Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
Mkuu umesoma vizuri zile Qualifications mbili nilizokuwekea kwa picha hapo juu?Hayo maelezo yametolewa kwa kuzingatia kalenda ya kuelekea msimu mpya wa mashindano ya CAF. Lakini tambua kuwa baada ya timu kufuzu hatua ya makundi, CAF hufungua tena dirisha dogo la usajili, kama unakumbuka kwenye dirisha hilo ndilo lililomleta Musonda na Baleke Tanzania.
Narudi kwenye ishu ya Msuva; naomba nikuulize maswali yafuatayo ili ujue ni wapi unakwama kuelewa.
Msuva mpaka sasa kasajiliwa na timu gani inayoshiriki michuano ya CAF? ( hapa ndipo tutakapojua uhalali wa hiyo leseni ya CAF kwa Msuva)
2) kama sheria inafungia hapo kwanini kuna dirisha dogo kwa timu zinazofuzu hatua ya makundi?
Umesoma vizuri nilichokiandika ukakielewa?
Ni kweli Msuva hana timu kwa sasa
Ila kwa mujibu wa vigezo walivyoweka CAF ili mchezaji acheze mashindano ya CAF ni lazima awe na leseni.
Msuva kutokuwa na timu yeyote inayoshiriki michuano ya CAF haifanyi aruhusiwe kushiriki ligi ya CAF bila leseni.
Umeongea kuhusu dirisha dogo lakini kama umesoma maelezo yangu paragraph ya mwisho utaona hicho kitu nimeelezea.