Nguruvi3
Platinum Member
- Jun 21, 2010
- 15,773
- 32,431
Kuna mahali ambapo hujapaelewa kwasababu hufuatilii nyuzi na maandishi ya Mohamed Said kwa ufasaha na kwa uangalifu.sokwe mjadala huu hauna lengo la udini kwa maana ya kubagua! La hasha.
Lengo la uzi huu ni kujaribu kuwapa haki sawa Wale MASHUJAA WOTE WALIFANIKISHA KUTULETEA UHURU KTK NCHI YETU! Suala ni moja hapa!
Unapoongelea pirika za kupigania uhuru basi HUNA BUDI KUYATAJA MAKANISA NA MISKITI KTK HISTORIA HII.
Na hili linatokana na harakati hizo kufanywa na watu waliokuwa na imani hizo na pirika hizo kupitia ktk miskiti na makanisa!Tatizo ni kwamba historia halisi IMEBATILISHWA!
Na kilicho batilisha historia hio ni mfumo mmoja unaotutafuna hapa TZ ULITWAO "MFUMO KRISTO"!
Hakuna ubaya wwt kutaja wapiganiaji wa uhuru wetu kuwa walikuwa ni waislamu au wakristo au wapagani!
Ubaya unakuja pale ambapo utataja imani hizi ili kuonyesha kuwa IMANI YAKO BORA KULIKO NYINGI KTK KUPIGANIA UHURU HUO!!
NA NDICHO ALICHO KIFANYA NYERERE!
Na kama umefuatilia mnakasha huu. Maalim Mohamed Said anajaribu kuuelezea ummah ya kuwa SI WAGALATIA PEKE YAO NDI9 WALIOSHIRIKI KTK PIRIKA HIZO!
LA HASHA! Na WAISLAMU PIA WALIKUWEMO LKN MFUMO KRISTO CHINI YA NYERERE UNAJARIBU KUMUONYESHA NYERERE PEKE YAKE KUWA NDIO SHUJAA!
Na utaona kuwa kuna wenye elimu ndogo wapo humu kuugeuza huu uzi kuwa ni wa kidini na SIO UZI UNAOTAKA KUONYESHA HISTORIA HALISI!
I will give you an example:-
We all know that "GURKAS" MOST OF THEM ARE BUDIST.
Why when there was a demonstration in london regards the "GURKAS" who fought alongside british army since second world war TO BE RECORGNISED, NOBODY SAYS THAT WAS A RELIGIOUS DEMONSTRATION?
How come today when someone decided to show that MUSLIMS DECERVE TO BE RECORGNISED IN TANZANIAN FREEDOM HISTORIES THAT PEOPLE LIKE YOURSELF THINGS "ITS RELIGIOUS BASED THREAD?? WHY??
The only way I can conclude here is PEOPLE ARE JELOUS!
JELOUS OF KNOWING THAT MUSLIMS DID ENDEED PLAY A BIG PART IN TO THE STRUGLE TOWARDS OUR INDEPENDENCE.
Hakuna mtu kasema waislamu ni mahodari kuliko wagalatia!Au ni wao tu ndio walioshiriki peke yao!
Historia iandikwe kwa haki! Thats all brother! And when that happen, we can all chill and relax and may be you guys can drink that dodoma wine and we can have our sharbati and faluda as always!
Teh teh teh teh.
Katika nyuzi zilizopita tumejadili na watu wengi sana walikubali kuwa historia iliyokuwepo haikuwa kamili kwasababu kuna matukio, watu na vitu havikuorodheshwa. Tukasema ni vema ikaandikwa kwa uhalisia wake.
Hilo limesemwa
Mohamed Said anachokiandika ni kusahihisha makosa kwa makosa makubwa zaidi. Kwa mfano, katika maandishi yake huwezi kumuona akizungumzia role ya Cecil Matola akina Kyaruzi na wengine.
Amejikita kuwakuza watu kwa msingi wa dini huku historia hiyo ikielemea upande wa dini kwa kuruka viungo muhimu sana.
Mfano wa pili, Mohamed Said alificha kuhusu mchango wa Mary Knoll shirika la kikkristo huku akiwananga kuwa wao walishirikiana na wakoloni. Hapa akimnanga zaidi Nyerere kumuonyesha kuwa hakuwa na lengo la Uhuru alikuwa opportunist. Amemnanga sana Nyerere kwa elimu, imani na hata sehemu anayotoka(ushahidi upo)
Kibaya zaidi kaenda mbali hadi kumdhalilisha kuhusu vitoweo eti akiandika historia kamili.
Mohamed akaenda kafuta baadhi ya matukio ili kudhalilisha watu. Akazua habari ambazo zimethibitika kuwa si za kweli (ushahidi wa maandishi yake upo).
Lakini muhimu sana ninalotaka wewe uelewe ni kuwa Mohamed Said haandiki historia ili watu wajue tu, ana lake jambo.Katika maandishi yake ametumia historia ya kupamba waislam halafu anachomeka hoja kuwa dhidi ya kuwa wao wamepigania uhuru sasa wamegeuzwa kuwa raia wa daraja la pili.
Hii maana yake ni kuwa historia anayosema imelenga kuuandaa mazingira ya hoja zake za waislam kukandamizwa, kudhulumiwa licha ya kuwa wao wamepigania uhuru.
Hilo ni tofauti na kauli zako hapo juu kwasababu wewe unalenga historia iwe kamili wakati yeye analenga historia iwe silaha. Hapo ndipo watu wengi sana wanatofautiana na Mohamed.
Hakuna anyekataa kuwa sehemu kubwa ya wakazi wa Dar walikuwa waislam. Lakini pia haina maana kuwa uhuru ulipiganiwa kuanzia Dar pekee.
Mbuwane Syke alipokwenda kumpiga mkwawa kama mamluki ni kwasababu Mkwawa alikuwa anapinga ukoloni. Sasa hii ya kutenga kifungu cha wazee wa Kariakoo na kusema bila wao yasingetokea si kweli.
Ni kutokana na hayo ndio maana niliuza kama lengo ni kuwaenzi wazee watu wanashauri nini.
Hakuna mwenye hoja hadi zilipotafutwa njia za kusema viandikwe vitabu.
Ukweli ni kuwa watu wanataka wale wanaotajwa wapewe nyadhifa kama sehemu ya shukran na wewe ni mmoja wao uliyesema familia ya Kiyate iulizwe ienziwe vipi. Medali zinatolewa nini tena kinatakiwa?
Ni makosa sana kusema watu wanapinga Uislam kama anavyosema Chamvinga.
Ukweli ni kuwa watu hawataki historia ipotoshwe, itumike kwa masilahi au imani ya dini isingiziwe ili kuzuia watu wasiwe huru kuchangia.
Kwa mfano, wapo wanaoelewa ukweli tunaousema kuhusu MS lakini hawawezi kusema MS kakosea kwani kufanya hivyo ni kuwa dhalimu na kuukana Uislam. Wamesahau MS haandiki historia ya Uislam anaandika historia ya Tanganyika ambayo waislam ni sehemu yake.
Ukimsoma MS lengo lake ni kujenga mazingira fulani kwanza ili hoja zake zinazomchonyota zipate kusimama.
Sisi wengine tunasema la hasha! historia iandikwe kwa taratibu na kanuni zake kama ilivyo.
Dini ziwe sehemu ya historia kwasababu ni sehemu ya, lakini zisiwe kama ndiyo historia yenyewe kwasababu zilikuwepo kabla ya harakati.
Wazee wetu wamesema '' walipigania uhuru kumkomboa mwafrika'' Sasa hili la kupigania uhuru kwa ajili ya waislam Mohamed Said kalitoa wapi
Nakushukuru kuwa umezungumza kitu nikakusoma.