Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kufuatia kifo cha kusikitisha cha Juma Said Mfaume, mkazi wa Mbagala Mlandizi, familia yake/mke anaweza kufungua kesi ya fidia dhidi ya wafanyakazi wa Kampuni ya OYA Microcredit. Juma, ambaye alikuwa mume wa Khadija, alifariki baada ya kupigwa na watu wanaodaiwa kuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo katika tukio lililotokea alfajiri ya Jumanne, tarehe 8 Oktoba 2024.
Inadaiwa kuwa wafanyakazi hao walifika nyumbani kwa Juma kudai marejesho ya mkopo wa Tsh 60,000 ambao Khadija, mke wa marehemu, alishindwa kulipa kikamilifu. Wakati wa mabishano kuhusu deni hilo, wafanyakazi hao walitaka kuingia nyumbani ili kuchukua mali kama fidia, jambo ambalo Juma alikataa. Hali hii ilisababisha ugomvi ambapo mmoja wa wafanyakazi hao alimpiga Juma kwa kigongo shingoni, na Juma kuanguka. Baada ya kuanguka, walimpeleka hospitali, ambapo alifariki.
Soma: Mke wa Juma aliyepigwa na Wafanyakazi wa 'OYA' aeleza alivyokopa
Mjane Khadija anayo haki ya kufungua kesi ya madai dhidi ya wafanyakazi hao wa OYA akidai fidia kwa madhara atakayopata kutokana na kifo cha mumewe huku kesi ya jinai dhidi yao ikibakia palepale. Aidha, kwa kuwa mjane huyo amedai kwamba mmewe hakuwa mdhamini katika deni hilo, haikuwa sahihi kwa wafanyakazi wale kumdai mume ukizingatia hakuwa sehemu ya mkataba wa kukopeshana fedha.
Endapo mjane huyo aliweka dhamana mali zozote za ndoa, sheria inaelekeza kuwe na hati inayoonyesha mke na mume kuridhia mali hizo kushikiliwa kama dhamana. Iwapo hatua hiyo haikufatwa wafanyakazi hao bado hawakuwa na mamlaka ya kutaka kutaifisha mali hizo kwa ulazima.
Pia, Soma:
+ Pwani: Wafanyakazi wa kampuni ya mikopo ya OYA, mbaroni kwa tuhuma za mauaji
+ Mfahamu Juma Jangalu anayedaiwa kuuawa na wafanyakazi wa OYA
+ Kampuni ya OYA 'yawakaanga' Wafanyakazi wake waliosababisha kifo cha mtu walipoenda kudai marejesho