Ishara hizi zinaweza kukusaidia ktk maamuzi

Ishara hizi zinaweza kukusaidia ktk maamuzi

yaani cpu,hayo unayoongea yooooote ni kweli na yamenigusa haswa,kama utabiri,basi umeupatia
 
Habari za Ijumaa wana JF wenzangu
Ni matumaini yangu mnaendelea vyema na majukumu yenu ya kila siku

Leo nina kitu kidogo cha kusema kwa wanawake kuhusu wanaume ktk mapenzi
Changamoto kubwa kwenye mahusiano ya kimapenzi ni kupata mpenzi mwenye upendo wa kweli na dhati. Nia ya kila mmoja ni kuwa na rafiki ambaye watatumia muda mwingi kufurahia pamoja kuliko kinyume chake.

Mapenzi ni amani, furaha na upendo na kama moja kati ya mambo hayo yanakosekana kwenye mahusiano hapo lazima lizaliwe tatizo.

Wanawake huwa na matarajio makubwa wanapoanza mahusiano na wanaume, na inapotokea hisia na mawazo yao yameshindwa kutimia huumia sana. Ni ngumu mwanamke kusoma mawazo ya mwanaume haraka kwa vile wanaume si watu wa kuonyesha mapema matarajio ya baadaye kama walivyo wanawake. Mwanaume anahitaji muda wa kufanya maamuzi kabla ya kwenda hatua nyingine, na mwanamke pia hufanya hivyo, lakin tofauti ni matarajio ya wanawake ni ya mapema zaidi

anawake hujisikia vibaya zaidi wanapoona mahusiano yao na wanaume yanashindwa yanashindwa kusogea hatua nyingine, na hofu kubwa ni kwamba kuchelewa huko kunaweza kukawa na hitimisho la kutengana. Wanaona wanaume ni watu dhaifu na wenye uvumilivu mdogo wa kukwepa vishawishi tka kwa wanawake. Hili ni kweli kwa asilimia kubwa ya wanaume. Na kwa sababu hiyo wanataka wanaume wachukue maamuzi ya haraka (sio kwa papara) ikiwa kama njia ya kulinda penzi.

Hivi hapa chini ni viangalizo vitakavyokupa taswira kama kweli mwanaume ana nia ya kweli kota moyoni au hana sababu.

Mkweli toka moyoni
1) Atakutafuta na kuongea na wewe mara nyingi kwa kadri atakavyoweza. Hii inawezekana kwa njia ya simu, email, barua, au hata kutuma salamu za mdomo kupitia watu wengine kama marafiki, ndugu na jamaa.

2) Atatimiza ahadi aliyokupa. Akisema atakutafuta kwa ajiri ya maongezi, kukupigia simu au ahadi nyingine yoyote atafanya hivyo kwa muda aliousema awali

3) Ataonyesha kujali kwa mambo unayoyapenda, kwa mfano kama unapenda kwenda muziki, filamu, aina fulani ya chakula, maua, au mambo mengine unayoyapenda ataungana na wewe ktk kufurahi hata kama itatokea kati ya mambo hayo sio hobi yake

4) Mwanaume wa aina hiyo atakuwa wazi kuonyesha hisia zake kwako, atakuwa wazi kwa kadri awezavyo, hii itakuwa ni pamoja na kukueleza jinsi gani anajisikia anapokuwa karibu na wewe

5) Atakufunza utamaduni wa kujenga urafiki wenye dhamira ya dhati, matumaini ya muungano imara na usiokuwa na tamati kati yenu na ukweli halisi pendo toka moyoni

Aliyekosa ukweli
1) Mwanaume asiyekuwa na nia kwanza atakuwa mgumu kutimiza ahadi alizotoa mwenyewe kwako, atakuwa na sababu nyingi na maelezo marefu yasiyolenga kukutia moyo wala nguvu

2) Wakati mwingine atakuwa mbali na wewe, hatopenda kuongea na wewe kwa kirefu, na akilazimika kuongea atafanya hivyo kwa muda mfupi tu na kukupa sababu kedekede kwanini hapaswi kuongea muda mrefu

3) Anaweza kukuambia atakuja muda fulani lakin asifanye hivyo na bado asikueleze sababu za kushindwa kuja kwake kama hutosumbuka kumuuliza

4) Atakuacha kwenye mtihani wa kutoweza kutambua wala kujua hisia zake kwako (anakupenda au hakupendi)

5) Hatojali hisia zako za kimapenzi, si kwa kukuangalia tu bali hata kwa vitendo kama itatokea amekubali kuwa na wewe faragha

6) Hatojali kukuuliza wala kukushauri kuhusu tatizo lolote linapotokea kwako hata kama atakuwa ameliona

7) Atakuacha huru (si kwa maana ya kukufuatilia) bali kutojali. Hii ina maana kwamba wewe mwanamke ndiye utakayekuwa na jukumu la kumtafuta na usipofanya hivyo kwake ndio furaha.

Ishara nzuri, lakini hizo sio ishara za mwanaume kuwa mkweli au kinyume chake, ungetumia jina jingine pengine 'mwanaume anayekujali' labda ingesaound vizuri coz wenye hizo sifa wanaweza kuwa kinyme chake pia. However YOU CAN NOT STUDY PEOPLE AND RELATIONSHIPS AND GET A PHD, YOU WANNA BE EXPERIENCED GET THE RUBBER ON THE ROAD, PENDA, PENDWA, UMIZA, UMIZWA MWISHO WA SIKU UTAJUA KAMA 1+1 NI TANGANYIKA AU ZENJI! WANAUME HAWASOMEKI, HAWATABILIKI, HAWALIMBATIKI, NI MAUTUNDU YAKO TU! NGOMA IMPATE MCHEZAJI!
 
Back
Top Bottom