Naona hapa kuna maRPC,SACP,Colonel,General Manager,Principal Secretary,Chief Engineer,maBusinesswomen,MaBrigeder,maDr wakubwa na wengine chief medical officer wa Nyerere ..........unazidi kufuta ile dhana ya Sheikh Mohamed awamu ya Nyerere kulikuwa ba ubaguzi wa kidini.Asante gombesugu unazidi kumvua nguo hadharani mzee wako wa gerezani.
Brigadier Ngongo,
Hili suala nafikiri ulishawahi kuulizia kitambo kwenye ule mnakasha ulopita/ulofungwa,nami nalikupa majawaba mema tu!?
Kwa kifupi,hao woote uwaonao hapo/nilowataja,kumbuka yakuwa Family/Wazazi Wao walikua ndo watu mashuhuri na wenye kujikimu kwa zama hizo hapo Mzizima/D'salaam.
Na Wazee Wetu hao hao kwa njia moja ama nyingine ndo pia waliokua wanaharakati vinara na pia waasisi wa zile TAA na TANU yake...na hata yule Nyerere akiwajua mno na kuwastahi kiduchu.
Nafikiri la kujiuliza ni,vipi kuhusu wale maelfu ya Waislam wengine maskini na waliokua nje ya uwezo na kusahauliwa/kuadhibiwa na wanaendelea kuadhibiwa na legacy ya yule Nyerere mpaka kesho!?
Unajua huko mikoani/mabara, nako pia kuna ndugu zetu wengi mno wa Kiislam na Masheikh wetu/Wazee Wetu wakubwa ambao nao pia walikua wakiadhibiwa silently na yule Nyerere.
Hawa Wazee Wetu wengi mno,khasa wanaotajwa mara kwa mara humu JF, ni bakhti yao tu yakuwa wengi wao ni wenyeji wa hapo Mzizima/wenye mji wao,au walikuwapo hapo Mzizima/D'salaam kipindi kile cha zile harakati,ndo pia waliokua mashuhuri/maarufu wakti huo....
Pamoja na hao unaodai nilowataja wakiwa na Ilm na vyeo vikubwa wakti huo wa Nyerere...pia unadai ati yakuwa hiyo inaashiria Nyerere hakuwa mbaguzi na kipindi chake kilikua ati ni chema kwa Waislamu!? Kwi! Kwi! Kwi!
Embu jiulize kiduchu,wakti wa Nyerere kulikua na Waislam wangapi ndo Head of Departments pale UDSM/Mlimani!?
Kulikua na Waislamu wangapi waliokua ni ma-Colonel au ma-Brigadier!?
Kulikua na Waislam wangapi kwenye Police wakti huo waliofikia au hata kunusa vyeo vya SSP au SACP kulinganisha na wenzao Wakristo!?
Kulikua ni Waislamu wangapi waliokua ni Wakuu/Makamanda wa Vikosi vya ulinzi na Usalama hapo nchini!?
Kulikua na ma-Chief Engineer wangapi Waislam kwenye Idara nyeti au nyinginezo za Serikali!?
Na hizo statistics niuliziazo, ni ya kwamba hata ukichanganya na wale Waislamu/Wanataaluma wa kutoka Zanzibar,ambao mara nyingi walikua wakitumika kama ni buffer zone tu na Nyerere,ili kuziba yale malalamiko ya ndugu zao Waislamu wa Tanganyika.
Kwa kifupi,hapa tuangalie huo mlingano/ratio wakti huo ya nafasi walizokua nazo hao Waislam wasomi ukilinganisha na wenzao Wakristo!?
Nakusihi Mkuu,kipata fursa nenda pale Immigration HQ,ukatuletee takwimu,uwiano/ratio ya nafasi zoote za uongozi au hata nafasi za kawaida baina ya Waislam na wenzao Wakristo....nasi tuhapa jamvini twakusubiria!? Kwi! Kwi! Kwi!
Chembilecho cha Maulana Dr Kahtaan;yakuwa tatizo ni huo MfumoKristo.
Kipata fursa pia nakusihi...rejea/pitia posts zoote humu jamvini.
Nimefurahika tumezungumza japo kiduchu.
Ahsanta.