change. Don't we?
Does it mean we are going to do things the way we did before ie Richmon. IPTL Dowans, City water, etc.
NOOOOOOO WAY WE NEEED TO CHANGE.
 
Niandike lwa kiswahili kwani nimeshagundua wa-Tz Kiingereza tabu! Kwa sababu huyu JK alisema ana majina ya wauza unga na hakuwafanya kitu zaidi ya kutabasamu! Juzi akasema ana majina ya wala rushwa wa TRA akatabasamu na Bunge likasema watu aliowateua na kuchafua hali ya hewa Richmond wawajibishwe na sasa ni zaidi ya mwaka mmoja bado anatabasamu pia alijua na aliwapa kinga DAWANS ambao hata ofisi wala CEO hajulikani wakakopa pesa Stanbic na Barclays USD 75million kwa dhamana ya mitambo iliyopwekwa kwenye kiwanja walichopewa pale Ubungo na tanesco na Banks wakatoa mkopo huo akatabasamu, Dowans wakapewa amri aliyosaini yeye waondoke akatokea Idris akaenda mahakamani kuzuia wasiondoke akatabasamu; Ngeleja akakataa kununua mtambo baadae akakubali na rais akatabasamu;Idris akataka kununua mitambo mibovu huku akijua imewekwa poni akatabasamu; Sita na Mwakyembe wakakoroma akatabasamu;Idris akatishia kuleta giza ifikapo Agosti 2009 RAIS akaendelea kutabasamu na kila mwezi anachukua airtime ITV na TBC 1 Kutabasamu. Ameenda kwenye mkutano wa IMF kwenye TWIN 'towers' haramu bila kujiandaa akatabasamu na IDRIS/NGELEJA NA Baraza zima Richmond ,EPA wanamcheka. HUYU KWELI NI RAIS WA AJABU ni sawa na ile hadithi ya mfalme aliyekuwa na pembe
 
Niandike lwa kiswahili kwani nimeshagundua wa-Tz Kiingereza tabu! Kwa sababu huyu JK alisema ana majina ya wauza unga na hakuwafanya kitu zaidi ya kutabasamu! Juzi akasema ana majina ya wala rushwa wa TRA akatabasamu na Bunge likasema watu aliowateua na kuchafua hali ya hewa Richmond wawajibishwe na sasa ni zaidi ya mwaka mmoja bado anatabasamu pia alijua na aliwapa kinga DAWANS ambao hata ofisi wala CEO hajulikani wakakopa pesa Stanbic na Barclays USD 75million kwa dhamana ya mitambo iliyopwekwa kwenye kiwanja walichopewa pale Ubungo na tanesco na Banks wakatoa mkopo huo akatabasamu, Dowans wakapewa amri aliyosaini yeye waondoke akatokea Idris akaenda mahakamani kuzuia wasiondoke akatabasamu; Ngeleja akakataa kununua mtambo baadae akakubali na rais akatabasamu;Idris akataka kununua mitambo mibovu huku akijua imewekwa poni akatabasamu; Sita na Mwakyembe wakakoroma akatabasamu;Idris akatishia kuleta giza ifikapo Agosti 2009 RAIS akaendelea kutabasamu na kila mwezi anachukua airtime ITV na TBC 1 Kutabasamu. Ameenda kwenye mkutano wa IMF kwenye TWIN 'towers' haramu bila kujiandaa akatabasamu na IDRIS/NGELEJA NA Baraza zima Richmond ,EPA wanamcheka. HUYU KWELI NI RAIS WA AJABU ni sawa na ile hadithi ya mfalme aliyekuwa na pembe


Mkereme, I like the way you have presented this. Nimekupata, tupo pamoja!
 
Hivi Raisi wetu kikwete si amezungukwa na vijana waliosoma na wenye upeo mkubwa sana na nilisoma kwa michuzi kuwa some of them wanaandaliwa kuja kuwa our next president in the future? ambao ndiyo wanamsaidia kikwete kumpa ushauri right?!...so why hao watu wasomi wasimsaidie raisi wetu jamani eeh kumuweka jikoni wamuandae vizuri kabla hajatokea hapa...my question is wanacofanya sasa ni nini haswa hao washauri wa raisi kikwete (cijana na wasomi)

Kelly, Rais wetu anasemekana kuwa mbishi na asiependa kushauriwa wakati mwingi. Vijana wasomi wanaomzunguka hawana nafasi yoyote ya kumshauri kwa lolote. Wengi wao ni wapya katika nyanja za siasa na kwake hawaonekani kama watu wanaoweza kumshauri lolote. Yeye hujiona kuwa ndie mjuzi wa yote, na wao wanatakiwa kujifunza kutoka kwake. Hii ndio sababu kubwa ya mambo kwenda yanavyokwenda sasa. Hakuna team work katika uongozi na wala hakuna organized decision making.

Katika uongozi wa nchi kwa sasa, kila mtu anafanya madudu yake mwenyewe.
 
Wakuu,
jamani twende mbele huku tukitazama nyuma.. Kikwete amechemsha na amechemsha sio kwa sababu ya kujua jibu la kusema isipokuwa hakuona ndani kabisa.. Na wala msijaribu kumpa sifa Mkapa kuwa angeweza kusema vizuri...

Tatizo hapa ni kwamba unafanya nini ama una mkakati gani dhidi ya hali mbaya ya Kiuchumi duniani..Bongo hatufanyi kitu, hatufahamu nini kinachotokea na wala hatuoni ndani zaidi ya kusoma

Jibu la swali la bibie Aisha ni kwamba Tanzania hatufanyi kitu na wala hatuna mkakati wowote kujiandaa na hali hii...sasa huyo Mkapa angesema vizuri kitu gani hapa..Kama kuna mtu atanimbia ingekuwa Mkapa, angekwisha andaa mkakati huu au ule kupambana na hali mbaya ya uchumi ningemsikia na pengine jibu lingekuwa rahisi..
Ni Mkapa huyu huyu aliyewafuata IMF mara ya kwanza kwa sababu hakuona ndani kabisa... Na alipingana na wachumi wengi nchini ikiwa ni pamoja na kina Dr. Mwapachu..hivyo uwezo wa kujibu swali kama huna mbinu ni Ujinga mwingne..

Kikwete amechemsha kwa sababu hakuna alofanya wala hajui afanye nini na hii yoite inategemea na ELIMU tuliyopewa.. Kila kitu tunategemea mzungu aje kutufanyia na Kikwete amedhihirisha wazi kwamba Tanzania bado kabisa inaihitaji IMF kutupangia mikakati hata kama ni ya kutumaliza...
By the way, Kipapi kimesimama!..huyu Aisha mbongo au? haaa haa haa!

Mkapa anastahili sifa katika mazungumzo ya namna hii. Aliweza mara zote kutetea mipango na maamuzi ya serikali yake katika forum za namna hii kwa uwezo mkubwa. Mkapa hakuwa mtu wa mzaha kwenye kujibu maswali. Alikuwa akijiandaa kujibu, kuzungumza na hata kujitetea. Alikuwa si mvivu wa kusoma. Alijua mambo mengi yanayoendelea duniani na alikuwa tayari kusikiliza watu wenye utaalam kumshinda yeye. Kama angekuwa bado yuko madarakani wakati huu, naamini angekuwa ameshaanza taratibu za kitaalam za kutafuta njia ya kujiweka vyema katika hii financial/economic crisis.
 
jamani kama kuna mtu amepata hiyo karatasi anayo tumia Aisha kuwa uliza hao mapanelist hebu iwekeni hapa tuone nini hasa kilifikiwa ktk mkutano mzima.
 
There is an adage which says that 'A leader is the mirror image of the people he is leading' Coming to the topic ! The problem is tabia ya Watanzania kwenda kichwa kichwa bila kujiandaa His Exellence JK angewaachia wataalam simply angetoa key note opening remarks na sio kutoa mhadhara ukiwa na overconfidence watu wa media huwa wanakufix if they know your weakness. Ni aibu kwa taifa wala tusicheke tutafakari and mend the wounds period!

Rais asingeweza kumtuma mtu yeyote kuhudhuria kwa niaba yake na ndani ya nchi yake kwenye kikao kikubwa kama hicho. Kikao ambacho kina Rais wa IMF, Mkurugenzi Mkuu wa World Bank na dignitaries wengine wengi. Angefanya hivyo, angeonyesha kutojali mkutano huo, na kuupunguzia nguvu anayostahili.
 
NN & P53 ............SIyo kama wamjibie at least wangejaribu kumpika vizuri..si mnaona wenyewe anavyochemsha hapo ni kwamba hana clue kabisa na what is going on ndani ya nchi yake...angalia ameulizwa swali la finacial crisi...amejikanyaga kishenzi na anajibu kuwa he will continue to do the same what the hell....yaani badala ya kufikiria changes for the future...oh well!...i am just confused aisee baada ya kumsikiliza raisi wetu kwa kweli....
Dear Kell01 na wengine wote,

Tatizo hapa sio lugha jamaa (Kikwete ) (nashindwa hata kumuita Raisi) alielewa swali vizuri sana, ukweli ni kwamba hakuna plan yeoyte so far, haya matatizo ya uchumi wa dunia yana kitambo sasa na yamekuwa yakizungumziwa kwa muda sasa, lakini cha ajabu eti sasa hivi ( wiki chache zilizopita ) ndio imeundwa task force ikiongozwa na ben ndullu kuangalia jinsi gani inchi it minimize haya matatizo walikuwa wapi siku zote????? na hawa wabunge wetu wanakazi gani mbona hawaishikizi serikali kuhusu hili, au nao ni mbumbumbu kama huyu jamaa (Kikwete), Ahhh lakini tumeshazoa mtindi huu ni kama vile ishu ya umeme wa dharula miaka nenda rudi wakati mvua ikileta tatizo tu ndio huwa tuna fikiria vyanzo vingine vya umeme, Inatia hasira hata kuendelea ngoja niishia hapa ( alisema mzee kitine inchi inaendeshwa bila mipango sasa hivi means inaendeshwa kihuni, wakamjia juuu )
Regards
Kipa
 
Katika discussion hiyo, nimeshuhudia lack of responsibility, knowledge na commitment ya viongozi wetu katika mambo muhimu. Haiwezekani kiongozi wa nchi asiwe na mkakati wowote wa kuokoa Taifa lake kutokana na hii Global Financial Crisis. Haiwezekani Taifa lisiwe linajua chochote kuhusiana na tatizo hili kubwa, na haiwezekani kusiwe na majibu ya awali (hata madogo tu) kuhusiana na issue hii ya GFC.

Mkodoleaji ameshangazwa kama mimi na wengine humu kutokana na lost opportunity aliyokuwa nayo Rais katika ku-market Tanzania kama msemaji wa kwanza kwenye discussion. Mkodoleaji ameuliza kama ingekuwa Kagame, Kibaki au Museveni waliopata nafasi kama hiyo wangefanyaje? Mimi nasema wangemaliza muda wote wa kikao wakielezea mambo mbalimbali na ya maana wanayofanya kujiweka sawa, kukabiliana na kujiepusha na hii GFC. Najua wangesema sana.

Mimi napenda kujibu swali dogo la Mkandara kuhusiana na nini Mkapa au hata baadhi yetu tulitegemea Rais ajibu kwenye swali la "Tanzania inafanya nini tofauti kutokana na GFC?" lililoulizwa na Aisha Sesay wa CNN. Jibu langu ni kama ifuatavyo;

1. Rais angeweza kuelezea mshituko ambao Tanzania umepata kutokana na GFC
2. Rais angeweza kuelezea serikali yake inachofanya au inachotarajia kufanya kuhusiana na issue hii. Kwa mfano, angeweza kuahidi kuwa ataunda task force ya Wataalam wa uchumi, fedha n.k wenye uwezo wa kuishauri serikali njia ya kupambana na tatizo la GFC, kwa kuainisha njia mbadala za mapato, mbinu za kubana matumizi, kuweka priorities za mambo mbalimbali, na kuanisha aina ya uchumi unaowezekana katika kipindi hiki pamoja na mambo mengine
3. Rais angeweza kuahidi/kuelezea serikali yake itakavyo badilika (mabadiliko katika hili ni lazima) ili kupunguza mtikisiko wa kiuchumi nchini
4. Rais angeweza kuomba wahisani (kama ilivyo kawaida ya TZ - Ndivyo tulivyo) waendelee kuipa support nchi kwa kusaidia kukuza uwekezaji, kuendelea kusaidia kiuchumi n.k.
5. Rais angeweza kuweka bayana sababu za nchi wahisani, wawekezaji wa nje na wengine wote wanavyoweza kufaidika na uwekezaji nchini

Ni mambo mengi Rais alitakiwa ayaseme katika nafasi hii adimu.
 
nahisi rais akujiandaa kujibu swali lolote sababu walishaongea naye huyo dada asimuulize mr.pres. chochote, sasa hule mshtuka wa kuulizwa cha kujibu kukawa hakuna, mbona hata mimi ningeweza si angemwambie tanzania tujiandae kivipi na sisi tunategemea misaada.tunamwachia mungu tu,dada angeelewa.
 
JK hakujiandaa tu vema kwa ajili ya hii mada!

Sijui kama ana nafasi kusoma majarida ya kinachotokea duniani ili kumpa facts na wider knowledge base ya kuwa Panelist mzuri!

Maandalizi tu hakufanya vizuri!

Na pia hana washauri wazuri wataalamu wa kumshauri how and what to prioritise in public sessions kama hizi za IMF!

Ila huyu mama wa Kinegeria Aisee.. kiboko! Wau!!! I really admire her!
 
Jamani Rais ana mambo mengi sana kichwani - ya kwake, ya familia, ya nchi yake etc. sasa Q&A kwa yoyote unaweza kuwa overtaken - lets understand that our President is a human being - hakuna mwanadamu asiye na kasoro - AJITOKEZE kama yupo -
 
Back
Top Bottom