Ishauri Serikali Namna ya Kukusanya Kodi kwa Wasiolipa Kodi!

Ishauri Serikali Namna ya Kukusanya Kodi kwa Wasiolipa Kodi!

Napendekeza tulipie na kodi ya kuwa hai...mtoa mada kama upo serious jitafakari dunia ya leo si ya kuwaza kodi ikujengee nchi.
Rasilimali tulizonazo zingesimamiwa uzuri hizi kodi wananchi wangechangia bila kuvutana mashati.
Kila nchi unayoipenda duniani imejengwa na kodi
 
Rais yupo pale kwa niaba yetu , hawezi kulipa kodi maana sisi tunamlipa yeye. Ni kama kuweka wela mfuko huku na kuzitoa kule.
Kulipa kodi kunatakiwa kuwa kwa watu wote. Kama ilivyo kwenye sheria, no one should be above the law. Kila mtu alipe kodi.
 
Nafikiri,
kuzidi kung'ang'ana kuchukua pesa za watu mfukoni kamwe haiwezi kuwa permanent solution ya kuongeza pato la taifa.
Kama mahitaji yanaongezeka kila siku sasa si itahitaji kuongeza kodi kila siku?
Nani anayeumia hapo?

Tunahitaji kubadili mifumo completely ili kukuza pato la taifa.

Kutoka economy ya kuuza malighafi kwenda economy ya viwanda na value addition.

Kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha biashara na utajiri.

Kutoka kufikiria kupata hela ya kula leo kwenda kujenga productivity na capital ya muda mrefu.
 
Mbunge yupi?
Sipigi kura mimi zungumza wewe unayekusanya maoni ya kukusanya kodi.
Tunaomba maoni yako TRA na Wizara ya fedha wapo kwenye huu uzi, serikali ikikusanya vyema kosi hata wewe utapata unafuu wa Maisha.
Tunahitaji kuongeza mishahara ya Walimu na watu wa ulinzi wa nchi, hatuwezi bila kodi.
 
Tunaomba maoni yako TRA na Wizara ya fedha wapo kwenye huu uzi, serikali ikikusanya vyema kosi hata wewe utapata unafuu wa Maisha.
Tunahitaji kuongeza mishahara ya Walimu na watu wa ulinzi wa nchi, hatuwezi bila kodi.
Ninazo kodi chungu nzima nalipa,waumize vichwa kwa wanazokusanya sasa waforcus na mipango maendeleo kuliko matumizi zaidi.
 
"Serikali corrupt haikusanyi kodi ,itabaki kufukuzana na watu barabarani" - Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 1995 Kilimanjaro Hotel.
 
Ya sasa haipo hivyo na ina nia njema, ndio sababu tuishauri.
Mwalimu Nyerere alikuwa mbele ya Muda .

Kama wanataka kodi waache kufukuzana na watu wadogo wagodo ,kodi kubwa kubwa ambayo inaweza kuendesha nchi wameshawapa wazungu/wachina bure au kwa faida ndogo sana wakirubuniwa na vipande vya pesa kuuza rasilimali.

Tuwakamate wote waliotuingiza mkenge wa kuuza mali zetu.

Tusitishe mikataba mobovu yote ya uporaji rasilimali zetu ,hapo tutapata fedha na kuacha kukimbizana na wamachinga.
 
Swali?kodi wanazozikusanya zinatumikaje???
Je wananchi wanaona wanatendewa haki kwa matumizi na kodi wanazolipa???

Ova
 
"Serikali corrupt haikusanyi kodi ,itabaki kufukuzana na watu barabarani" - Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 1995 Kilimanjaro Hotel.
Kwa wenzetu huko duniani
Kodi unalipa mwenyewe
Bila ya kushurtishwa,maana kodi yako unaona kabisa inatumika kwa usahihi

Ova
 
TRA ni wakala wa kukusanya kodi kwa niaba ya Serikali, lakini pia zipo serikali za Mitaa na mamlaka zingine.
Ishauri Serikali yako pendwa namna ya kukusanya kodi kwa watu wafuatao ambao wanaingiza malaki na milioni kwa siku lakini hata leseni ya Biashara hawakati:-​
  1. Wauza viatu , urembo na nguo wanaozunguka Bar na sehemu za starehe:- Hawa watu wananuanua kiatu KArume au Kiboriloni/Memorial na kuuza mara mbili ya bei, kwa siku anauza pea 10 mpaka 15 na hana risiti wala leseni, anaitwa maachina wakati kuna mwenye fremu analipa Pango, Leseni , umeme, ulinzi, Taka, Osha, WCF na hauzi kama huyu machinga.​
  2. Wauza Chakula KAriakoo, wanaopanga barabarani: Mwanaume anakuja na kirikuu amejaza Safuria 5 kubwa za kulisha zaidi ya watu 700 , anauza chakula kwa Tshs 3,000/= na kinaisha chote, analipa 500 tu ya kupaki kiirikuu , the rest ni faida kwake at the same time kuna mwenye Ka-restaurant, ana leseni , TMDA, OSHA< TAKa,Ulinzi, TMDA N, TRA KILA MWEZI NA HAUZI SAHANI 30 KWA SIKU, .​
  3. MAFUNDI SIMU VIBARAZANI NA WENYE KUJIBANZA NDDANI YA KIGOLI CHA MTU: Huyu simu akitengeneza moja tu, service charge ya chini ni elfu 20, kwa siku ana lakinii mbili, halipi kodi yeyote, na kuna watu wanauza simu , wanawapangisha hawa mafundi ndani ya ofisi zao na kula kodi badala ya seruikali wakat.​
  4. Wauza ugoro, shisha na kuchesha kamari: Ukifika kinondoni biafra pale kituo cha daladala kuna mtu anauza shisha, ana kamari, anauza bia na pombe zote 24/7 wakati sehemu nyingine ni marufuku kuuza pombe asubuhi, halipi kodi yeyote na kibanda kinaja wahalifu wakati wenye Pub ndogo tu wana kodi zaidi ya 8.​
  5. Daladala: LATRA itoe mashine zitazokuwa simple , abiria walipe na kupatiwa EFD receipt, hii ni kwasababu Eicher ya Mbagala ilikadiriwa kubeba abiria 40 lakini likotoka kawe lina abiria 85 , waliosimama ni wengi kuliko waliokaa na nauli ni ile ile .​
  6. Special Hire: Haya magari yalikuwa yanapaki pale Biafra kabla ya hekma kuona ni bora kuuza uwanja kwa mabebu. Hawa wanapaswa walipe kodi kadri wanavyoingiza tofauti na wanavyowekewa flat rate.​
  7. Washehereshaji/Mc : Wanaosherehesha harusi, misiba, tuzo kwa siku analipwa 2,000,000 milioni mbilikwa uchache, kwa wiki ana sherehe mbili mpaka tatu, huyu mtu ndio utaona wanaishi lavish life na wanalipa kodi sawa na mama aliyeajiria manispaa kufagia barabara. TRA iwape Mashine, walipe kwa sherehe na siyo flat rate.​
  8. Mighahawa ya Masaki/ Morroco Square/Oysterbay: Hawa wanalipa kodi TRA ila , soda 5000 haina risiti, wanauza chkulaelfu 50 hakuna risiti, sasa serikali inajuaje kuwakadiria? WAtoe risiti ili Mama apate fedha za kuendesha nchi.​
  9. Wanaoziba Pancha/ Fundi tairi? Pale Magomeni Usalama / mkabala na kituo cha mwendokasi kuna mtu anaziba pancha hata leseni ya biashara hana, hana kodi ya pango kwakuwa ni nyumba ya uridhi mda wote magari yamejaa yanabadili tairi mpya, wanaziba pancha na kazi kama hizo, daladala zinajaa hapo usiku mpaka asubuhi na halipi chochote, ni mita 100 tu kutoka manispaa ya kinondoni[Meya huwa haoni maana gari yake ina tinted] lakini basi vijana wake wanaoana.​
  10. Car wash: Kwa sasa kuosha gari nje tu bil NDANI WALA CHINI ni elfu 10, kwa siku mtu aosha gari 30 kwa uchache, analipa kodi sawa na muuza ubuyu kwenye beseni, si sawa, hawa wawe na mashine za EFD kwa kila gari ijulikne na pia mapato yao ya mwezi yajulikane.​
  11. Msaada wa Kisheria:- Hiz NGO zimekuwa utitiri, Ukieenda mahakama ya Familia pale Temeke utakuta UDSM legai Aid, LHRC, WILAC na nyingine nyingi wanajinasibu kutoa msaada wa kisheria ila ukweli ni kwamba wanachukua watu wenye uwezo wa kulipa mawakili. Mtu anakuja anataka mirathi, dhamani ya miradhi inafika milioni 700 ila anataka msaada, wanapewa msamahamaha wasilipe ada za serikali lakini ukweli ni ukwepaji wa kodi, hawa watu waangaliwe kwa jicho la tatu.​
  12. Guta/Baiskeli za Guta: Ha wapo kwenye masko na wanafanya inazofanya kirikuu, hawalipi hata dhumuni, hawakamatwi na trafick maana hawana registration number, waangaziwe.​
  13. WAUZA CHENJI VITUO VYA DALADALA.: BOT hairuhusu kufanya biashara ya fedha bila leseni, yet najua watu wa BOT wanakaa Masaki na mbezi ya chini hivyo huwa hawaoni hizi biashara: Hawa ndio wanaleta scarcituy ya fedha ndogo ndogo mtaani. Wanazikusanya kwa mandoo zinakaa ndani, wanauza kwenye vituo vya daladala, hawalipi chochote na hawana leseni, yetu wanaonwa na kuachwa.​
  14. Wauza Used/screpa Tandale / Temeke na Ilala: Spea ndogo mtumba unauziwa milioni 5 halipi kodi zaidi mmasai anayelinda pale usiku, wakati mtu wa kariakoo ana kodi kibao kwenye spea hiyo hiyo.​
  15. WASUSI:Uzuri TRA na Hazina kuna warembo sana na kila jumamosi wanabadili staili ya nywele, wanajua wanavyolipa pale mwenge kwa msusi , kusuka mtu mmoja ni kama 60,000 na wapo wengi kwa siku wanasuka watu 10 mpqkq 15 na halipi zaidi kodi ya pango lakini serikali hamna kitu na BRELA WAMELALA BADALA KUZINGATIA SHERIA KWAMBA KILA BIASHARA LAZMA JINA LIANDIKISHWE?​
  16. brela/ watumishi brela: Wanapata mshahara mwisho wa mwezi lakini pia wanafungua makampuni na kuchaji fedha, wao wanapokea laki 5 kwa kampuni wakati kwa mawakili wanaolipa kodi ni milioni moja na nusu, hawa wanatumia muda mwingi kufanya "vimeo" kuliko kazi za umma.​
  17. Bajaj zisizo Bolt: Baja imeundwa kubeba watu 3 ila inabeba watu 5. Bajaj inachaji mtu mmoja tshs 4000 kutoka Tegeta mpaka Posta, hizo fedha wangekuwa wanlipa kodi wangesaidi a serikali kujenga makazi ya watumishi hasa Polisi na Madaktari wakae karibu na vituo vya kazi.​

ONGEZA WENGINE TUJENGE NCHI YETU TANZANIA:-
Hao walalahoi msiwasumbue kabisa wamechoka sana akili,MISHAHARA IPUNGUZWE,SEREKALINI,BUNGENI N.K.
 
Kwa wenzetu huko duniani
Kodi unalipa mwenyewe
Bila ya kushurtishwa,maana kodi yako unaona kabisa inatumika kwa usahihi

Ova
Ni kweli na ikizidi unarudishiwa ,huku kwetu tuliochoka ndiyo tunakamuliwa kodi kwa kwenda mbele ila matajiri/wanasiasa hawalipi kodi kabisa.

Mfanyabiashara anakatwa kodi baada ya kutoa matumizi yote yaani ile faida ndiyo inakatwa kodi ,sisi tuliochoka tunatozwa mzigo waote kupitia direct and indirect taxes...Ukija kwenye PAYE inalambwa kabla hata ya kutoa madumizi yake ya msingi.
 
Ni kweli na ikizidi unarudishiwa ,huku kwetu tuliochoka ndiyo tunakamuliwa kodi kwa kwenda mbele ila matajiri/wanasiasa hawalipi kodi kabisa.

Mfanyabiashara anakatwa kodi baada ya kutoa matumizi yote yaani ile faida ndiyo inakatwa kodi ,sisi tuliochoka tunatozwa mzigo waote kupitia direct and indirect taxes...Ukija kwenye PAYE inalambwa kabla hata ya kutoa madumizi yake ya msingi.
Swadakta

Ova
 
Back
Top Bottom