Islam’s role in Tanzania’s freedom struggle

Wanaukumbi, hapa chini tawawekea historia ya TANU kwa ufupi ambayo iliandikwa Chuo Cha Kivukoni baada ya kutwishwa jukumu hilo na Mwalimu Nyerere, halafu muangalie nafasi za wazee wa Dar es Saaam zipo wapi.

HISTORIA YA TANU

[h=4]2.0 TANU NA HARAKATI ZA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA[/h] 2.1 TANU ilizaliwa katika mazingira yaliyoandaliwa na Tanganyika African Association (TAA):
TAA iliundwa 1948 kufuatia tukio la kutengana kwa African Association (AA) ya Tanganyika na Zanzibar. AA ilizaliwa Dar es Salaam 1927 chini ya uongozi wa Cecil Matola akiwa Rais na Kleist P. Sykes akiwa Katibu. Malengo ya AA yalikuwa ni kupigania haki, maslahi na umoja wa Waafrika. AA ilikuwa na matawi yake makuu Dodoma na Zanzibar. Aidha, AA ilifungua matawi katika miji iliyokuwa makao makuu ya wilaya.
Katiba ya TAA ilitamka wazi kwamba Chama hicho hakikuwa na malengo ya kisiasa. Mwaka 1953 yalifanyika mabadiliko ya uongozi katika TAA. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa TAA. Chini ya uongozi mpya, Katiba ya TAA ilionekana kwamba isingeweza kukidhi malengo ya kisiasa. Mwalimu alipewa jukumu la kuandaa Katiba mpya ya TAA ambayo ingezingatia malengo ya kisiasa. Baada ya uandaaji wa Katiba hiyo kukamilika, haja ya kubadili jina ilionekana dhahiri na majina mengi yalipendekezwa likiwemo la TANU. Nafasi ya TAA ilichukuliwa na TANU iliyozaliwa tarehe 7 Julai, 1954. TANU ilirithi matawi ya TAA, wanachama na viongozi wa TAA katika maeneo mengi.
Waasisi wa TANU ambao walihudhuria na kushiriki katika Mkutano wa kuzaliwa kwa TANU walikuwa 17:

  1. Mwalimu J.K. Nyerere – Rais wa TAA/TANU
  2. Geremano Pacha – Jimbo la Magharibi
  3. Joseph Kimalando – Jimbo la Kaskazini
  4. Japhet Kirilo – Jimbo la Kaskazini
  5. C.O. Milinga – Jimbo la Mashariki
  6. Abubakari llanga – Jimbo la Ziwa
  7. L.B. Makaranga – Jimbo la Ziwa
  8. Saadani A. Kandoro – Jimbo la Ziwa
  9. Suleman M. Kitwara – Jimbo la Ziwa
  10. Kisung'uta Gabara – Jimbo la Ziwa
  11. Tewa Said Tewa – Jimbo la Mashariki
  12. Dossa A. Aziz – Jimbo la Mashariki
  13. Abdu Sykes – Jimbo la Mashariki
  14. Patrick Kunambi – Jimbo la Mashariki
  15. Joseph K. Bantu – Jimbo la Mashariki
  16. Ally Sykes – Jimbo la Mashariki
  17. John Rupia – Jimbo la Mashariki

    1. TANU ilizaliwa baada ya Vita ya Pili ya Dunia:

Katika vita ya Pili ya Dunia (1939 – 1945), Watanganyika walishiriki wakiwa askari upande wa Waingereza. Katika kushiriki huko, baadhi yao walipigana vita nchi za nje, kwa mfano, India, Burma, Madagascar n.k. Wakiwa huko vitani walipata fursa ya kubadilishana mawazo ya kisiasa na askari wenzao waliokutana nao katika uwanja wa vita.
Baadhi ya askari hao wa Tanganyika waliporejea kutoka vitani walikuja na fikra mpya za ukombozi wa Mwafrika. Fikra hizi mpya zilioana na zile za Kituo cha Wasomi wa Kiafrika waliokuwa London. Kituo hicho kilijishughulisha sana na suala la ukombozi wa Mwafrika kupitia midahalo.

    1. TANU ilizaliwa katika mazingira ya vyama vya ushirika:
Katika miaka 1950, wakulima walikwishajiunga na kuanzisha vyama vya kuuza mazao yao ya biashara ili waweze kupata bei nzuri kwa kupunguza gharama ya mtu wa kati ambaye alikuwa ni mfanyabiashara wa Kiasia. Baadhi ya Vyama vya Ushirika vilivyokuwepo kabla ya TANU ni:-

  • Kilimanjaro Co-operative Union Ltd (1933)
  • Ngoni – Matengo Co-operative Union Ltd. (1936)
  • Rungwe African Co-operative Union Ltd. (1949)
  • Bukoba Co-operative Union Ltd. (1950)
  • Lake Province Native Growers Association.
Kwa kuwepo vyama vya ushirika, ujumbe wa TANU kuwafikia wananchi ulirahisishwa. Wanachama wa vyama vya ushirika walijiunga na TANU. Wanachama na viongozi wa vyama vya ushirika waliunga mkono TANU katika madai yake ya kudai uhuru. Baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika walichaguliwa kuwa viongozi wa TANU katika ngazi ya Taifa. Kwa mfano:-

  • Ndugu Nsilo Swai
  • Sir George Kahama
  • Ndugu Jeremiah Kasambala
  • Balozi Paul Bomani
  • Ndugu John Mhavile.
TANU nayo iliunga mkono vyama vya ushirika katika madai yake ya bei nzuri ya mazao yao na kuondoa ushuru wa kahawa uliokuwa unatozwa na Serikali Kuu. Aidha, TANU ilihimiza na kuwahamasisha wananchi kuanzisha na kuimarisha vyama vya ushirika. Kazi hii ya kuhimiza na kuhamasisha wananchi kujiunga na ushirika iliendelea kufanywa na TANU hata baada ya Tanganyika kupata uhuru wake.
Baada ya Uhuru, TANU iliuona ushirika kuwa ni chombo cha kuleta maendeleo hivyo wananchi walihimizwa kuanzisha ushirika katika maeneo ambayo hayakuwa na vyama vya ushirika. Hali hii inaendelea hadi hivi sasa ambapo katika mfumo wa uchumi wa Soko, CCM inauona ushirika kuwa ni chombo cha kumwezesha mwananchi kiuchumi katika kumiliki na kuendesha uchumi wa Taifa lake..

Itaendelea.
 

Shariff Ritz,
Hakika kwa hili umeleta mambo makubwa.

In Sha Allah tunakufuatilia kwa karibu...
 
Ni kusengenya 100%. No doubt

Wickama,
Mimi ushauri wangu ni huu kwako.

Kwa kuwa huyo anaenituhumu kaegemea katika ujuzi wake katika Uislam
nakusihi utafute maana ya ''kusengenya'' kama ilivyoelezwa katika Uislam.

Ningeweza kukueleza maana ya ''kusengenya'' katika Uislam lakini nahofu
utaleta ubishi zaidi na ndiyo nataka ulipate hilo somo kutoka kwengine na
kwenye vyanzo vya elimu ya dini ya Kiislam.

Nimeandika kitabu cha historia ya uhuru wa Tanganyika na kwa mtazamo
wowote ule kusema kuwa Abdu au Dossa kama wafadhili wakubwa wa TAA
na TANU walifanya hiki na kile katika harakati za kudai uhuru huko hata
kidogo si ''kusengenya.''

Achilia mbali kuwa hayo maneno yameandikwa katika kitabu kwa hiyo ni sawa
na kuyasema maneno hadharani huko hakuwezi kuwa ''kusengenya.''

Itafute maana ya ''kusengenya.''
Ikiwa utashindwa tueleze In Sha Allah.


Itakuwa makosa kwangu kujadili suala la ''kusengenya'' wakati huko
''kusengenya'' hakupo.

Hata hivyo nakufungulia mlango wa kupenya ikiwa utapenda.
Tuwekee hapa jamvini maandishi yangu ambayo wewe unaona ni
''masengenyo.''

Weka neno kwa neno kama nilivyoandika na tuwaache wanaukumbi nao watoe fikra
zao.
 
mkuu ameshaweka wazi kila kitu. implication yake ni kushabikia wapenda kuvuruga amani nchini. nampa majibu kwasababu,nataka kuweka wazi anavyoeleweka kwa kupenda kushabikia vurugu.

mkuu tanzaniaa tumeshuhudia makanisa yakichomwa moto, mchungaji akiuwawa na waislamu kule kanda ya ziwa, mapadre wakimwagiwa tindikali, shek arusha akilipuliwa na bomu, na mabinti wa uingereza wakimwagiwa tindikali, shekh ulanga akiagiza watu wauane kule mombasa kenyea. mkuu kutokana na hayo ningeomba unipe tofauti ya shetani na mungu kwa matendo yao.
 

Gombesugu,
Hii umeshusha ni ''heavy.''
Wala sitii neno.

Ramadhani Aziz alimuoa dada yetu marehemu Salama Biti Hussein Juma.
Hivi karibuni nimeliona kaburi lake pale Makaburu ya Kisutu.

Kitwana Luga kila nikipita pale Swahili namkuta kakaa nje ya nyumba yake barazani.

Allah amweke pema peponi.
 
Inaendelea.. HISTORIA YA TANU



    1. TANU ilizaliwa katika mazingira ya vyama vya wafanyakazi:
Lengo kuu la Vyama vya Wafanyakazi lilikuwa ni kutetea maslahi ya wafanyakazi. Baadhi ya vyama vya wafanyakazi ni:-

  • Chama cha Wafanyakazi Serikalini (1929)
  • Chama cha Makuli (1937)
  • Chama cha Wapishi na Madobi (1939)
  • Chama cha Wapishi na Watumishi wa Ndani
  • Chama cha Madereva
  • Chama cha Walimu
  • Chama cha Wafanyakazi wa Reli
  • Chama cha Wafanyakazi Mashambani
  • Chama cha Wafanyakazi Viwandani.
Vyama vya Wafanyakazi viliunda Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (Tanganyika Federation of Labour –TFL) tarehe 10 Oktoba, 1955.
Wafanyakazi kupitia vyama vyao walikuwa na madai yafuatayo:-

  • nyongeza ya mshahara
  • mapumziko ya mchana siku ya kazi
  • umri wa kustaafu na
  • kuondoa ubaguzi katika ajira na huduma za jamii.
Vyama vya wafayakazi vilisaidia kuvunja ukabila na hivyo kuwa chanzo cha umoja. Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi lilisaidia kueneza TANU kwa njia zifuatazo:-

  • Kila Chama cha Wafanyakazi chini ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi (TFL) kilitakiwa kuwashawishi na kuwahimiza wanachama wake kujiunga na TANU.
  • Kila mwanachama wa TANU aliyekuwa mwanachama wa Chama cha Wafanyakazi alitakiwa kulipa mchango wake wa kila mwezi kwa TANU.
  • Vyama vya Wafanyakazi, wakati mwingine kupitia TFL, viliweza kusaidia TANU kifedha fedha hizo zilitokana na michango ya hiari.
  • Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi lilisaidia sana kuleta mwamko wa kisiasa miongoni mwa wafanyakazi.
Vyama vya Wafanyakazi vilifanya yote hayo kwa kuelewa kwamba uhuru ndio ungekuwa suluhisho la kweli la matatizo yao.
Kama ilivyokuwa kwa vyama vya ushirika, baadhi ya viongozi wa vyama vya wafanyakazi walichaguliwa kuwa viongozi wa TANU. Mwaka 1958, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, Mzee Rashid Mfaume Kawawa, alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya TANU. Toka wakati huo hadi hivi sasa, Mzee Kawawa amekuwa na uongozi uliotukuka katika TANU/CCM.
Kwa upande wake, TANU iliunga mkono madai ya vyama vya wafanyakazi na migomo ya wafanyakazi. Katika historia ya Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, mgomo wa wafanyakazi wa Shamba la Mazinde huko Tanga na mgomo wa wafanyakazi wa Kiwanda cha Bia Dar es Salaam ni miongoni mwa migomo maarufu.
Shamba la Mazinde lilikuwa mali ya bepari mmoja wa Kiingereza, mwanachama mashuhuri wa United Tanganyika Party (UTP) aliyewahi kushiriki katika kugombea na kushindwa na mgombea wa TANU katika Uchaguzi Mkuu wa Baraza la Kutunga Sheria mwaka 1958. Wafanyakazi katika Shamba la Mazinde walijiunga na Chama cha Wafanyakazi Mashambani (Tanganyika Plantation Workers' Union – TPWU) ambacho kilikuwa kimeshirikishwa katika Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi. Mmiliki wa Shamba la Mazinde alikuwa na tabia ya kuwafukuza wafanyakazi walioonyesha kupinga UTP na walioamua kujiunga na Chama cha Wafanyakazi Mashambani. Katika harakati za kuwaunga mkono wenzao waliofukuzwa, wafanyakazi wote elfu tatu (3,000) waliamua kugoma na matokeo yake wote walifukuzwa kazi.
Jitihada za TFL kusuluhisha mgogoro huo kati ya Mwajiri na wafanyakazi zilishindikana. TFL na TANU kwa pamoja viliunga mkono mgomo wa wafanyakazi wa Shamba la Mazinde. TANU kupitia Mwalimu Nyerere ilitoa wito kwa wananchi wa Mkoa wa Tanga kuwahifadhi wafanyakazi waliofukuzwa kazi. Wananchi waliitikia wito wa TANU na kuwapokea na kuishi nao. Aidha, TFL na TANU vilitoa wito kwa wananchi kususia shamba la Mazinde. Wafanyakazi hao hawakurejea kazini hata baada ya mmiliki kuwataka kufanya hivyo. Matokeo yake ni kwamba mmiliki huyu wa Shamba la Mazinde hakuchukua muda akafilisika na akarejea kwao Uingereza.
Huu ulikuwa ni ushindi wa TANU na TFL. TANU ilitambuliwa na wafanyakazi mashambani na iliendelea kuimarika. Kwa kuwa ngome ya UTP, na baadaye African National Congress (ANC) ilikuwa huko Tanga pigo hili lilisababisha kifo cha UTP na kuzorota kwa ANC.
Kuhusu mgomo wa Kiwanda cha Bia Dar es Salaam, mgomo ulianza Aprili hadi Juni, 1958. Mgomo uliwashirikisha wafanyakazi wapatao mia tatu (300). Wafanyakazi walikuwa wanadai nyongeza ya mshahara. Wafanyakazi wote waliogoma walifukuzwa kazi na mwajiri.
Katika kuonyesha mshikamano na wafanyakazi katika mgomo huu wa Kiwanda cha Bia, TANU ilichukua hatua zifuatazo:-

  • Ilitoa wito kwa nchi nzima kususia pombe zote za kigeni;
  • Iliwaomba wananchi wa Dar es Salaam kuwasaidia wagomaji kwa kuwachangia chakula na fedha;
  • Iliwaomba wananchi wenye nyumba Ilala kuwapokea wagomaji katika nyumba zao pasipo kuwatoza kodi ya nyumba.
Kama kawaida yao, wananchi waliitika wito na maombi ya TANU. Kwa kupitia migomo TANU ilizidi kuimarika miongoni mwa wafanyakazi.
2.5 TANU ilizaliwa katika mazingira ya kero na adha za wananchi kutoka Serikali ya Kikoloni:

Malalamiko hayo ya wananchi yalijidhihirisha katika maeneo yafuatayo:-

  • Upinzani huko Upare dhidi ya ulipaji kodi kulingana na mapato (Mbiru);
  • Wahehe kukataa kuogesha ng'ombe wao;
  • Waluguru kupinga juhudi za kuhifadhi mapori na kulima matuta;
  • Wafugaji (Wasukuma) kupinga kodi ya ng'ombe na kupunguza idadi ya ng'ombe, kumi kwa kila mia;
  • Wameru wapatao 3,000 walipinga kunyang'anywa ardhi yao na Serikali ya Kikoloni na kuwapa walowezi.
TANU ilitumia kero hizo za wananchi katika kuwaunganisha wananchi na kuwaelekeza namna ya kutafuta haki zao.
Kuhusu ardhi ya Wameru, Katika mkutano wake wa kwanza, TANU ilitoa tamko lifuatalo:-
"Mkutano huu unasikitika sana juu ya mambo yaliyofanywa na Serikali ya nchi hii huko Meru. Mkutano unakubali kwamba Serikali inayo mamlaka kuchukua ardhi ya raia hata kwa lazima ili ardhi hiyo iwe faida ya watu wote kama vile kupitisha reli, barabara, kujenga hospitali, shule au kutumia kwa jambo lingine la manufaa kwa wote. Lakini Serikali haina mamlaka kuchukua ardhi ya raia ili ardhi ile wapewe raia wengine waitumie kwa faida yao wenyewe … Mkutano huu unataka Serikali iwarudishie Wameru ardhi yao ama kuwalipa fidia kwa hasara walizopata kubwa, kwa kufukuzwa kama mahabusu, kama Baraza la Umoja wa Mataifa lilivyokubaliana." [SUP] [/SUP](Historia ya Chama cha TANU 1954 hadi 1977, uk 36).
2.6 Kuenea kwa TANU na Kupata Ushindi:
Dhumuni la kwanza la TANU mwaka 1954 lilikuwa ni kuwatayarisha Watanganyika kujitawala na kujitahidi kwa bidii mpaka Tanganyika imepata uhuru na inajitawala. TANU ilibaini kwamba lengo lake kuu ni kupigania uhuru wa Tanganyika na silaha yake kubwa ni umoja hasa umoja wa Waafrika. Kwa mnasaba huo, TANU iliacha mlango wake wazi kwa Waafrika bila ya kujali kabila, dini, rangi, jinsia na majimbo yao. Toka mwanzo, msingi huu uliifanya TANU kuwa chama cha umma. Hata hivyo uamuzi wa kukifanya Chama cha TANU kuwa wazi kwa Waafrika tu ulikuwa ni uamuzi wa kimkakati tu. Haikukusudiwa kukifanya Chama hicho kuwa cha kibaguzi na kwa hakika kiliendelea kushirikiana na kuwaenzi Waasia na Wazungu walioafiki imani na madhumuni ya TANU.Miongoni mwa Waasia na Wazungu waliokuwa na mtazamo wa kizalendo katika shughuli za kisiasa ni Amir Jamal, Al-Noor Kassim, Derek Bryceson, Babra Johnson na Leader Stirling. Baada ya uhuru (1962), Waasia na Wazungu waliruhusiwa kuwa wanachama wa TANU.
Katika harakati za kuitangaza TANU, njia mbali mbali zilitumika:-

  • TANU ilifungua matawi katika maeneo mbali mbali ya nchi yetu.
  • TANU ilitumia mikutano ya hadhara katika kufikisha ujumbe wake kwa wananchi.
  • TANU ilitumia mikutano ya ndani ya wanachama.
  • TANU ilitumia vyombo vya habari, hususan magazeti, kama vile Sauti ya TANU, Habari za TANU na Mwafrika.
2.7 Jumuiya za TANU za Umoja wa Wanawake, Umoja wa Vijana na Wazazi zilifanya kazi kubwa katika kukieneza na kukiimarisha Chama.
TANU ilianzisha rasmi mwaka 1955 sehemu ya Wanawake wa TANU. Chama kilitambua kwamba mapambano ya kudai uhuru yasingeweza kufanikiwa bila ya kulitumia jeshi kubwa la Wanawake. Chama kilimpata Bibi Titi Mohamed na kumpa jukumu la kuwakusanya wanawake ili washiriki katika mapambano ya kudai uhuru. Sehemu ya Wanawake ilipewa majukumu yafuatayo:-

  • Kupata wanachama wa TANU wengi;
  • Kueneza Chama hasa vijijini kwa moyo wa kujitolea;
  • Kuona kwamba viongozi wa Chama wako salama/ulinzi wa viongozi na
  • Kukipatia Chama fedha kutokana na shughuli halali mbali mbali.
Katiba ya TANU ya mwaka 1954, sehemu ya sita, ilitoa nafasi kwa vijana kuunda umoja wao ili waweze kushiriki kwa ukamilifu katika mapambano ya kudai uhuru. Umoja wa Vijana ulikuwa na majukumu yafuatayo:

  • Kuwaandaa vijana katika uongozi;
  • Kuwahimiza vijana kujitolea kufanya kazi za TANU;
  • Kutekeleza shabaha za TANU;
  • Kuunda makundi ya starehe na maendeleo miongoni mwa wanachama kama vile, elimu, biashara na michezo;
  • Kukusanya habari na kufuatilia mwenendo wa kisiasa nchini;
  • Kushirikiana na vyama vingine vya vijana visivyo na upinzani kwa TANU.
2.8 TANU ilivyopambana na kuvishinda vikwazo na hila za Mkoloni
Jumuiya ya Wazazi (Tanganyika Parent's Association – TAPA) iliundwa mwaka 1955 chini ya Ndugu Lawi Sijaona. TAPA ilikuwa ndiye mtekelezaji mkuu wa Azimio la Mkutano Mkuu wa Tabora lililohusu upanuzi wa elimu. Katika kutekeleza jukumu lake, TAPA ilifungua shule za msingi na sekondari nyingi nchini na kuendesha kisomo cha Watu Wazima. Huu ulikuwa mkakati wa makusudi wa kuwaandaa wananchi kushika madaraka baada ya uhuru.
Jinsi TANU ilivyozidi kuimarika ndivyo hivyo ilivyopambana na vikwazo na hila za Mkoloni:

  • Serikali ya Kikoloni ilipitisha Sheria mwaka 1953 ya kuwakataza watumishi wa Serikali wa mataifa yote kujiunga na vyama vya siasa. Aidha, Tangazo la Serikali Namba 2 la 1954 lilifafanua kuwa hata Sukuma Union kilikuwa ni Chama cha Siasa. Kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Namba 6 la 1954, maafisa wote wa Serikali waliokuwa wanachama wa TANU na waliotaka kuendelea na utumishi serikalini walitakiwa kujiuzulu mara moja. Aidha, Sheria ya vyama vya siasa, 1954, ilitaka kila tawi la TANU lisajiliwe kabla ya kuandikishwa kisheria. Sheria hii iliiwezesha serikali ya mkoloni kusajili au kutokusajili tawi lo lote la TANU.

  • Mara tu baada ya TANU kuundwa, Rais wake Mwalimu Nyerere alitakiwa na Serikali ya Kikoloni achague moja kati ya mambo mawili ama kuendelea kuiongoza TANU au kujiuzulu uongozi wa TANU na kuendelea na kazi yake ya ualimu katika Shule ya Sekondari Pugu. Mwalimu aliamua kuendelea kuihudumia TANU hivyo akalazimika kujiuzulu kazi ya ualimu. Bila shaka, Serikali ya Kikoloni ilidhani kwamba Mwalimu asingejiuzulu ualimu. Katika suala hili, uamuzi wa Mwalimu haukuwa rahisi hasa kwa kuzingatia kwamba kazi ya ualimu ndio alikuwa ameisomea, riziki yake na ya familia ilitokana na ualimu na kwamba kuitumikia TANU wakati huo ilikuwa ni kupambana na Serikali ya Kikoloni na hii ilikuwa ni hatari kubwa. Kwa kujiuzulu ualimu, Mwalimu alipata nafasi kubwa zaidi ya kuihudumia TANU.

  • Mwalimu Nyerere mwaka 1958 alishitakiwa na Serikali ya Kikoloni kwa kosa la kuwakashifu District Commissioners wa Songea, Geita na Musoma. Kwamba kashfa hiyo aliifanya kwa kupitia makala aliyoiandika kupitia Gazeti la "Sauti ya TANU" Toleo Namba 29 la tarehe 27 Mei, 1958. Katika kesi hii iliyosikilizwa na Mahakama ya Dar es Salaam, Mwalimu alihukumiwa faini ya shs. 3,000/= (shilingi elfu tatu) au kifungo cha miezi 6. Mwalimu alilipiwa faini hiyo na TANU.

  • Serikali ya kikoloni pia ilijitahidi kadri ilivyoweza kuwatumia baadhi ya machifu kuwa chombo cha kuzuia uenezaji wa TANU. Machifu walipewa madaraka makubwa zaidi na zaidi ili wajisikie kuwa ni sehemu ya utawala na kwamba TANU ilikuwa na lengo la kuwakosesha maslahi yao. Mwaka 1957, Serikali ya kikoloni iliunda Baraza la Machifu wa Tanganyika (Territorial Convention of Chiefs). Kwa kuwatumia machifu, Serikali ya kikoloni ilitegemea kuwagawa Watanganyika kwa misingi ya ukabila ili kuweza kuwatawala wananchi kwa urahisi zaidi. Aidha, Serikali ya kikoloni ilikuwa na lengo la kuwagonganisha machifu na viongozi wa TANU.

  • Serikali ya kikoloni ilihimiza kuundwa kwa United Tanganyika Party (UTP) ndani ya Baraza la Kutunga Sheria mwaka 1956. UTP ilikuwa ni chombo na Sauti ya Serikali ya kikoloni kwa sababu zifuatazo:-

  1. Uongozi wa UTP uliundwa na Wajumbe wa Baraza la Kutunga Sheria,
"Tanganyika Unofficial Members Organization (TUMO)"

  1. Wajumbe hao waliteuliwa na Gavana na hivyo hawangeweza kupingana na siasa ya Serikali ya Kikoloni.
Licha ya hila na vikwazo vya mkoloni, TANU ilijikuta ina mtihani mgumu wa kuamua kushiriki ama kutokushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza mwaka 1958. Akifungua kikao cha kwanza cha Baraza la Kutunga Sheria mwaka 1956, Gavana Edward Twining alitangaza kuwa Serikali ilikuwa na mpango wa kufanya Uchaguzi Mkuu wa kwanza mnamo 1958. Sharti moja kubwa la uchaguzi huo lilikuwa kwamba kila mpiga kura apige kura tatu: moja kwa Mzungu, moja kwa Mwasia na moja kwa Mwafrika.
Suala hili la kura ya Mseto lilijadiliwa kwa undani katika Mkutano Mkuu wa TANU uliofanyika Tabora mwaka 1958 na kuhudhuriwa na Wajumbe 300 kutoka sehemu zote za Tanzania Bara. Ili kupata nafasi nzuri ya kujadili agenda hii, Mwalimu Nyerere aliomba asiwe Mwenyekiti wa kikao hicho, nafasi yake ilichukuliwa na Mwalimu Kihere kutoka Tanga.
Mwalimu Nyerere aliweza kuushawishi Mkutano kukubali kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa kwanza mwaka 1958. Hoja za Mwalimu zilikuwa ni kwamba kama TANU isingeshiriki, ingekuwa imeshindwa kwani isingekuwa na wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria. Kujitoa katika uchaguzi huo kungekuwa na maana ya kujitoa katika uwanja wa mapambano ambao sasa ungemilikiwa na UTP. Uamuzi wa TANU kushiriki katika uchaguzi huo ulikuwa ni wa busara kwani wagombea wote waliosimamishwa kwa tiketi ya TANU walishinda na hivyo TANU kunyakua viti vyote vya wajumbe wa kuchaguliwa wa Baraza la Kutunga Sheria.
Matokeo ya kukubali kura ya mseto, aliyekuwa Katibu Mwenezi wa TANU, Ndugu Zuberi Mtemvu aliamua kuachana na TANU na kuanzisha African National Congress (ANC) mwaka 1958. Hata hivyo toka kuanzishwa kwake hadi kifo chake, ANC haikupata hata kiti kimoja katika Baraza la Kutunga Sheria. Aidha, Ndugu Mtemvu alibwagwa kwa kishindo na Mwalimu Nyerere katika kugombea Urais wa Jamhuri ya Tanganyika mwaka 1962.
Uchaguzi Mkuu wa pili ulifanyika mwaka 1960. Katika uchaguzi huo, TANU ilijikuta imefanikiwa kupitisha wagombea wake 58 bila ya kupingwa. Kati ya wagombea hao 58 waliopita bila kupingwa, 8 walikuwa Wazungu, 11 Waasia na 39 Waafrika. Tarehe 30 Agosti, 1960 ulifanyika uchaguzi katika sehemu nyingine ambako kulikuwa na zaidi ya mgombea mmoja katika jimbo la uchaguzi. Wagombea viti wote jumla walikuwa 25 kati ya hao 11 walisimamishwa na TANU na walishinda isipokuwa mmoja tu wa kiti cha Mbulu, Chifu Amri Dodo aliyeshindwa na Herman E. Sarwatt ambaye alikuwa mgombea binafsi. Hata hivyo, Sarwatt alikuwa ni mwanachama wa TANU.
Pamoja na vikwazo hivi Msimamo sahihi usioyumba uongozi bora umoja mshikamano ari na dhamira ya wananchi ya kutaka kujitawala vilikuwa chachu iliyosababisha TANU kupata ushindi wa kishindo na kutokana na ushindi huo, Gavana Richard Turnbull alimwomba Rais wa TANU, Mwalimu Nyerere kuunda Baraza la Mawaziri ambalo lilikuwa na jukumu la kuongoza nchi kwa jumla na kumshauri Gavana. Serikali ya Madaraka iliundwa na kuapishwa tarehe 3 Septemba, 1960. Tanganyika ilipata Serikali ya Ndani tarehe 1 Mei, 1961 na uhuru kamili tarehe 9 Desemba, 1961 na Mwalimu Nyerere kuwa Waziri Mkuu wa Kwanza wa Tanganyika huru...

Itaendelea...
 
Ni kusengenya 100%. No doubt

Hapo ki lugha yaani kiarabu pana mambo takriiban matatu au manne yanataka kufanana lakini ni tofauti, nami ntakusaidia hiyo uloandika hapo, lakini mambo yenyewe ni :- 1-FITNA
2-KUSENGENYA
3-HUSUDA,
Sasa ama KUSENGENYA ni kumsema nduguyo kwa yale yanayomchukiza, na kama hayo umsemayo akiwa hanayo basi utahesabika UMEZUA, na hapo sasa kwa wenye fani ama ilimu ya Sharia wanajua nini hukumu ya MZUZI,
Pia hapo pana namna nyengine, si kila kumsema nduguyo inakuwa umezua la, inatizamwa na kitu waita wao
MUQTADHAL HAALI, kwani bila hivyo itakuwa hairuhusiwi hata kufanya masimlizi ya mtu/watu kwani yote tungeliyasema ni UZUZI,
Sasa sijajua Wickama ulilenga nini ama hiyo tafsiri ndiyo umetembea nayo katika hoja yako?
Nadhani nimejaribu kuweka bayana, lakini naamini wengi humu wamebobea, hivyo nataraji marekebisha nilipopunguza ama kuongeza.
 

Hapa 2013 hata mie sijakuelewa vizuri ina maana Sheikh Illunga ndo alitoa amri Sheikh mwenzake apigwe bomu huko Arusha ama umechanganya mambo kidogo as a human being? Na nadhani pia pana Sheikh hukohuko Arusha alimwagiwa Tindikali, sasa hebu niweke sawa ndugu yangu ili hii safari twende nayo vizuri mmoja wetu akabaki porini, vingenevyo hiyo kauli yako ndo itakuwa imezaa maana ya neno UCHOCHEZI.
 

Wabara,
Mie Sheikh wangu ''Riadh Salhin'' lakini nimeiogopa hata kutalii kwa
kuwa nilikuwa na hakika hapa jamvini wapo wajuzi.

Ahsante sana Allah akuzidishie.
Nimefyonza ilm kama Spike Lee anavyopenda kusema.
 

mkuu tukiachana na zile Cult zenye kumpa msaada mungu kuua binadamu wengine ambao inadaiwa mungu yule aliwaumba mwenyewe, ikafikia wakati yeye mungu hawezi tena kuwaua hivyo anakula njama na binadamu ili wamsaidie kuua binadam wenzao.pengine bnadamu wale wanaakili sana na wameshaijua janja ya mungu yule hivyo so rahisi yeye kuwatawala tena.
As a human being, ni kuwa kama utashindwa kutenganisha kati ya shetwain na mungu kwa matendo waweza jikuta ni agent wa shetani bila kujua. mkuu kiimani kuna gap kubwa kati ya mungu na shetani. ikiwa na maana moja ni hasi zaidi wakati jingine ni chanya zaidi. hivyo framework hii ya hasi na chanya inakupa urahisi kujua matendo yaliyo hasi yanamwakilisha nani?. ukichukulia hali halisi ya nchi zetu. hapa nahop ntakuwa nimeeleweka zaidi.
naomba mkuu usichanganye hasi na chanya iliyopo kwenye betri na redio na kwenye masomo ya kemia na fiziksi. ha ha ha ha
 

2013 Mungu na Shetwani ni mbali na hawezi huyo Shetwani tia mguu pale, na hiki kipande ni kipana sana kukufafanulia ukafahamu kwa kirahisi, Muhimu fahamu M/Mungu ni mwenye uwezo uwezao usowezeshwa na chochote chenye kuweza/mtenza nguvu muadilifu/mjuzi
Lakini hapa katika ilimu sote twajua lazima viwango vya ufahamu viwe tofauti ili wapatikane waongozi na waongozwa, haina maana kuwa waongozwa woote huwa hawana akili laa hasha!
Ila ujue nduu yangu 2013 pana mtu ataka afahamu vile alivyo fahamu yeye, na ni shida sana kufahamu vile ulivyo fahamu wewe kuliko kufahamu hakika ya vile inavyotakikanika ifahamike.
 
Wabara,
Mie Sheikh wangu ''Riadh Salhin'' lakini nimeiogopa hata kutalii kwa
kuwa nilikuwa na hakika hapa jamvini wapo wajuzi.

Ahsante sana Allah akuzidishie.
Nimefyonza ilm kama Spike Lee anavyopenda kusema.

Shaikh langu Muhamad Said, mie hujisikia faraja sana pia nisomapo bandiko zako,

Hawa jamaa zetu walituelewa ndivyo sivyo, hoja zimewaisha kabisaa,

Sasa kama muungwa walitakiwa wasipinge kwa ukubwa wa MATUSI bali nao washushe nondo na rejeo zao, badali yake wageuka kuwa washambulizi wa mtu/ Shaikh Muhamad Said,

Pole sana Mzee wetu Muhamad Said, matunda yako yanaonekana, endelea kutugeiya vitu adimu vilivyo kuwa vimetiwa kapuni,

Allaah kareem aendelee kukuzidishia utujuze vijana wako tupo nawe Al akhy.
 
Ritz;7638832]Hakuna makosa kusema waliopigania walikuwa wazee wazalendo wa Kiislam, ambao walikuwa na mapenzi na Nyerere kama kijana wao wala hawakumbagua

Sijui hili tusema ni uzuzi, muktadhal haal au Jarhu wata'adir.
Ritz anasema hakukuwa na ubaguzi, Mohamed anasema ulikuwepo. Hapo lazima kuna uzuzi kwa mmoja wenu
Ritz anasema walikuwa wazee wazalendo wa kiislam, wazee wanasema hapana hakuna kubaguana! hii ni muktahal haal

Wakati Ritz anasema hayo Mohamed anampinga lakini kwa kutumia Jarhu wata'adir

Nipo pembeni natazama watu wanaongea na kujibiziana wenyewe! wazungu wanasema 'Friendly fire''

cc chamvinga, Wickama
 
Last edited by a moderator:
Haya maneno siyo yangu ni maneno ya Nyerere takuwekea bahati nzuri mie kwenye huu mnakasha nimejikita sana kumnukuu Nyerere, mwenyewe kama reference.

Msome vizuri Mohamed Said ukimsoma kwa chuki hauwezi kumuelewa.
 
Last edited by a moderator:
Haya maneno siyo yangu ni maneno ya Nyerere takuwekea bahati nzuri mie kwenye huu nimejikita sana kumnukuu Nyerere.

Msome vizuri Mohamed Said ukimsoma kwa chuki hauwezi kumuelewa.
Niambie kama kuna Uzuzi nimefanya katika maandishi niliyowanukuu. Sikuongeza au kupunguza!

Nimeeleza ulichokisema na alichokisema Mohamed, kilichoonekana ni 'Jarhu friendly'

teh teh
 
Niambie kama kuna Uzuzi nimefanya katika maandishi niliyowanukuu. Sikuongeza au kupunguza!

Nimeeleza ulichokisema na alichokisema Mohamed, kilichoonekana ni 'Jarhu friendly'

teh teh
Teh teh teh! Nikuambie nini tena wakati mie nasomesha hapa, narudia tena mie kwenye huu mnakasha wala situmii mipini yangu kabisa natumia Ulimbo wa maneno ya Nyerere, natakuwekea wala usihofu, wewe endelea kurusha ngumi hewani,teh teh teh.

Sijasema mie amesema Nyerere vuta subra takuwekea huo Ulimbo uhangaike nao.
 

Kwanza sioni jambo la maana kuendelea kujadiliana mambo ya jarhu wala muktadha lhali kwani sio hoja ya msingi. Kama bado msimamo wako kasengenywa haya ni twende na hoja iliyo mezani. Mtama wako tuliousubiri muda mrefu tumeshauona na tumeshaupatia majibu yake. Halafu nimekuona sehemu nyingi unaniita chamvinga badala ya chamviga sijui ni makusudi? Chamvinga katika lugha yetu inaleta maana nyingine.
 
Last edited by a moderator:
Mujitahid CHAMVIGA.

Hapana mtama wake bado haujaletwa humu alisema mpaka atokee mtu amchokonoe kama watu hawajakimbia jukwaa na kukunja jamvi teh teh teh.

Kesho tukijaliwa tutaanza kudadavu bayana za historia ya TANU ya Kivukoni.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…