Grevic Jos
Member
- Aug 29, 2013
- 57
- 2
Mdau hapa naona haiko sawa.
Watu tunahistoria ya kusomeshwa na wazazi wetu kupitia SACCOS kwa mikopo na marejesho ya fedha kidogo kidogo za mama zetu wakaanga vitumbua.
Tumesoma shule za private kwa kuwa ni serikali hii haikutaka kutupangia shule zake kwa kuwa ufaulu wetu ulikuwa ni wa kiwango cha chini.
Hali imeendelea hivyo hadi katika ngazi za diploma, na hii yote ni katika kutafuta sifa linganishi za kutuwezesha kufika huko kwenye vyuo vikuu, na Mungu amesaidia hili.
Sasa serikali ikifikiria sisi kupitia njia mbadala kuwa tuna uwezo inakosea kwani nayo pia ni sababu ya sisi kusomeshwa shule na vyuo hivyo, na si kwamba wazazi wana pesa la hasha; wamekopa sana ktk SACCOS hizi hadi wamepoteza sifa za kukopesheka tena kwa kuwa madeni walionayo ni makubwa mno.
Kwa wale waliopewa wakadisco, bado pia wana haki ya kupata tena siku wakimaliza masomo wakafaulu basi watarejesha madeni.
Ni ukiritimba wa serikari na watu wachache iliowakabidhi hatamu za kuvisimamia vyombo hivi vya fedha.
DUUH!NI KWELI NDUGU,lakini wafanyacho wao ni kufuata miongozo waliyopewa kuhusu ugawaji wa mikopo.TATIZO LINAKUJA KUWA NI ZILE KANUNI zinazowaongoza Hazitambui "some"cases kama hizo ulizoandika!
Ila dah,POLENI SANA,
dont lose hope my bro&sisters!