Ishi vizuri na familia yako hasa watoto wako. Punguza au acha kabisa utemi, ubabe na udikteta

Ila ukumbuke wakikua mapambio yote kwa mama yao. Mimi nawajali ila nimeona kwa familia yangu asilimia tisini ni mama mama mama
 
Ila ukumbuke wakikua mapambio yote kwa mama yao. Mimi nawajali ila nimeona kwa familia yangu asilimia tisini ni mama mama mama
Ni vile unajenga uhusiano wako na watoto wako, watoto wanaweza kutaja baba baba Baba kila wakati
 
Upole usizidi kwenye baya waadhibu(Mithali 23), kwenye furaha jizime data.
 
Huo unao itwa upendo hautakiwi kuingilia mamlaka ya ukuu wako kama kichwa cha familia ,onesha upendo panapo hitajika na pia onesha ukali panapo hitajika ukali unatakiwa kubalansi.
 
Mimi huwa nikiwa safari madogo mda mwingine hawalali wanauliza baba yuko wapi hadi ni waambie laleni nakuja
ila nikiwa kazini hzi za usiku wala hawasumbui.

Ulichosema ni sahihi sana ubabe hauna faida.but huwa namwaga mkong'oto wakizingua hadi waombe po ubaba wa kunipanda kichwani ndo hauna nafasi kabisa
 
Ni vile unajenga uhusiano wako na watoto wako, watoto wanaweza kutaja baba baba Baba kila wakati
Kitendo cha kutimiza majukumu yako kama baba ndani ya familia ni upendo tosha kabisa kwao.
Mm sina mazoea na dingi wangu na wala hakuwa na mazoea na watoto kipindi tunakuwa lakini hilo haliwezi kunifanya nisitambue umuhimu wake kwenye maisha yangu maana ndo alikuwa anashinda juani nile, nisome,nitibiwe nikiumwa, nivae, nisome.
Ukiona mtoto eti hampendi baba yake kwa kisingizio cha eti baba yake hakujenga urafiki naye kipindi cha utoto huyo ni mpumbavu kama wapumbavu wengine.
 
Umesema vyema, kuna kutambua mchango wa baba ukiwa mtu mzima, na kuna kumfurahia baba ukiwa mtoto kutokana na ukaribu wake na yeye. Wanaume pamoja na ubize walionao, wanapaswa kujenga msingi mzuri kwa watoto wao, hasa mahusiano mazuri. Wanawake wanaweza kufaidi matunda ya watoto wao kuliko wanaume, kwa sababu wamama huwa karibu sana na watoto wao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…