Mohamed Said.
Naomba utujuze kiduchu kuhusu historia ya TANU waasisi wake kuna vitu vinanichanganya, historia ya Kivukoni inasema TANU imeundwa na watu 17 tu.
Kuna hawa wazee ambao walikuwa wanaunda baraza la wazee wa TANU chini ya mwenyetiki Sheikh Suleiman Takadir, hawamo kwenye kitabu cha Kivukoni.
Idd Faiz Mafongo, Abasi Mtemvu, Idd Tosir, Ally Mwinyi, na wengine ambao unaweza kututajia ambao walikuwa wanachama wa mwanzo wa TANU wote hao wametoswa na historia ya Kivukoni, wamewekwa kina Japhet Kirilo.
Hebu tupe darsa kwenye hili.
Shariff Ritz,
Ni kweli waasisi wa TANU ni 17 na hawa wametoka katika majimbo ya Tanganyika.
Hebu soma hii kwa kuanzia:
It was under this political atmosphere that the seventeen TAA delegates from the
branches in the provinces and headquarters met in Dar es Salaam from 7 th July,
1954, to deliberate on a new constitution for a new political party-TANU.
The Eastern Province which had a majority of delegates was represented by Abdulwahid
and Ally Sykes, Dossa Aziz, Tewa Said Tewa, Patrick Kunambi, Kasella Bantu, John Rupia,
Julius Nyerere and C.O. Millinga; Western Province was represented by Germano Pacha;
Northern Province by Joseph Kimalando and Japhet Kirilo; Lake Province represented by
Abubakar Ilanga, L.M. Bugohe, Saadan Abdu Kandoro, S.M. Kitwana and L.M. Makaranga.
Of the seventeen founding members, nine of them came from the headquarters, four from
Lake Province, one from Western Province and two from Northern Province.
This distribution of delegates gives a picture of the pattern of political activity in Tanganyika
before the formation of TANU.
Shariff,
Hao hapo juu ni waasisi wa TANU kama tunavyoelezwa lakini kwa kweli katika hao kila mmoja
ana mchango wake na si kuwa kwa kuwa wao wamehudhuria mkutano ule wa TAA 1954 basi
wao ndiyo walikuwa vinara wa harakati.
La hasha.
Nakupa mfano mmoja.
Hamza Mwapachu hayuko katika orodha ya waasisi.
Ali Migeyo hayupo katika orodha ya waasisi.
Dr. Michael Lugazia hayupo katika orodha ya waasisi.
Abbas Sykes hayupo katika orodha ya waasisi.
Na ukipenda wale madaktari wa TAA - Dk. Kyaruzi, Joseph Mutahangarwa, Dk. Mwanjisi, Dk. Tsere
wanaweza kutiwa katika orodha ya waasisi.
Lakini kuna ile TAA Political Subcommittee ya 1950 ya Sheikh Hassan bin Amir, Hamza Mwapachu,
Abdulwahid Sykes, Steven Mhando, Said Chaurembo na John Rupia.
Hawa wote walikuwa katika mchakato wa kuasisi TANU.
Lakini zaidi la kuzingatia ni kuwa juu ya hawa wote kulikuwa na kamati ya ndani zaidi ya TANU hii
walikuwa Abdulwahid Sykes, Ally Sykes, Hamza Mwapachu, Dossa Aziz, Julius Nyerere na John Rupia.
Sasa ukipenda unaweza ukawatia wale Wakenya watatu Dome Okochi Budohi, Patrick Aoko na C.
Ongalo.
hawa walikuwa katika halmashauri kuu ya TAA iliyoingia katika uongozi na Nyerere mwaka 1953.
Unaweza ukarudi nyuma zaidi na kuangalia wazee waliotoa maoni yao mbele ya Kamati ya Udhamini ya Umoja
wa Mataifa mwaka 1954 msemaji mkuu akiwa Said Chamwenyewe na wanakamati mmoja wao akiwa Sheikh
Suleima Takadir na Mohamed Jumbe Tambaza.
Haishangazi kuwa wazee hawa mara baada ya TANU kuundwa wakaunda kamati ya Wazee wa TANU mwenyekiti
akiwa Sheikh Suleiman Takadir.
Kwa mukhtasari hii ndiyo historia ya waasisi wa TANU na wote hao niliowataja hapo juu wote walikuwa wanajua
kwa miaka mingi kuwa TANU ilikuwa iko njiani inakuja.
Huenda waandishi wa Kivukoni haya hawakuwa wanayajua kwa hiyo hatuwezi kuwalaumu kwa kutoyaandika katika
historia yao.
Juu ya hayo ikiwa wanahistoria hadi sasa hawatanyanyua mguu kujitoa katika msimamo wa kumwangalia Nyerere
peke yake kama ndiye pekee alipigania uhuru wa Tanganyika daima watabaki katika giza na mengi yatawapita.
Mimi nimeyajua kwa kuwa hao waasisi wenyewe ndiyo wazee wangu na wengine nimewadiriki kuwaona na kuzungumza
nao.
Waasisi wa TANU ni wale 17 kwa sababu ule ulikuwa mkutano wa wajumbe maalum kutoka majimboni usingeweza
kuhudhuriwa na kila mtu.