Ishu ya mitihani kuvuja Serikali ituambie ukweli, Waziri kujichanganya maana yake kuna kitu hakipo sawa

Ishu ya mitihani kuvuja Serikali ituambie ukweli, Waziri kujichanganya maana yake kuna kitu hakipo sawa

BigTall

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2022
Posts
525
Reaction score
1,257
Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Omary Kapinga ndiye ambaye aliyeanza kwa kutoa jibu kuwa mitihani haijafuja tangu mwaka huo, binafsi naona kama kuna kitu hakipo saw ana takwimu zake ndio maana hadi Spika amezungumzia na kuamua kuiweka hoja hiyo pebeni kwa muda

"Suala la uvujaji wa mitihani halipo, mara ya mwisho mitihani ilivuja mwaka 2008. [...] Kinachotokea ni udanganyifu wa mitihani katika baadhi ya maeneo, baada ya mitihani kufunguliwa na kuingia kwenye vyumba vya mitihani."- Naibu Waziri wa Elimu, Omary Kapinga



====================================


Waziri alivyojichanganya suala la kuvuja kwa mitihani Nchini

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omar Kipanga.jpg

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omar Kipanga akiwa Bungeni.

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imesema kuwa uvujaji wa mitihani ulitokea kwa mara ya mwisho Nchini mwaka 2008 na kwamba hivi sasa wanaendelea kupambana na udanganyifu.

Hayo yamesemwa leo Mei 17, 2022 na Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Omar Kipanga wakati akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Singida Mjini (CCM), Mussa Sima aliyehoji mkakati wa kuondoa suala la ukosefu wa maadili linalosababisha udanganyifu wa mitihani.

Akijibu swali hilo, Kipanga amesema uvujaji wa mitihani kwa mara ya mwisho ulitokea mwaka 2008 na ni suala la ukosefu wa maadili na wamekuwa wakitoa elimu.

Amesema mwaka 2011 udanganyifu ulifanyika kwa wanafunzi 9739 lakini mwaka 2021 ni wanafunzi 393 tu walifanya udanganyifu kwenye mitihani.

Amesema wataendelea kudhibiti vitendo vya udanganyifu wa mitihani na baada ya muda watapata mafanikio makubwa kuhakikisha hakuna mtu atakayejihusisha na udanganyifu wa mitihani.

Katika swali la msingi Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Husna Sekiboko amehoji Serikali inachukua hatua gani kukomesha kuvuja kwa mitihani nchini.

Akijibu swali hilo, Kipanga amesema Serikali imekuwa ikichukua hatua mbalimbali kwa lengo la kukomesha tabia ya udanganyifu katika mitihani ya Taifa ikiwemo mitihani ya kumaliza Elimu ya msingi, sekondari na vyuo.

Amesema elimu hiyo inatolewa kwa walimu, wasimamizi wa mitihani na wadau wote wa elimu kuhusu athari za udanganyifu katika mitihani ili kuhakikisha kuwa wanatekeleza jukumu la usimamizi wa mitihani hiyo kwa uadilifu na kwa kuzingatia Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyowekwa kwa ajili ya uendeshaji wa mitihani.

“Hatua nyingine zilizochukuliwa kutokana na udanganyifu katika mitihani ni hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Sheria za nchi,” amesema.

Amesema hatua hizi zimekuwa zikichukuliwa kwa walimu, wasimamizi na wadau wote wanaohusika katika kusimamia mitihani pale ambapo ilibainika pasi shaka kuwa wameshiriki katika kosa hilo.

“Serikali itaendelea kuwachukulia hatua kali kwa mujibu wa sheria kwa wahusika wote wanaojihusisha na udanganyifu wa mitihani ili kuhakikisha kuwa nchi inapata wataalam wenye sifa stahiki,” amesema.

Amesema suala la uvujaji wa mitihani ya Taifa lilijitokeza 2008 haujawahi kutokea uvujaji wa mitihani.

Hata hivyo, Sekiboko ameomba Mwongozo wa Spika akisema kuwa majibu ya Naibu Waziri yana viashiria vya udanganyifu kwani mwaka 2021 yeye (Sekiboko) na wenzake walipewa kazi ya kupitia uvujaji na udanganyifu kwenye mitihani, hivyo si sahihi kusema kwamba mara ya mwisho mitihani kuvuja ni mwaka 2008.

Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson amejibu kuwa atatolea ufafanuzi baada ya kujiridhisha na kazi ambayo kamati aliyokuwemo Mbunge Sekiboko ilikwenda kufanya, lakini akasisitiza kuwa uvujaji wa mitihani ni sehemu ya udanganyifu katika mitihani.
 
Yan unadanganya had unajisahau kuwa unayemdanganya nae alikuwa ni mhusika kwenye hicho unachodanganya.
Hapo spika kaamua tu kumfichia aibu waziri
 
Mitihani ya msingi na sekondari inasimamiwa na askari wenye bunduki utasema watoto ni waharifu.
 
Back
Top Bottom