Jack Daniel
JF-Expert Member
- Sep 23, 2021
- 2,912
- 12,904
Watu wengi siku hizi wanaishi Kwa presha sana,hii ni kutokana na kuiga mafanikio ya wengine,
Kama vile,Nyumba nzuri,biashara,usafiri wa uhakika na uwezo wa vitu vingi.
Hii inasababisha kufanya mambo Kwa kufuata majira ya mwaka.
Utasikia nataka ifikapo mwakani niwe na hiki au nimefanya hili,na mtu huyu asipofikia matarajio yake,au kuyakosa kabisa, inasababisha hali fulani ya kujikatia tamaa na kulazimisha baadhi ya mambo.
Ikiwemo kukopa kwenye mabenki au Kwa watu binafsi,kuweka rehani ,nyumba,mashamba na hata baadhi ya nyaraka muhimu ili kuendana na kasi aliyojiwekea.
Wakuu,siyo vibaya kuweka matarajio na mipango kabambe,
Maisha yapo tu kulingana na nature ilivyo,utafanikiwa muda wowote,iwe mwezi wa kumi,wa kwanza,mwezi wa nane,yaani ni muda wowote.
Maombi na mitishamba ni dhana na fikira potofu tu ,mafanikio yanakuja Kwa mipango na mikakati,
Mafanikio hayana muda rasmi.
Muda na wakati ukifika utafanikiwa.
Fanya kazi Kwa bidii mwanakwetu.