Wickama
JF-Expert Member
- Mar 8, 2009
- 1,466
- 1,196
haya nimuachie mohamed said kwani mimi sikuwa more concerned na haya ila nimeeleza kuwa usengenyaji mnaosema mzee ms si kweli.
Ni kusengenya 100%. No doubt
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
haya nimuachie mohamed said kwani mimi sikuwa more concerned na haya ila nimeeleza kuwa usengenyaji mnaosema mzee ms si kweli.
Wanaukumbi, hapa chini tawawekea historia ya TANU kwa ufupi ambayo iliandikwa Chuo Cha Kivukoni baada ya kutwishwa jukumu hilo na Mwalimu Nyerere, halafu muangalie nafasi za wazee wa Dar es Saaam zipo wapi.
HISTORIA YA TANU
2.0 TANU NA HARAKATI ZA KUPIGANIA UHURU WA TANGANYIKA
2.1 TANU ilizaliwa katika mazingira yaliyoandaliwa na Tanganyika African Association (TAA):
TAA iliundwa 1948 kufuatia tukio la kutengana kwa African Association (AA) ya Tanganyika na Zanzibar. AA ilizaliwa Dar es Salaam 1927 chini ya uongozi wa Cecil Matola akiwa Rais na Kleist P. Sykes akiwa Katibu. Malengo ya AA yalikuwa ni kupigania haki, maslahi na umoja wa Waafrika. AA ilikuwa na matawi yake makuu Dodoma na Zanzibar. Aidha, AA ilifungua matawi katika miji iliyokuwa makao makuu ya wilaya.
Katiba ya TAA ilitamka wazi kwamba Chama hicho hakikuwa na malengo ya kisiasa. Mwaka 1953 yalifanyika mabadiliko ya uongozi katika TAA. Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alichaguliwa kuwa Rais wa TAA. Chini ya uongozi mpya, Katiba ya TAA ilionekana kwamba isingeweza kukidhi malengo ya kisiasa. Mwalimu alipewa jukumu la kuandaa Katiba mpya ya TAA ambayo ingezingatia malengo ya kisiasa. Baada ya uandaaji wa Katiba hiyo kukamilika, haja ya kubadili jina ilionekana dhahiri na majina mengi yalipendekezwa likiwemo la TANU. Nafasi ya TAA ilichukuliwa na TANU iliyozaliwa tarehe 7 Julai, 1954. TANU ilirithi matawi ya TAA, wanachama na viongozi wa TAA katika maeneo mengi.
Waasisi wa TANU ambao walihudhuria na kushiriki katika Mkutano wa kuzaliwa kwa TANU walikuwa 17:
- Mwalimu J.K. Nyerere – Rais wa TAA/TANU
- Geremano Pacha – Jimbo la Magharibi
- Joseph Kimalando – Jimbo la Kaskazini
- Japhet Kirilo – Jimbo la Kaskazini
- C.O. Milinga – Jimbo la Mashariki
- Abubakari llanga – Jimbo la Ziwa
- L.B. Makaranga – Jimbo la Ziwa
- Saadani A. Kandoro – Jimbo la Ziwa
- Suleman M. Kitwara – Jimbo la Ziwa
- Kisung'uta Gabara – Jimbo la Ziwa
- Tewa Said Tewa – Jimbo la Mashariki
- Dossa A. Aziz – Jimbo la Mashariki
- Abdu Sykes – Jimbo la Mashariki
- Patrick Kunambi – Jimbo la Mashariki
- Joseph K. Bantu – Jimbo la Mashariki
- Ally Sykes – Jimbo la Mashariki
- John Rupia – Jimbo la Mashariki
- TANU ilizaliwa baada ya Vita ya Pili ya Dunia:
Katika vita ya Pili ya Dunia (1939 – 1945), Watanganyika walishiriki wakiwa askari upande wa Waingereza. Katika kushiriki huko, baadhi yao walipigana vita nchi za nje, kwa mfano, India, Burma, Madagascar n.k. Wakiwa huko vitani walipata fursa ya kubadilishana mawazo ya kisiasa na askari wenzao waliokutana nao katika uwanja wa vita.
Baadhi ya askari hao wa Tanganyika waliporejea kutoka vitani walikuja na fikra mpya za ukombozi wa Mwafrika. Fikra hizi mpya zilioana na zile za Kituo cha Wasomi wa Kiafrika waliokuwa London. Kituo hicho kilijishughulisha sana na suala la ukombozi wa Mwafrika kupitia midahalo.
Katika miaka 1950, wakulima walikwishajiunga na kuanzisha vyama vya kuuza mazao yao ya biashara ili waweze kupata bei nzuri kwa kupunguza gharama ya mtu wa kati ambaye alikuwa ni mfanyabiashara wa Kiasia. Baadhi ya Vyama vya Ushirika vilivyokuwepo kabla ya TANU ni:-
- TANU ilizaliwa katika mazingira ya vyama vya ushirika:
Kwa kuwepo vyama vya ushirika, ujumbe wa TANU kuwafikia wananchi ulirahisishwa. Wanachama wa vyama vya ushirika walijiunga na TANU. Wanachama na viongozi wa vyama vya ushirika waliunga mkono TANU katika madai yake ya kudai uhuru. Baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika walichaguliwa kuwa viongozi wa TANU katika ngazi ya Taifa. Kwa mfano:-
- Kilimanjaro Co-operative Union Ltd (1933)
- Ngoni – Matengo Co-operative Union Ltd. (1936)
- Rungwe African Co-operative Union Ltd. (1949)
- Bukoba Co-operative Union Ltd. (1950)
- Lake Province Native Growers Association.
TANU nayo iliunga mkono vyama vya ushirika katika madai yake ya bei nzuri ya mazao yao na kuondoa ushuru wa kahawa uliokuwa unatozwa na Serikali Kuu. Aidha, TANU ilihimiza na kuwahamasisha wananchi kuanzisha na kuimarisha vyama vya ushirika. Kazi hii ya kuhimiza na kuhamasisha wananchi kujiunga na ushirika iliendelea kufanywa na TANU hata baada ya Tanganyika kupata uhuru wake.
- Ndugu Nsilo Swai
- Sir George Kahama
- Ndugu Jeremiah Kasambala
- Balozi Paul Bomani
- Ndugu John Mhavile.
Baada ya Uhuru, TANU iliuona ushirika kuwa ni chombo cha kuleta maendeleo hivyo wananchi walihimizwa kuanzisha ushirika katika maeneo ambayo hayakuwa na vyama vya ushirika. Hali hii inaendelea hadi hivi sasa ambapo katika mfumo wa uchumi wa Soko, CCM inauona ushirika kuwa ni chombo cha kumwezesha mwananchi kiuchumi katika kumiliki na kuendesha uchumi wa Taifa lake..
Itaendelea.
Ni kusengenya 100%. No doubt
mkuu ameshaweka wazi kila kitu. implication yake ni kushabikia wapenda kuvuruga amani nchini. nampa majibu kwasababu,nataka kuweka wazi anavyoeleweka kwa kupenda kushabikia vurugu.Teh teh teh teh!
Kijana 2013 umerudi na kale ka mchezo kako ka kupinga ngoma mwenyewe na kucheza mwenyewe!
Unapotaka kujua kitu basi wajibu wako ni kuuliza. Baas!
Sio unauliza halafu unatoa jibu mwenyewe! Na unaongezea maneno yako meeengi!
Sasa mwalimu unaemuuliza hayo maswali atakusaidia vipi!?
Haya ndio matatizo ya kukesha kwenye ngoma za michiriku! Unapiga na kucheza mwenyewe!
Teh teh teh teh!
Shariff Ritz,
Jumma Al Kareem!
Unajua mara kadhaa kuna baadhi ya watu/family huwa unazitaja,ambazo nami pia wanajuana na family yetu...ndipo ninapokhis mimi nawe pia lazim itakua tunafahamiana!? Duh! Kwi! Kwi! Kwi!
Labda Sheikh Mohamed Said kabla hajakupatia jawaba lake,nipa fursa nami nikwambie japo kiduchu.
Huyo Bwana Kitwana Luga ulomuulizia,nakhis ndo huyo huyo ambaye nami alikua pia akijuana mno na Mzee wangu.
Huyo Bwana mimi khabar zake nalizipata kupitia kwa Al Marhum Sheikh Qassim Bin Jumaa.
Kitwana Luga...Baba yake Mzazi ni Al marhum Bwana Abdallah Juma Luga alikua pia ni mfanyibiashara mwenye kujikimu na pia alikua na ardhi kubwa pale Tungi na Kibada/Kigamboni.
Enzi ya Wakoloni huyo Bwana Abdallah Juma Luga,pia alikua ni Akida wa kukusanya mapato/kodi kwenye maeneo yake. Nafikiri Wakoloni walipenda pia kutumia Wazee Wetu mashuhuri kuendeleza zile dhuluma zao!
Huyu Bwana pamoja na hayo,pia alikua ni rafikize wakubwa mno Shariff Abdallah Al Attas,John Rupia tangia utotoni...walipokua wakubwa Bwana Abdallah Juma Luga na Shariff Abdallah Al Attas wao walioa nyumba moja!
Kwa hiyo kwa upande mwingine nasikia yule Kitwana Luga,pia Shariff Abdallah Al Attas alikua ni Uncle yake...yaani amemuolea Mamiye mdogo.
Walikua wakicheza football enzi hizo pale Ferry/Magogoni...lakini tatizo enzi hizo vijana wengi walikua hataki/hawamkubali ati kucheza mpira na John Rupia maskini kutokana alikua mgeni hapo mjini/hawamjui na wengine wakidai sababu ya dini/Ukristo wake!?
Ndipo yule Bwana Abdallah Luga,kwa kuwa alikua pia na umbo kubwa,akaamrisha yakuwa lazim kila mtu amkubali John Rupia kucheza nae na kuanzia siku hiyo awe kama mwenzao/ndugu yao!
Mapenzi/hishma baina ya John Rupia,Shariff Abdallah Al Attas na Abdallah Juma Luga,yaliendelea kushamiri mno mpaka kwenye families zao,khasa watoto wao.
Ndo maana utaona yule Kitwana Luga nae alikua ni rafikize wa karibu mno,kina Paul Rupia na nduguye Mpuya Rupia...maana alicheza nao tangia wadogo.
Bwana Abdallah Juma Luga,alikua pia ni mmojawapo ya Waasisi wa mwanzo ya TAA na pia alikua kipenzi na sahib mkubwa wa karibu wa Bwana Aziz Bin Ali...baba yao kina IGP Hamza Aziz na Bwana Dossa Aziz.
Bakht mbaya huyo Bwana Abdallah Juma Luga alifariki miaka michache kabla ile TANU haijazaliwa...maziko yake inasemekana yalikua makubwa mno wakti/zama hizo na kuhudhuriwa na umma halaiki na takriban Wazee Wetu woote waliokua mashuhuri zama hizo.
Tukirejea kwa mwanae,huyo Kitwana Luga...yasemekana alisomea pale H.H The Agakhan High School aka Tambaza.
Baada ya hapo alipelekwa nje ya nchi kuendelea na masomo yake...yasemekana Egypt,Israel na Jarumani.
Sasa kumbuka pia huyo huyo, Kitwana Abdallah Luga ulomuulizia...Dada yake wa mwanzo kuzaliwa ndie Mamiye Sheikh Yahya Hussein,Dada yake wa mwisho ndo pia alokua Mke wa Alhaj Issa Mtambo Gonera...ambae pia baadae alikuja kuolewa na Alhaj Kitwana Kondo na kuzaa nae mtoto mmoja nafikiri!?
Wakti ule msafara wa Waislam ulioongozwa na Mufti Sheikh Hassan Bin Amir unafika pale Cairo,Balozi alikua Bwana Abdallah Suweid.
Kumbuka Bwana Abdallah Suweid alikua na mwanae akiitwa Dr. Suweid. Huyo Dr. Suweid baade ndie aliewahi kuwa Mume wa Fatma Ali Hassan Mwinyi!?
Kitwana Abdallah Juma Luga,Mola amrahamu...kabla ya kuondoka kwenda masomoni,tayari alikua ni askari wa Usalama wa Taifa.
Ndo maana hata wanafunzi wenzie wengi pale Cairo walishindwa kutambua kwanini alikua very close na watu wengi mno wa mataifa mbalimbali ghafla,na pia mara kadhaa akionekana na watu mashuhuri kutoka Tanganyika waliokuja kutembelea pale...kwa mfano Bwana Abdilwahid Sykes,Abdilrahman Babu na Abbas Sykes,Oscar Kambona na wengineo.
Yale maangamizi ya Nyerere dhidi ya ule msafara wa Mufti Sheikh Hassan Bin Amir na harakati za Waislam,yalikua yakijulikana na watu wachache mno mmojawapo ni Balozi Suweid Abdallah na Kitwana Luga...ambao woote hawakupendezwa asilan na unyama ule wa Nyerere.
Kitwana Luga,ndie mtu wa mwanzo kuwastua na kuwapa khabar Waislam kuhusu ule msafara/harakati yakuwa wawe waangalifu,maana kuna "nguvu za kiza" zinawatazama kwenye hizo nchi zoote watakazopitia.
Zaidi ya hapo Kitwana Abdallah Luga,akatuma telegrams Zanzibar kwa Sheikh Abdallah Saleh Farsy...ambae nae alikua akimjua Kitwana Abdallah Luga kupitia kwa Sheikh Hussein Juma wa UTP.
Pia Kitwana Abdallah Luga,alituma Telegram nyingine kwa Uncle wake Shariff Abdallah Al Attas....ambae nae kutokana na influence na connections zake kwenye harakati za siasa wakti ule, khabar zikawafikia watu fulani muhimu,akiwemo Bwana Ali Sykes,Abdilwahid Sykes na Viongozi,Wazee Wetu/Masheikh zetu wengine waliokua vinara wa zile jumuia za Waislam.
Wakti Kitwana Luga aliporejea Tanganyika pia alifanikiwa kurejea na baadhi ya nyaraka muhimu kutoka pale Embassy Cairo na kuthibitisha kwa Wazee Wetu ile mipango/maangamizi yoote ya Nyerere dhidi yao!
Khabar inasemekana zilianza ku-leak kiduchu...maana Nyerere alikhis yakuwa Wazee Wetu,wanaanza kuwa "wajanja",kila mitego aliokua akiwawekea walikua hawanasi tena!? Kwi! Kwi! Kwi!
Ndipo Nyerere akaamuru Balozi Suweid aondolewe pale Cairo na kumweka Salim Ahmed Salim...na post ile ile ya Cairo pia iliwahi kuchukuliwa na Alhaj Ali Mwinyi.
Kitwana Luga baada ya kurejea Tanzania,alipelekwa post yake ya mwanzo kule Mbamba Bay....ati kupigana na makaburu wa South Afrika!? Kwi! Kwi! Kwi!
Bwana Ramadhan Aziz,aliekua nduguye IGP Hamza Aziz....alioa kwa Sheikh Hussein Juma wa UTP.
Nafikiri mpaka hapo bado tuko pamoja na bado unaifuatilia hiyo social/family network,Shariff Ritz!? Kwi! Kwi! Kwi!
IGP Hamza Aziz,akaamuru Kitwana Luga aletwe police kama kule Usalama wa Taifa ati Nyerere "hamuamini" tena...lakini nafikri Nyerere tayari alishabonyezwa yakuwa wale watu walikua na family connection fulani!?
Ndipo akarejea tena Police...lakini Nyerere aliposikia hizo khabar,akaamrisha Kitwana Luga apelekwe TAZAMA Pipelines,kuwa Director of Security Operations!? Kwi! Kwi! Kwi!
Yaani kilitengenezwa Cheo makhusus ili yule Bwana awepo mbali na files za Serikali tu! Kwi! Kwi! Kwi!
Baada ya IGP Hamza Aziz kuondoka madarakani,mara Nyerere akamchongea Kitwana Luga kesi ya kinafiki...iliyokhusu corruption kubwa na kuhusisha wale Al Abry family wa Iringa. Kulikua hakuna ushahidi wowote,hiyo kesi ilitupwa na Kitwana Luga akarejeshwa Usalama HQ na kuwa Desk Officer tu!
Mara za mwisho tulikutana nae kitambo Kilimanjaro Hotel nikiwa na Mzee wangu...inasemekana rafikiye mkubwa Salim Ahmed Salim alipokuwa Prime Minister ndo alompatia post "pahala fulani".
Huyu jamaa alikua na network kali mno...yaani alikua karibu mno na vijana/watoto wenzie woote wa mjini na pia Wazee Wetu.
Alikua ni mtu maarufu na mwenye marafiki wengi,lakini pia alikua karibu mno na both Wolter/Harith Mwapachus,Mwandoro,Hassan Diria,Kitwana Kondo,Alhaj Ali Mwinyi,Salum Hiriz,both Ali/Abass Sykes,Mbwana Bakari,Ibun Bin Saleh family,Mzee Salum Shamte,Mzee Mangara Tabu,Shariff Abdilkadir Juneid,Colonel Dr. Keis Mtambo,Sheikh Aboud Maalim,Brigadier Yusuf Himid,Lawrence Gama,Abdallah Fadhil Batenga,Zakaria maftah,Prof. Idris Mtulia,Prof Kigongo Fimbo Mnyonge,Prof. Mmari,Prof.Kaisi na wengineo wengi mno.
Nakumbuka tulihudhuria msiba/maziko yake na Mzee wangu...yaani palikua na watu/jamaa wengi mno...na rafikiye kipenzi maskini Dr. Salim Ahmed Salim alikuwepo pale akitokea Addis Ababa OAU,siku hiyo nilimuona pia Al Marhum Bwana Ali Sykes na wengineo lukuki.
Huyu Bwana alifariki akiwa labda si mkubwa asilan.
Miaka kadhaa ilopita nilikua pale Stavangar/Norway,nilikutana na mmojawapo ya watoto wa kike wa Bwana Kitwana Luga, alikua pale akisoma/anaishi....lakini nimepoteza contact nae,Wallahi!?
Tafadhali,tusasambure au kurekebisha kwa pamoja,mie nimeweka kiduchu tu kwa niyajuayo...ili kumkumbuka mmojawapo wa hawa ma-unsung hero wetu mwingine sisi Waislam.
Ahsanta.
Ni kusengenya 100%. No doubt
mkuu ameshaweka wazi kila kitu. implication yake ni kushabikia wapenda kuvuruga amani nchini. nampa majibu kwasababu,nataka kuweka wazi anavyoeleweka kwa kupenda kushabikia vurugu.
mkuu tanzaniaa tumeshuhudia makanisa yakichomwa moto, mchungaji akiuwawa na waislamu kule kanda ya ziwa, mapadre wakimwagiwa tindikali, shek arusha akilipuliwa na bomu, na mabinti wa uingereza wakimwagiwa tindikali, shekh ulanga akiagiza watu wauane kule mombasa kenyea. mkuu kutokana na hayo ningeomba unipe tofauti ya shetani na mungu kwa matendo yao.
Hapo ki lugha yaani kiarabu pana mambo takriiban matatu au manne yanataka kufanana lakini ni tofauti, nami ntakusaidia hiyo uloandika hapo, lakini mambo yenyewe ni :- 1-FITNA
2-KUSENGENYA
3-HUSUDA,
Sasa ama KUSENGENYA ni kumsema nduguyo kwa yale yanayomchukiza, na kama hayo umsemayo akiwa hanayo basi utahesabika UMEZUA, na hapo sasa kwa wenye fani ama ilimu ya Sharia wanajua nini hukumu ya MZUZI,
Pia hapo pana namna nyengine, si kila kumsema nduguyo inakuwa umezua la, inatizamwa na kitu waita wao
MUQTADHAL HAALI, kwani bila hivyo itakuwa hairuhusiwi hata kufanya masimlizi ya mtu/watu kwani yote tungeliyasema ni UZUZI,
Sasa sijajua Wickama ulilenga nini ama hiyo tafsiri ndiyo umetembea nayo katika hoja yako?
Nadhani nimejaribu kuweka bayana, lakini naamini wengi humu wamebobea, hivyo nataraji marekebisha nilipopunguza ama kuongeza.
Hapa 2013 hata mie sijakuelewa vizuri ina maana Sheikh Illunga ndo alitoa amri Sheikh mwenzake apigwe bomu huko Arusha ama umechanganya mambo kidogo as a human being? Na nadhani pia pana Sheikh hukohuko Arusha alimwagiwa Tindikali, sasa hebu niweke sawa ndugu yangu ili hii safari twende nayo vizuri mmoja wetu akabaki porini, vingenevyo hiyo kauli yako ndo itakuwa imezaa maana ya neno UCHOCHEZI.
mkuu tukiachana na zile Cult zenye kumpa msaada mungu kuua binadamu wengine ambao inadaiwa mungu yule aliwaumba mwenyewe, ikafikia wakati yeye mungu hawezi tena kuwaua hivyo anakula njama na binadamu ili wamsaidie kuua binadam wenzao.pengine bnadamu wale wanaakili sana na wameshaijua janja ya mungu yule hivyo so rahisi yeye kuwatawala tena.
As a human being, ni kuwa kama utashindwa kutenganisha kati ya shetwain na mungu kwa matendo waweza jikuta ni agent wa shetani bila kujua. mkuu kiimani kuna gap kubwa kati ya mungu na shetani. ikiwa na maana moja ni hasi zaidi wakati jingine ni chanya zaidi. hivyo framework hii ya hasi na chanya inakupa urahisi kujua matendo yaliyo hasi yanamwakilisha nani?. ukichukulia hali halisi ya nchi zetu. hapa nahop ntakuwa nimeeleweka zaidi.
naomba mkuu usichanganye hasi na chanya iliyopo kwenye betri na redio na kwenye masomo ya kemia na fiziksi. ha ha ha ha
Wabara,
Mie Sheikh wangu ''Riadh Salhin'' lakini nimeiogopa hata kutalii kwa
kuwa nilikuwa na hakika hapa jamvini wapo wajuzi.
Ahsante sana Allah akuzidishie.
Nimefyonza ilm kama Spike Lee anavyopenda kusema.
Ritz;7638832]Hakuna makosa kusema waliopigania walikuwa wazee wazalendo wa Kiislam, ambao walikuwa na mapenzi na Nyerere kama kijana wao wala hawakumbagua
[TABLE="width: 660"]
[TR]
[TD]Mohamed Said: There were no problems of personality clashes at the headquarters apart from a small faction of radical Muslims who were plotting to oust Nyerere from Party leadership for being a Christian.
This was the second time the issue of religion had cropped up since Nyerere assumed leadership of the movement for the first time in 1953.
A meeting was called to clarify the status of Christianity in TANU and to establish a nationalist-secularist ideology as a way of preserving national unity.
This meeting coined the name ‘Yuda' which was to be the label of any member of TANU who discriminated his fellow African because of his faith
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]
Haya maneno siyo yangu ni maneno ya Nyerere takuwekea bahati nzuri mie kwenye huu mnakasha nimejikita sana kumnukuu Nyerere, mwenyewe kama reference.Sijui hili tusema ni uzuzi, muktadhal haal au Jarhu wata'adir.
Ritz anasema hakukuwa na ubaguzi, Mohamed anasema ulikuwepo. Hapo lazima kuna uzuzi kwa mmoja wenu
Ritz anasema walikuwa wazee wazalendo wa kiislam, wazee wanasema hapana hakuna kubaguana! hii ni muktahal haal
Wakati Ritz anasema hayo Mohamed anampinga lakini kwa kutumia Jarhu wata'adir
Nipo pembeni natazama watu wanaongea na kujibiziana wenyewe! wazungu wanasema 'Friendly fire''
cc chamvinga, Wickama
Niambie kama kuna Uzuzi nimefanya katika maandishi niliyowanukuu. Sikuongeza au kupunguza!Haya maneno siyo yangu ni maneno ya Nyerere takuwekea bahati nzuri mie kwenye huu nimejikita sana kumnukuu Nyerere.
Msome vizuri Mohamed Said ukimsoma kwa chuki hauwezi kumuelewa.
Teh teh teh! Nikuambie nini tena wakati mie nasomesha hapa, narudia tena mie kwenye huu mnakasha wala situmii mipini yangu kabisa natumia Ulimbo wa maneno ya Nyerere, natakuwekea wala usihofu, wewe endelea kurusha ngumi hewani,teh teh teh.Niambie kama kuna Uzuzi nimefanya katika maandishi niliyowanukuu. Sikuongeza au kupunguza!
Nimeeleza ulichokisema na alichokisema Mohamed, kilichoonekana ni 'Jarhu friendly'
teh teh
Sijui hili tusema ni uzuzi, muktadhal haal au Jarhu wata'adir.
Ritz anasema hakukuwa na ubaguzi, Mohamed anasema ulikuwepo. Hapo lazima kuna uzuzi kwa mmoja wenu
Ritz anasema walikuwa wazee wazalendo wa kiislam, wazee wanasema hapana hakuna kubaguana! hii ni muktahal haal
Wakati Ritz anasema hayo Mohamed anampinga lakini kwa kutumia Jarhu wata'adir
Nipo pembeni natazama watu wanaongea na kujibiziana wenyewe! wazungu wanasema 'Friendly fire''
cc chamvinga, Wickama
Mujitahid CHAMVIGA.Kwanza sioni jambo la maana kuendelea kujadiliana mambo ya jarhu wala muktadha lhali kwani sio hoja ya msingi. Kama bado msimamo wako kasengenywa haya ni twende na hoja iliyo mezani. Mtama wako tuliousubiri muda mrefu tumeshauona na tumeshaupatia majibu yake. Halafu nimekuona sehemu nyingi unaniita chamvinga badala ya chamviga sijui ni makusudi? Chamvinga katika lugha yetu inaleta maana nyingine.