Wakuu,
jamani twende mbele huku tukitazama nyuma.. Kikwete amechemsha na amechemsha sio kwa sababu ya kujua jibu la kusema isipokuwa hakuona ndani kabisa.. Na wala msijaribu kumpa sifa Mkapa kuwa angeweza kusema vizuri...
Tatizo hapa ni kwamba unafanya nini ama una mkakati gani dhidi ya hali mbaya ya Kiuchumi duniani..Bongo hatufanyi kitu, hatufahamu nini kinachotokea na wala hatuoni ndani zaidi ya kusoma vitabuni..
Jibu la swali la bibie Aisha ni kwamba Tanzania hatufanyi kitu na walka hatuna mkakati wowote kujianda na hali hiyo...Sasa kama kuna mtu ataniembia Mkapa angekwisha andaa kitu hiki kupambana na hali mbaya ya uchumi ningemsikia na pengine jibu lingekuwa rahisi..Ni Mkapa huyu huyu aliyewafuata IMF mara ya kwanza kwa sababu hakuona ndani kabisa... Na alipingana na wachumi wengi nchini ikiwa ni pamoja na kina Dr. Mwapachu..hivyo uwezo wa kujibu swali kama huna mbinu ni Ujinga mwingne..
Kikwete amechemsha kwa sababu hakuna alofanya wala hajui afanye nini na hii yoite inategemea na ELIMU tuliyopewa.. Kila kitu tunategemea mzungu aje kutufanyia na Kikwete amedhihirisha wazi kwamba Tanzania bado kabisa inaihitaji IMF kutupangia mikakati hata kama ni ya kutumaliza...
By the way, Kipapi kimesimama!..huyu Aisha mbongo au? haaa haa haa!