Ishauri Serikali Namna ya Kukusanya Kodi kwa Wasiolipa Kodi!

Rais yupo pale kwa niaba ya nani? You are not serious.
Kwa niaba ya Wananchi, Si sawa kulipa kodi, hiyo haipo ndugu na hakuna protocal ya hivyo.
Kwa kifupi rais ni kama Malkia au mfalme, ambapo anapaswa kutunzwa maisha yake yote awapo na atokapo madarakani , yeye na familia yake.
 
Namna rahisi ya kufanya watu wote walipe kodi ni kuwafanya watu wote wafanye kazi rasmi zinazotambulika zenye staha.
% kubwa ya watanzania ni unga unga mwana, hata hizo kazi ulizozitaja watu wanafanya kwa sababu wamekosa kazi rasmi.
Na pia kodi ionekane inafanya nini, nalipa kodi na sioni maendeleo mtaani.
 
Kwa niaba ya Wananchi, Si sawa kulipa kodi, hiyo haipo ndugu na hakuna protocal ya hivyo.
Kwa kifupi rais ni kama Malkia au mfalme, ambapo anapaswa kutunzwa maisha yake yote awapo na atokapo madarakani , yeye na familia yake.
tate usisikitike, Rais utamlipa kiasi gani wakati yeye ndio mkuu wa nchi na haina.?
 
Huu uzi unani gaslight 🤬
 
Tuwe na mfumo mmoa, nunua chukua risiti, uza toa risit, kutokutoa risiti iwe uhujumu uchumi, wakifilisiwa walau watu 500 , watu watajua serikali ipo serios.
Mashine za kutolea risiti bei juu, makadirio ya kodi yapo juu, unategemea vipi kupata kodi! Makadirio ya kodi yawe 'very reasonable' kiasi kwamba mtu mwenyewe aone hata aibu kwa nini asilipe hiyo kodi. Lakini pia ili kuhamasisha matumizi ya hizi mashine za risiti, EFD, serikali iangalie jinsi ya kuwapatia wafanya biashara kwa bei ya punguzo. Hii itasaidia kuwaunganisha wafanya biashara wengi kwenye mfumo wa kodi wa kidijitali na kukusanya mapato mengi zaidi
 
SAwa, kuhusu kupata EFD ya punguzo ama bure maana inatumika kukusanya kodi, JF Toons Mshana Jr kaka yangu amewahi kushiriki mikutano mingi ya wana habari na anajua kabisa hizi ukinunua kadri unavyotumia hela yako inarudishwa.
Lakini mamlaka zitachukua na kufanyia kazi.
 
Suala lingine kwenye biashara zetu kuna msururu mrefu wa wadai kodi. Halimashauri (leseni ya biashara), ushuru wa usafi, fire extinguisher, kodi ya mapato TRA - tena hawa kodi mixer (mapato, stamp, withholding kwa wenye ofisi za kupanga) nk. Ukiangalia hizi zote ni eidha taasisi za serikali au mawakala. Kwa nini kusiwe na kodi moja tu inayokusanywa mfano na TRA, then hawa wengine wote wakapata mgao wao kutokea huko TRA? Yaani hii ni kupunguza usumbufu kwa wadai kodi kuwa wengi na kupunguza mianya rushwa
 
Ni kweli, ukitaka fremu hataka ni Zingiziwa shambani ulipe kodi zote utalipa kodi zaidi ya 15 huku aliyepanga barabarani halipi hata moja na anapanga mbele ya fremu yako, Raisi akisikia hili atakaa na kamishna wa TRA wabadili sheria mapema kabisa kupitia bunge.
 
Nje ya mada
kwa sababu za vita vya irani na wapinzani wake serikali ingepeleka mjadala bungeni wa dharura na mapendekeza ili maamuzi ya jadiliwe
VAT ilipaswa ishuke hadi 13%, Kenya tayari wameshusha kutoka 13% hadi 8%
 


Binafsi nafikiri mipango miji wetu ndio wanafanya mambo mengi yawe magumu; hata sijui wanafanya kazi gani? tunaona majumba yana jengwa barabarani, petro station kama uyoga kila pahala???
Kwa wenzetu wanaojua maana ya kukusanya kodi; Biashara nyingi ulizotaja zinawekewa maeneo tofauti tofauti yanayofikika na kujengewa vibanda rafiki na huduma za vyoo na maji zinakuwepo; watu wanalipa kodi bila shida
Huku kwetu; haijakaa sawa sawa kulipisha mtu kodi wakati amepanga mboga barabarani? Analisha watu chakula barabarani/ chini ya mti? anauza scraper uani kwa mtu, nk nk nk ndio sababu watu inakuwa vigumu kuwashawishi walipe kodi....

Hao wanaozunguka bar, ungewatoa kwani wengi wao wanauwezo mdogo sana lakini pia; hiyo kazi ni ngumu sana, Isiikie tu ukiwa nyuma ya key board.
 
Wakati tunapanga njia za Kukusanya, kuna watu wanapanga njia za kutumia lavishly, tunawaona na tunao na wengine ni Jamaa zetu wa karibu, tunajua historia zao na mifumo iloyopo halafu hakuna mtu anayeweza kuwafanya chochote, hicho Tu ndio kinachonifanya nikose confidence ya kutoa njia nzuri za Kukusanya mapato, guts zinakataa kabisa.
 

Inawezekana hizo sekta zikarasimishwa taratibu na kutambulika kimfumo
mfano mamalishe na wakaanga chipsi wanaweza kulipia vibali au vitambulisho na sio kulipa kodi
mafundi ujenzi wa nyumba, umeme, maji, simu, mbao, magari hawa watawekwa ktk makundi maalumu na kusajiriwa na kulipa vibali
Saluni za kiume na za kike na zile huduma za kukanda viungo zote zitakuwa zinapewa vibali ambavyo watalipia kwa mwaka

suala la mashine za EFD ni changamoto nyingi hazitumiki, wateja wengi hawana elimu ya umuhimu wa risiti
Mtoa mada upo sahihi
 
TRA Ijikite katika kutoa elimu zaidi Kwa mlipa Kodi, Kila mtu awe proud na ajisikie furaha na amani kulipa Kodi stahiki kiufupi dhana ya Magufuli ya uzalendo ilikua superb Kwa baadhi ya matatizo nchini
 
TRA Ijikite katika kutoa elimu zaidi Kwa mlipa Kodi, Kila mtu awe proud na ajisikie furaha na amani kulipa Kodi stahiki kiufupi dhana ya Magufuli ya uzalendo ilikua superb Kwa baadhi ya matatizo nchini
Elimu kwa mlipa kodi ni kubwa sana, kila kona, sasa umepeleka ngombe kwenye maji imekataa kunywa, si unailazimisha?
 
Elimu kwa mlipa kodi ni kubwa sana, kila kona, sasa umepeleka ngombe kwenye maji imekataa kunywa, si unailazimisha?
Hahaha ni kweli ng'ombe hazielewi ila nachojua ni kwamba hizo ng'ombe ni chache sana zenye uelewa na masula ya kodi Kuna zingine ukikutana Nazi malishoni hata haijui rate ya kodi yake ni kiasi gani yenyewe inachojua ni kupinga tu. Mi binafsi nna kishughuli flani nafanya nilikuja kugundua kuwa Kodi ya mwaka mzima ni Tsh120000 tu Hadi nikajicheka coz kwenye shughuli hiyo Kwa mwaka unagenerate millions.
 
Napendekeza tulipie na kodi ya kuwa hai...mtoa mada kama upo serious jitafakari dunia ya leo si ya kuwaza kodi ikujengee nchi.
Rasilimali tulizonazo zingesimamiwa uzuri hizi kodi wananchi wangechangia bila kuvutana mashati.
 
Napendekeza tulipie na kodi ya kuwa hai...mtoa mada kama upo serious jitafakari dunia ya leo si ya kuwaza kodi ikujengee nchi.
Rasilimali tulizonazo zingesimamiwa uzuri hizi kodi wananchi wangechangia bila kuvutana mashati.
Kodi kazi yake ni ulinzi na maendeleo na si zawadi ya kununua magoli. Ukitaka matumizi yabadilishwe mtume mbunge wako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…