Ishauri Serikali Namna ya Kukusanya Kodi kwa Wasiolipa Kodi!

Napendekeza tulipie na kodi ya kuwa hai...mtoa mada kama upo serious jitafakari dunia ya leo si ya kuwaza kodi ikujengee nchi.
Rasilimali tulizonazo zingesimamiwa uzuri hizi kodi wananchi wangechangia bila kuvutana mashati.
Kila nchi unayoipenda duniani imejengwa na kodi
 
Rais yupo pale kwa niaba yetu , hawezi kulipa kodi maana sisi tunamlipa yeye. Ni kama kuweka wela mfuko huku na kuzitoa kule.
Kulipa kodi kunatakiwa kuwa kwa watu wote. Kama ilivyo kwenye sheria, no one should be above the law. Kila mtu alipe kodi.
 
Nafikiri,
kuzidi kung'ang'ana kuchukua pesa za watu mfukoni kamwe haiwezi kuwa permanent solution ya kuongeza pato la taifa.
Kama mahitaji yanaongezeka kila siku sasa si itahitaji kuongeza kodi kila siku?
Nani anayeumia hapo?

Tunahitaji kubadili mifumo completely ili kukuza pato la taifa.

Kutoka economy ya kuuza malighafi kwenda economy ya viwanda na value addition.

Kutoka kilimo cha kujikimu kwenda kilimo cha biashara na utajiri.

Kutoka kufikiria kupata hela ya kula leo kwenda kujenga productivity na capital ya muda mrefu.
 
Mbunge yupi?
Sipigi kura mimi zungumza wewe unayekusanya maoni ya kukusanya kodi.
Tunaomba maoni yako TRA na Wizara ya fedha wapo kwenye huu uzi, serikali ikikusanya vyema kosi hata wewe utapata unafuu wa Maisha.
Tunahitaji kuongeza mishahara ya Walimu na watu wa ulinzi wa nchi, hatuwezi bila kodi.
 
Tunaomba maoni yako TRA na Wizara ya fedha wapo kwenye huu uzi, serikali ikikusanya vyema kosi hata wewe utapata unafuu wa Maisha.
Tunahitaji kuongeza mishahara ya Walimu na watu wa ulinzi wa nchi, hatuwezi bila kodi.
Ninazo kodi chungu nzima nalipa,waumize vichwa kwa wanazokusanya sasa waforcus na mipango maendeleo kuliko matumizi zaidi.
 
"Serikali corrupt haikusanyi kodi ,itabaki kufukuzana na watu barabarani" - Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 1995 Kilimanjaro Hotel.
 
Ya sasa haipo hivyo na ina nia njema, ndio sababu tuishauri.
Mwalimu Nyerere alikuwa mbele ya Muda .

Kama wanataka kodi waache kufukuzana na watu wadogo wagodo ,kodi kubwa kubwa ambayo inaweza kuendesha nchi wameshawapa wazungu/wachina bure au kwa faida ndogo sana wakirubuniwa na vipande vya pesa kuuza rasilimali.

Tuwakamate wote waliotuingiza mkenge wa kuuza mali zetu.

Tusitishe mikataba mobovu yote ya uporaji rasilimali zetu ,hapo tutapata fedha na kuacha kukimbizana na wamachinga.
 
Swali?kodi wanazozikusanya zinatumikaje???
Je wananchi wanaona wanatendewa haki kwa matumizi na kodi wanazolipa???

Ova
 
"Serikali corrupt haikusanyi kodi ,itabaki kufukuzana na watu barabarani" - Mwalimu Julius Kambarage Nyerere 1995 Kilimanjaro Hotel.
Kwa wenzetu huko duniani
Kodi unalipa mwenyewe
Bila ya kushurtishwa,maana kodi yako unaona kabisa inatumika kwa usahihi

Ova
 
Hao walalahoi msiwasumbue kabisa wamechoka sana akili,MISHAHARA IPUNGUZWE,SEREKALINI,BUNGENI N.K.
 
Kwa wenzetu huko duniani
Kodi unalipa mwenyewe
Bila ya kushurtishwa,maana kodi yako unaona kabisa inatumika kwa usahihi

Ova
Ni kweli na ikizidi unarudishiwa ,huku kwetu tuliochoka ndiyo tunakamuliwa kodi kwa kwenda mbele ila matajiri/wanasiasa hawalipi kodi kabisa.

Mfanyabiashara anakatwa kodi baada ya kutoa matumizi yote yaani ile faida ndiyo inakatwa kodi ,sisi tuliochoka tunatozwa mzigo waote kupitia direct and indirect taxes...Ukija kwenye PAYE inalambwa kabla hata ya kutoa madumizi yake ya msingi.
 
Swadakta

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…