Ritz
JF-Expert Member
- Jan 1, 2011
- 51,303
- 40,190
Nguruvi3.chamvinga , kama unaongelea suala hili katika mizania ya dini unajichanganya. Nimesema huko nyuma suala la uhuru litenganishwe na dini kwasababu njema kabisa.
Pamoja na matumizi ya dini kuhalalisha hoja zako bado umejichanganya. Hoja yako katika kifungu cha mwisho unaanisha kujenga msimamo wako katika dini. Ukifika hapo lazima useme ukweli kwasababu dini hiyo uliyoitumia kuweka msimamo ndiyo inayoagaiza ukweli. Kwabahati mbaya umekiuka msingi ulioujenga mwenye. Nitaeleza
Umesema Nyerere alifanyiwa mema na kisha kuwageuga wenzake baada ya uhuru.
Usichosema ni kuwa hao waliotenda wema baadhi yao ndio walimtenga kwasababu ya imani yake mwaka 1957 na hata kupelekea kuanzishwa kwa AMNUT na kisha kujificha katika chaka la EAMWS kama Sheikh Amir.
Umeshindwa kusema ukweli kuwa Nyerere aliwatendea wema kama kumtaka Sheikh Amir awe sehemu ya baraza la mawaziri na sheikh kukataa.
Umeshindwa kueleza kuwa waliokorofishana na mwalimu si wote ni baadhi kwasababu zile zile za kutaka kumuondoa madarakani si kwa njia ya kura bali ya imani yake.
Kwakushindwa kusema hayo msimamo wako wa kidini haukufuata maadili ya dini ya ukweli.
Haukufuata maadili kwasababu hata vifungu unavyotumia kuhalalisha ubaya bado vinajichanganya. Nitafafanua:
Malalamiko ya kuonewa yalitakiwa yasemwe na walionewa kwa maana ya kuwa wao ndio waathirika.
Hakuna mahali katika rekodi Mshume Kiyate alipita barabarani akitangaza msaada wa sh 200 na mboga kwa omba omba Nyerere.
Hakuna mahali ambapo hadi sasa tumeona au kuonyeshwa kuwa Abdu Sykes alipita bara barani akieleza chumba alichomwachia Nyerere na Mkewe.
Ninaamini kuwa wazee hawa alifanya kwa nia njema kabisa na wala si katika kusenganya.
Anayeleta hoja ya kusengenya ni Mohamed ambaye ni msimuliwaji. Pengine angeandika katika lugha njema isingeleta taabu, ameandika katika lugha dhalili kwa Nyerere na hivyo kukiuka kanuni ya Jarhu wata'adir.
Ingeelezwa kuwa wazee hao walimfadhili Nyerere wakati hana kazi hiyo ingesomeka kama Jarhu Wata'adir. Lakini inapokwenda hadi kuzungumzia vitoweo na malazi hiyo ni dhalili.
Sijui kama dhalili ni jambo jema naomba msaada wako ili nisije andika nikajeruhi kwa kupindukia(Jarhu wata'adir)
Unaposema Nyerere amejenga misingi mibovu ya taifa hili hapo ume generalize. Misingi gani unayoongelea? Tena unasema JK Kikwete anajitahidi kurekebisha. Umesahau kuwa ni Nyerere aliyejenga mazingira ya JK Kikwete kuwa rais kuanzia utotoni hadi ukubwani kama ilivyo kwa akina Mohamed Said n.k.
Umesahau kuwa kuna marais wawili waliopita kabla ya JM Kikwete ambao kila mmoja alikuwa na mchango wake kwa namna moja au nyingine.
Kisichokuwa na ubishi ni kuwa wote wamefanyakazi katika mazingira aliyeoyajenga Nyerere.
Hakuna anayefanya jambo ambalo Nyerere hakulifanya, hakuna nasimama kwa hili kwa ushhidi wa kutosha!
Hivyo ukiona mtu anavuna jiulize nani alipanda mti huo wa matunda. Au ndio yale ya Tabora mtu kusema huu ni mwembe wangu wakati historia inaonyesha ulipandwa wakati wa Abushir? Nani anakumbuka hilo!
Yote hayo umeyafanya kwa kuvuka mpaka na wala hakuna jarhu mata'adir.
Hakuna uhalali wa kujenga excuse kwa upande mmoja na kuvuka mipaka kwa upande mwingine.
Usiposimama kusema ukweli hapoa utakuwa umekiuka msingi wa kutumia jarhu mata'adir.
Ahsante
Naona unaendelea kupiga ngumi hewani teh teh teh!
Hebu jisome tena ulichokiandika ndiyo utajua nani anajichanganya kati yako na Mujitahidi CHAMVIGA. unasema wanaotakiwa kulalamika kusema wameonewa wale waathirika, ndiyo maana tunakuambia wewe una chuki na Waislam kila dhulma walizofanyiwa na Nyerere kwako unaona sawa, wewe unamtaja Sheikh moja tu Hassan bin Amir kuna masheikh walikuwa mikoani Mwanza, Dodoma, Tabora, Kilwa, Tanga, walikamatwa wala hawakuwa wanasiasa nakutajia tena.
Baada ya kupatikana uhuru kilichofuatia ni kuwakamata hawa masheikh na kuwafunga jela, Sheikh Abdulkarim Abdulwahid, Maalim Popo Saleh, Sheikh Suleiman Masudi Mnoji, Sheikh Jumanne Bias, Sheikh Bilal Waikela, Ali Migeyo, Maalim Matar, Sheikh Nurdin Husein, Sheikh Ali Comorian, Sheikh Al Amin Mafta, Sheikh Hashimu Haji, Sheikh Abdalla Mwamba, Sheikh Amin Abdalla, Sheikh Maftaa, na wengine wengi.
Nguruvi3. sisi Waislam ndiyo waathirika wenyewe hivi unataka Masheikh wasemewe na nani kama siyo Waislam, nyie Maskofu wenu wakipatwa na matatizo wote mnanyanyua midomo yene tena wewe uliandika kuwa kuishambulia serikali ushahidi upo, Masheikh wakipata matatizo unasema wanaotakiwa kulalamika ni waathirika, eboo!! wewe mbona unakesha JF kumtetea Nyerere kwa nini usiwaachie kina Madaraka Nyerere, Makongoro Nyerere na watoto wengine wa Nyerere, wewe kweli kauzu.
Majanga.
Last edited by a moderator: