magangawarioba
Member
- Feb 24, 2025
- 15
- 9
Ni uanaume wa hovyo uoNiliwahi shuhudia familia moja baba hacheki na wowote ..aliwahi mvua mkewe tisheti yake kwamba hataki mkewe avae nguo zake,sio sox wala boxa..aisee nyie kuna wanaume wa shoka
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ni uanaume wa hovyo uoNiliwahi shuhudia familia moja baba hacheki na wowote ..aliwahi mvua mkewe tisheti yake kwamba hataki mkewe avae nguo zake,sio sox wala boxa..aisee nyie kuna wanaume wa shoka
Ni vile unajenga uhusiano wako na watoto wako, watoto wanaweza kutaja baba baba Baba kila wakatiIla ukumbuke wakikua mapambio yote kwa mama yao. Mimi nawajali ila nimeona kwa familia yangu asilimia tisini ni mama mama mama
Mimi huwa nikiwa safari madogo mda mwingine hawalali wanauliza baba yuko wapi hadi ni waambie laleni nakujaMHADHARA (88)✍️
Ishi vizuri na familia yako hasa watoto wako. Punguza au acha kabisa utemi, ubabe, udikteta, ukatili, na ukali usio na maana kwa watoto wako.
Kama umefikia hatua ambayo ukiwa mbali na familia yako watoto wanashangilia huku wanatamani usirudi milele, ndugu yangu badili mtindo (mfumo) wako wa kuishi na watoto.
Tafuta maisha lakini hakikisha unapata muda wa kukaa na familia yako. Ukiwa nyumbani na watoto jipe muda wa kuwasikiliza. Mtoto anapokuita "baba-baba-baba" wewe itika na uonyeshe kwamba uko tayari kumsikiliza, huenda ana taarifa au jambo jema la kukueleza.
Baba mwema ni yule ambaye akisafiri au akiwa mbali na nyumbani kwake watoto wanamkumbuka baba yao. Kama utawajengea watoto mazingira mazuri ya ukaribu na urafiki, ukisafiri watoto kila mara watamuuliza mama yao "baba atarudi lini".
RIGHT MARKER
Dar es salaam.
Kitendo cha kutimiza majukumu yako kama baba ndani ya familia ni upendo tosha kabisa kwao.Ni vile unajenga uhusiano wako na watoto wako, watoto wanaweza kutaja baba baba Baba kila wakati
Umesema vyema, kuna kutambua mchango wa baba ukiwa mtu mzima, na kuna kumfurahia baba ukiwa mtoto kutokana na ukaribu wake na yeye. Wanaume pamoja na ubize walionao, wanapaswa kujenga msingi mzuri kwa watoto wao, hasa mahusiano mazuri. Wanawake wanaweza kufaidi matunda ya watoto wao kuliko wanaume, kwa sababu wamama huwa karibu sana na watoto wao.Kitendo cha kutimiza majukumu yako kama baba ndani ya familia ni upendo tosha kabisa kwao.
Mm sina mazoea na dingi wangu na wala hakuwa na mazoea na watoto kipindi tunakuwa lakini hilo haliwezi kunifanya nisitambue umuhimu wake kwenye maisha yangu maana ndo alikuwa anashinda juani nile, nisome,nitibiwe nikiumwa, nivae, nisome.
Ukiona mtoto eti hampendi baba yake kwa kisingizio cha eti baba yake hakujenga urafiki naye kipindi cha utoto huyo ni mpumbavu kama wapumbavu wengine.