Is our president serious?

Mimi nashangaa kwa nini tunamtetea JK. Rais wetu tunamjua alivyo mchovu kwenye huu upande. Kama amekuwa forign minister kwa miiak 10 na haku-improve hivi mnategemea mabadiliko sasa. Akina Mkandara wanateea udini tu hakuna kitu kingine.

Anyway, nafikiri kwa sasa tungekuwa tunajiuliza kwa vipi mpaka sasa TZ haina mkakati wowote huku wakijuwa hali halisi ya GFC ya dunia. Mimi nasema hivi kwa kuwa nchi yetu inategemea 45+ % ya bajeti yake kutoka kwa wafadhili. Kwa hali inavyokwenda kuna uwezakano mkubwa hiyo misaada tusiipate kama tulivyoahidiwa. Sasa kama mpaka sasa hatuna mkakati wowote, je planing itaanza lini????
 
Jamani Rais ana mambo mengi sana kichwani - ya kwake, ya familia, ya nchi yake etc. sasa Q&A kwa yoyote unaweza kuwa overtaken - lets understand that our President is a human being - hakuna mwanadamu asiye na kasoro - AJITOKEZE kama yupo -

Mkuu Preacher, nakubaliana na wewe kabisa kuwa Rais wetu ni binadamu kama sisi wote na ana mapungufu yake kama sisi wote tulivyo na yetu. Yeye ni kiongozi wetu (kwa kutuomba tumchague).

Tunachozungumzia hapa ni inakuwaje kiongozi wa nchi changa/masikini ya awamu ya Tatu kama yetu, yenye uongozi unaojivunia, yenye watu zaidi ya mil 35 inashindwa kujisemea katika mambo kama haya. Haya yanafanyikia nyumbani (labda ndio maana tunayaona kwa macho yetu). Je yanapofanyikia huko nje, nini hasa taswira ambayo wenyeji wetu na mataifa mengine huipata kuhusu Tanzania? Je, inajenga au inabomoa?

Mkuu, Rais wetu aliomba tumchague, akazunguka nchi nzima akitoa ahadi kemkem, akachaguliwa kwa kura nyingi na wengi wetu (80%), Akashinda na akawa Rais wa nne (4) wa Jamhuri ya Muungano. Akatushukuru na akasisitiza tena ahadi zake kwetu. Hivyo ni mategemeo yetu kuwa, licha ya kutekeleza ahadi hizo kwa vitendo, ataweza kuzitetea na kuzizungumzia kwa mapana na haiba kubwa (kwakuwa ndio kazi aliyotuomba tumwamini nayo Mkuu). Ni mategemeo yetu kuwa anajua zaidi ya wengi wetu matatizo na usuluhisho wa matatizo yetu mengi na ana nguvu za kuyafanyia kazi. Tunategemea awe muoga kuliko alivyoonyesha kwenye kikao hicho kuhusu mustakbali wa Taifa lake hasa kipindi hiki kigumu.

Mkuu, anaposhindwa hata kuongea, inatupa wasiwasi kuhusu kutenda. Ni hayo tu.
 
Jamani Rais ana mambo mengi sana kichwani - ya kwake, ya familia, ya nchi yake etc. sasa Q&A kwa yoyote unaweza kuwa overtaken - lets understand that our President is a human being - hakuna mwanadamu asiye na kasoro - AJITOKEZE kama yupo -

Kuna tofauti baina ya kuwa na mambo mengi na kuwa vegetable, Kikwete ni vegetable tu.

Si kwamba alistukizwa barabarani akaulizwa haya maswali (kama anavyopenda yeye kuwastukiza watu, remember alivyo m harass Mgawe yule Director General wa Bandari kuhusu kuna magari ambulance ngapi na ziko wapi? bila advance notice?). Kikwete alijua kabisa kuna hii forum, hakufanya homework yake tu.

Kikwete ana matatizo mawili, hawezi ku "think on his feet" na kutoa jibu zuri haraka, anaanza kwa kuboronga na kama akitoa jibu la kueleweka basi litakuja katika raundi ya tatu ya swali hilo hilo.Sioni swala la mambo mengi, kama una mambo mengi unatakiwa kuwa na mengi ya kusema pia, Kikwete ni slopoke tu.Zaidi ya hapo Kikwete anafikiri kwamba yeye ndiye anaye set agenda, fine, anashindwa hata ku spin na kusema "the question is...." kama wanavyofanya wanasiasa wenzake siku zote (ushaona mwanasiasa kaulizwa swali ambalo hawezi kulijibu, anajishaua, halafu kuua soo anasema "look, the question is..." anajiuliza swali tofauti lenye kubeba vi talking points vtyake na kulijibu) Kikwete alishindwa hata kufanya hivi.

Na huyu dada naye alienda overboard kwa kuwapeleka watu mpwita mpwita bila itifaki wala kuwa sensitive kwa masuala mengine ambayo yanagusia Foreign policy.Huwezi kuwauliza wakuu wa nchi kuhusu swala ambalo linagusia foreign policy kama vile msimamo wao kuhusu uongozi wa Wshington kwa kuwalazimisha wanyooshe mikono on a simple Yes or No question that has a gazillion potential to be misinterpreted and even ending up being explosive.

No wonder amepata impression kwamba watu wengi hawakubaliani na Jeffrey Sachs wakati in actual fact watu wengi wanakubaliana na Jeffrey Sachs (all one needs to do is African countries foreign policies and opposition to washington) but people are not ready to simplify that in a simplistic manner like she wanted to bully them into.Some of these things have not been decided on in proper cabinet meetings, na hawa wazee wameenda pale kama wawakilishi wa nchi, sasa huyu dada alitaka kuwauliza maswali personal, hapa kuna explosive situation, vipi kama waziri haafikiani na rais kuhusu hili, je anyooshe mkono against rais in public view? na ku risk a show of lack of unison and collective responsibility? Ndiyo maana washua kibao wakaona isiwe tabu, ngoja tuuchune tu.
 
kati ya vitu ambavyo watz tulichemsha ni kumchagua kikwete. hayuko serious. he's very dangerous kwanza.ni mdini sana. ameingia hapo ili kuwapendelea waislam tu kwenye vyeo, na atahakikisha muda atakaomaliza amewapendelea vya kutosha.
Nadhani ubadilishe jina na kujiita utumbo utumbo kutokana baadhi ya pumba unazoandika hapa, what a waste.
 
Nimegundua pia section waliyochukua media kama quote yake ya maana ni pale alipokuwa anaongelea demand, marobota ya pamba hayauzwi nk...lakini kusema kweli sehemu nyingi ameonyesha 'udhaif' hata kama yeye sio technical person, lakini si ana shahada ya uchumi?

I can imagine waandishi wana kazi kubwa ya kuedit....otherwise this is total embarrassment

Kisha he goes all the way kumwahidi Aisha tanzanite! how does this fit in kama sio utamaduni wetu ulee wa takrima?
 
Last edited:

Kiranga umegundua? You know what I'm saying? Yani yule binti kawaburuza buruza tu kama watoto wa shule pale.

Kwanza binti kashindwa ku moderate mkutano kapitiliza muda kwa zaidi ya saa nzima, kachukua muda wa Rais saa nzima over! Mkwara mwingi mwanzoni kadai wenye maswali marefu atawakatisha, wapi!

Halafu Waziri anaeongea Kifaransa (sijui Ki-Senegal) huyu moderator alikuwa na translation headset masikioni alitakiwa atuambie Msenegali anasema nini kifupi.

Halafu binti hajui protocol, ilibidi Rais na yule director wa IMF ndio wawe wa mwisho kufunga mkutano. Yeye kamchomeka Kikwete katikati katikati kwenye closing remarks.

Halafu kamkatisha katisha Kikwete wakati anajibu, japo Kikwete kweli alikuwa mzito. Ameshindwa kuelewa kwamba yule Rais amefanya favor kuja kwenye joint forum na watu wa chini yake, mawaziri. Sio kitu advisable kwa sababu unaweza kuwa upstaged na waziri, ni risk, ambayo kweli ime backfire kwa Kikwete, ilibidi yule binti atambue toka mwanzo na awe careful and graceful.

Halafu kuna sehemu Isha aka make a big fuss about the fact kwamba kuna mjuba mmoja alisema mkutano wa viongozi wa Africa ulikuwa "shambolic." She made a big stink about it, wakati yale ni mawazo ya mtu mmoja tu! Na kuna waziri mmoja pale (sijui wa wapi yule) akakataa hiyo hadithi kwamba mkutano ulikuwa shambolic. Binti akatokea kaishiwa!

Na lingine ni hilo la kuwaambia wanyoshe vidole kama wanakubali kwamba Washington doesn't govern anymore. Hilo ni swali unauliza mtu kwenye one on one interview, sio pale ambapo Kikwete kanyosha kidole halafu Mkullo hakunyosha. Hilo swala linahusiana na foreign policy ya nchi ambayo inabidi wawe na sauti moja. Nishai.

Hivi Kiranga unajua ni kwa nini yule binti aliweza kuwatisha tisha ovyo watu pale?
 

Kaizer,

Halafu na Aisha mwenyewe hakuonyesha professionalism.Kwa kukubali zawadi hii anajiingiza katika vishawishi vya kuwa "chummy" na viongozi.Kama muandishi anatakiwa ku maintain umbali wake ili aweze kuwabana vizuri, sasa kama akikubali Tanzanite kesho keshokutwa akiwa katika position ya kumbana Kikwete ataweza kumbana kweli?

Najua Kikwete anaweza kujitetea kwamba anatumia nafasi hii kuitangaza Tanzanite na anakuwa anamfanya huyu binti awe kama billboard, kwamba watu wakimuona amevaa Tanzanite anaweza kuulizwa hii nini, umepata wapi etc, na hivyo kuongeza mauzo ya Tanzaniate, especially because she is highly visible as a CNN journalist, kwa hiyo kwa upande mmoja Kikwete anafanya kazi yake.Any concerns about propriety should rest because he did this publicly (kwa hiyo hakuna kificho)

Kwa hili mimi naona huyu dada kwa kukubali offer ndiye aliyechemka, after all zawadi itakwenda CNN au kwake? Protocol ya ku reciprocate itakuwaje, atatoa yeye mwenyewe zawadi kwa Kikwete au atatoa wapi?

Kwanza CNN ina policy against journalists wake kupokea gifts

CNN, Fox Crack Down on Junketeers - Media Blog - Jeff Bercovici - Mixed Media - Portfolio.com

 
...kwahiyo sasa mmegundua umuhimu wa kuwepo midahalo kwenye kinyang'anyiro cha kugombea uraisi, ubunge na uwakilishi?

mmeamini midahalo ni kipimo kimojawapo kugundua IQ ya mgombea, haswa yale maswali ya nyongeza?

mkitaka kujua wanaochapia, endeleeni kusikiliza vipindi vya maswali na majibu Bungeni toka kwa wabunge kwenda kwa waheshimiwa mawaziri... maswali mengine, kama yalivyo majibu mengine ni aibu tupu!

...haki yetu kuwasaili wagombea.
 
Kiranga, I think that was a joke! Sidhani kama Kikwete alimaanisha kuwa amempatia Aisha zawadi ya Tanzanite. If anything, alimaanisha kuwa Isha should buy some before leaving the country. Ndivyo nilivyoelewa.
 

... If anything, alimaanisha kuwa Isha should buy some before leaving the country. Ndivyo nilivyoelewa.

Zungu Pale,

Angekuwa amemaanisha kwamba Isha akanunue mwenyewe hivyo vito vya thamani basi Isha asingesema "mmemsikia"? Akiamaanisha kwamba Kikwete kaahidi zawadi!

Labda useme ni utani, lakini usibadilishe ukweli kwamba Kikwete ali offer zawadi na mwandishi akakubali!

Yule dada kuna mambo mengi ameharibu pale ambayo asingeweza kufanya akiwa kwao Magharibi, kuchukua zaidi ya nzima ya muda wa Rais!
 
Hivi Kiranga unajua ni kwa nini yule bingi aliweza kuwatisha tisha ovyo watu pale?

Ushawahi kuona traffic police kakamata mtu ambaye hajui Kiswahili halafu akaamua kumuachia bila kumfanya lolote?

Yai mwanangu yai, yai na ile confidence inavyo ooze pale, na sisi culture yetu iko passive (Kikwete anasema ataenda kuwa humble kwa Gordon Brown!) Mpaka Bob Geldof kampaka kwamba rais anaenda bandarini nansema anawajua wezi na wazembe lakini hataki kuwa fire (jamaa kamsema live pale pale) tuko passive pasive, kuanzia mikataba ya Mzovero na Carl peters mpaka ya EPA.

Demu kasoma na kukaa West kaja na mi aggressive approach ya west (plus) lakini kakosa tact, na grace (negative) na nafikiri hata experience bado.

Ana potential ya kuwa mwanahabari mzuri sana kama akiichannel hiyo confidence vizuri, lakini otherwise anaweza kukutana na kina Mugabe type huko, ma egomaniac prima donna Museveni types wanafunga forum pale pale, kisa moderator hana adabu anawapeleka peleka wazee wananyoosha vidole kama watoto wa darasa la kwanza.
 

Exactly, binti kawaona watu wenyewe wachovu akaleta jeuri.

Kama unavyosema, a Ghaddafi or an Omar Bongo Ondimba anafunga kikao pale pale!

Binti anacheza yule. Kawatisha na Kiingereza. Kwanza pale mtu kama mimi najua masuala hayapandi ningeleta jeuri, ningeomba headset ya Kiswahili! Putin style! Wangekoma na mimi.

Kikwete anasema ataenda kwenye G20 kuwa "humble"!

Yule panelist Mwanamama, ex-finance minister wa Nigeria na foreign minister wa South Africa wakakataa! Wakasema Noooo! No no no! Hatuendi kuwa humble kwa Gordon Brown! Screw that! Wakakataa!
 
Suala lililonipa taabu mimi ni pale ambapo viongozi wa Africa wana"demand" kusikilizwa na kuwa na ushawishi zaidi kwenye hizi "Bretton Wood Institutions". Kila aliyeongea alionesha kuwa bila misaada hakuna kinachoendelea Africa. This was wrong and a brave mistake. Dr. Ngozi tried to tell our leaders that the World needs Africa. We have the resources they need. So, all is needed is to forge a business partnership, period. Una bidhaa inayohitajika (high demand), then bado unanyenyekea bila utaratibu maalum. Hii masuala ya ku-negotiate kwa uoga as if we have nothing to offer yataendelea kuwafanya wazungu wazidi kutudharau. Na wazidi kufaidi raslimali zetu na kutuacha tukipiga miayo.

Kikwete na wenzake wameonesha kutofahamu World Bank na IMF ni kitu gani. Na Dr. Ngozi alishindwa kuwafahamisha washiriki World Bank ni nini? If I have to paraphrase a statement by J. Wambia, a former World Bank employee who said " World Bank is a bank like any other bank. Those who put in their money, decide how their money should be used. At the World Bank, you vote with your wallet and not with your mouth." The same applies for IMF. Sasa, viongozi wetu wanazungumza kana kwamba, the two are charity organizations and they have big stake in the two institutions. And one stands to benefit more if he/she thinks of World Bank as a source of knowledge more than funding.

Africa, what is our problem? Tunasubiri kuambiwa nini cha kufanya na Bob Geldof - a mere rockstar!
 


Mkuu Kiranga,

Huyu Aisha naye si 'mwenzetu' tu kasoro chombo anachoripotia? LOL

Nakubaliana na hilo la kutokuwa professional kaa alivotaka tuamini, 90 minutes ikawa lisaa limoja zaidi, hivi kwa nini JK asingewalk out kama alikuwa pale in courtesy?

Mi mwenyewe nilivosikia hilo la kunyosha mikono nikasema eh! hivi haka 'katoto' kanaweza kuwaaambia watu wazima wanyoshe mikono ki hivi, hata kama ni kwenye mkutano?
 
Jamani sidhani kama hizo petty issues kama za kufuata protocal au kutumia muda mrefu kwenye maswali au hata professionalism ya huyo Journalist vina umuhimu hapa. Hebu tuache mchezo ya kutafuta vijisababu vya justify ugoigoi hapa. Kitu kikubwa hapa ni uzembe wa Rais wetu Kikwete, kushindwa kujibu swali ambalo alitakiwa awe na jibu au hata na idea ya kitu cha kujibu.

Pia sidhani kwamba lile swali lilikosewa kuulizwa eti sijui viongozi warudi wakaongee na baraza la mawaziri ili ijulikane Foreign Policy ya Tanzania, hakuna kitu kama hicho, unapozungumzia sera za kiuchumi na wewe ni kiongozi wa nchi lazima uwe na plans na hata contingency plans ambazo zinaweza kuiinua nchi kutoka katika janga hilo. Hii crisis haijatokea leo ambapo Rais anakuwa hana jibu hata moja.

Kikwete umechemsha big time.
 
Oh please! Aysha is not to blame for the Tanzanite related exchange of words, she asked not!the president offered, must've been intimidated by her beauty and brains in one package of course... Mnaosema kakosa adabu mna double standards coz she's female angekuwa male mnesema jamaa anaguts! Mr president alichemsha, Aysha is not to blame, she was just doing her job....well.
 

Geeque,

Ni muhimu tuweze ku cultivate a fair and equanimity minded, mulifaceted way of looking at things, to have a multi-track sober mind if you will.

Hili si swala la either or, all or nothing, Kikwete or Aisha. Ukiangalia mchango wangu hapo juu nimemsema sana Kikwete kuhusu udhaifu wake, nikamtetea pia ilipobidi, ana huyu dada pia nimempa kudos zake, lakini sehemu alipochemsha nimemsema tena.

Kwa hiyo wote wana strength zao (Kikwete ameweza ku maintain composure yake gracefully hata baada ya kuendeshwa kama a lesser man na huyu dada, a plus) Huyu dada hakuacha viongozi wamu intimidate (a plus) na pia wote wana weaknesses zao (Kikwete hakujiandaa, hakuweza kujibu maswali barabara mpaka raundi ya tatu) a negative (Aisha hakuweza kuwa graceful, hakuonyesha tact na experience, amepitisha muda, hakufuata protocol kuanzia jinsi ya kufunga mkutano mpaka maswali mengine aliyouliza hayakuwa appropriate kama tulivyoongea hapo juu)

Kwa hiyo ili kuangalia issues in their true lights inabidi tuondoe huu mtizamo wa upande mmoja tu, inabidi tuangalie pande zote, na tuseme wazi kuwa Kikwete ingawa alikuwa slow na alikuwa anaboronga, lakini pia alikatishwa etc na huyu dada ingawa alikuwa na confidence na aliuliza maswali bila uoga, aliwaburuza watu, hakufuata protocol na hakuwa professional, yote yanaonekana katika viyo video wala hamna ubishi.

Kuhusu swali la Foreign policy lile lilikuwa inappropriate, unaweza kumuuliza mtu mmoja katika interview lakini huwezi kuwauliza mawaziri kibao na rais wao, kwa sababu hilo ni swali la cabinet level decison na serikali inafanya kazi kwa collective responsibility.Plae watu wamekuja kama wawakilishi wa serikali, hawajaja kama Mkullo na Kikwete, sasa ukiuliza swali ambalo Waziri wa fedha na rais wanaonekana kutofautiana in animpromptu "nyoosheni vidole question" una undermine collective responsibility na foreign policy ya a sovereign country, hili swali liko katika "gotcha politics" na kama kwenye mahakama swali kama hili unapewa " Objection your honor".Ni mwandishi asiyekuwa na experience tu anayeweza kuuliza swali kama lile kwa jinsi ile.
"

Hatuko hapa kumpamba au kum bash mtu, ni facts tu.
 
Last edited:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…