Islam’s role in Tanzania’s freedom struggle

Swali ni hili Waislam hawana shida ya kupewa majina ya barabara.
 
Swali ni hili Waislam hawana shida ya kupewa majina ya barabara.
Mohamed Said kasema mitaa inabadilishwa majina na kuitwa Yusuph Makamba. Mtaa wa Kiyate nao ulikuwa hati hati.

Yeye ndiye anaandika historia na mumekuwa mnasema bayana zake kama ulimbo, sasa kwanini mkatae kuwa hakuna madai ya barabara? Kwani kuna ubaya tukiwaenzi wazee kwa majina ya bara bara. Mbona kuna Shekilango, Azikiwe n.k. leo kuna tatizo gani tukisema wazee wapewe majina. Nini kinakuchonyota kiasi cha kuona hiyo ni dhalili.

FYI, Sheikh Takdir alipingana na K.Sykes na A.Sykes. Hapo ndipo tunasema historia ikiandikwa kwa macho ya makengeza lipo tatizo. Itauuundwa!! hatimaye itajisahihisha. Sasa hivi inazidi kujisahihisha.
 

Nguruvi,
Hapa sijakuuelewa khasa unakusudia nini.

Nitajitahidi kueleza mawazo yangu.

Kuhusu kuzipa barabara majina ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika
binafsi sina tatizo la hilo.

Kuhusu ''kuundwa'' kwa historia mie nimejitahidi kueleza kama akili yangu ilivyojaalia.

Lakini kubwa kitabu changu ndicho kilichopambana na hao ''waundaji'' wa historia wa
Kivukoni na nimo humu kueleza historia ya kweli.

Kuhusu Sheikh Takadir.

Sheikh Takadir alipingwa na kila mtu ukiwatoa watu wachache sana mmojawapo
aliyemuunga mkono alikuwa Ramadhani Mashado Plantan.
 

Siku ukiweza kuubadili Uislaam ndio siku unaweza kuwabadili Waislaam waliopita, wa sasa na wajao. Na nnakuahidi hautoweza.

Kuna ambae anaweza kuubadili ukweli kwa uongo? Huyo anajidanganya nafsi yake tu.

Hivi nikuulize, kinawauma nini haswa mnapoisoma historia ya Waislaam wa Tanganyika? Au ndio Islamophobia? Kila msikiapo Uislaam, Waislaam nyie huwaingia hofu ya ajabu na hamuishi kutapatapa.

Ngoja nikupe dersa dogo, ikiwa wewe unaamini kuwa Uislaam au Muislaam ni adui yako, basi nakuasa msome vizuri adui yako ndiyo utakapomuelewa vizuri na hata ukimshambulia itakuwa rahisi kwako kupambana nae, kwa nini huanzii kwa kusoma na kuuelewa Uislaam ili umjuwe vizuri "adui" yako?
 

Nguruvi,
Haya majeshi ya Wazulu, Wanubi na Wamanyema walioingia Tanganyika kuupa nguvu
ukoloni mimi binafsi siwaoni kama ni watu dhalimu.

Hapa nchini tunao ''Kavirondo'' kama wazee wetu walivyopenda kuwaita.

Hawa walikuwa askari katika jeshi la Muingereza waliokuwa wakitumika dhidi ya Waafrika
wenzao.

Ikiwa Wanubi, Wazulu na Wamanyema waliotumika katika jeshi la Wissman ni madhalim basi
ndugu zetu waliokuwa katika jeshi la kikoloni na wao ni madhalim pia.

Mimi nawaona hawa kama tatizo la ukoloni.

Wazee wetu wakiwabeba Wazungu kwenye machela wakipatanao katikati ya mapori na wangetaka
wangeweza wakawaua huko.

Hili hawakulifanya.
Sasa hawa wazee wetu tuwaitaje?

Wasaliti?
 
Wickama,

Jitahidi kusoma neno kwa neno ili upate maana!

Ukipata maana, fanya tafakuri jadidi, ni nani alokusudiwa!
Upembuzi wa jambo kabla ya kuwasilisha penye wengi, ni kitu kizuri, umuepusha mtu na aibu!

Ahsante!



Tayeb;

Ipo hadith ya mama Aisha (ra) kugombezwa na mtume (saw) kuhusu kumsema mgeni wao mmoja kuwa ni MFUPI akakaripiwa kuwa KASENGENYA. Tena yeye aliashiria tuuuuuu. Sasa linganisha na hii ya huyu nduguyo kutaja kuwa fulani NDIYE alikuwa anamlisha JKN kuwa ndio jeraha adilifu lakini sigara itapitiliza. Wakati watoa malisho na vyakula na malazi walikaa kimya. Na sheria iko wazi kuwa kama mfanya aibu au kosa alijificha basi alijua aibu yake na hupaswi kubomoka ubinafsi wake kama huu wa MS. Na huyu wala sio mrithi wa hao waathirika ni msimuliwaji tuu. Yaani sio katika wanaoruhusiwa na sharia kumfanyia kisasi JKN assuming aliua ndugu zake (awataje tupime na kuona kuwa yeye ni mrithi halali ambaye angeruhusiwa kisasi). Wala wakati anaandika tuhuma zake hakumwonyesha wala kumuuliza mtuhumiwa kabla hajazichapisha mbele ya hadhara yaani kufanya uadilifu. Uwe na ujasiri wa kuita MKATE kwa jina lake halisi. Tena kwa wasio waislamu inatakiwa kuwafanyia uadilifu wa juu zaidi na yapo maandishi yanayotaka na kusisitiza hivyo. Sio lazima uwe graduate wa Al-azhar. Nduguyo usisite kumshauri baada ya kumpa LIKE kuwa afanye toba iliyotakasika. Zipo aya kibao zinazoonya kuwa kuwachukia watu KUSIPELEKEENI KWENYE KUWADHULUMU AU KUTOWATENDEA UADILIFU.

Mwisho nakuuliza; huyo aliyeMRUDI mama Aisha (ra) unadhani angem-SUPPORT huyu bwana kwa haya ya vitoweo vya JKN?
 
Last edited by a moderator:
Wickama unatoa hadithi ya nabii s.a.w inayosema kumsengenya nduguyo ni kama kula nyama yake!!

Nakakuuliza Nyerere ndugu yetu!?

Halafu hapa hakuna anaesengenywa hata kidogo!

Hapa kinachoongelewa ni historia.

Na kama kila kipande cha historia kinachohusu watu tofauti kinaitwa KUSENGENYA! basi hadithi zote zinazo elezea unafiki wa kina abujahal na wenzake ni KUSENGENYA!

Na zile zinazosema kuwa kuna baadhi ya maswahaba waliwakomboa watumwa kwa kuwanunua kwa pesa kadhaa, pia NI KUSENGENYA!

Na kusema mfanya biashara fulani kila ikifika ramadhani basi huwasaidia maskini wa mtaa fulani hela ya kula!
Kwa tafsiri yako PIA NI KUSENGENYA!

Tafadhali jaribu kusoma na kufahamu nini maana ya KUSENGENYA KWANZA!
Kabla ya kuja hapa kusema kuwa kule kusaidiwa kwa yule Adui wa haki chakula na sigara na tumbaku ni KUMSENGENYA!

Mafundisho yanatwambia;- ziko sadaka za aina mbili, ya siri na ya dhahiri!
NA ZOTE NI NZURI!
Ispokuwa ya siri ina daraja kidogo zaidi lkn haina maana ya dhahiri haifai!

Sasa kama yule Nyerere alisaidiwa na watu wakasema kwenye kuiweka sawa historia! Hio kwa msomi yyt wa dini atakwambia SIO KUSENGENYA!

NA kwa sababu umetumia hadithi kuwonya watu!
Na mimi nakukumbusha kuwa;-

Mtume wa Mungu s.a.w.anasema" mwenye kuji shabihisha na watu wa tabaka fulani. Basi na yeye ni mmoja wapo!
(Bukhari na muslim).

Sasa hao unaokaa nao na kutumia hekima zako kuwapambia na kujaribu kuficha uovu wao. Basi na wewe ni ktk wao!

Ahsanta.
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi,Kuhusu Sheikh Takadir.

Sheikh Takadir alipingwa na kila mtu ukiwatoa watu wachache sana mmojawapo
aliyemuunga mkono alikuwa Ramadhani Mashado Plantan.
Ahsante, very candid!! Nashukuru sana umenielewa vema na kwakweli sina uchoyo wa fadhila umelisema kwa ukweli.

Nitakapotofautiana nawe ni pale 'statement' ya Takdir inapohusishwa na mzee John Ketto.
Kwavile umeeleza kuwa Takdir hakukubalika kutokana na misimamo yake basi hata kauli zake na tuhuma zake kwa Ketto hazikuwa na maana kabisa.
Hilo linamwacha Ketto kama mpigania uhuru bila kujali imani yake.
 

Wickama,
Naziona jitihada zako.

Utapata shida sana kwa hiyo njia ulochukua.
Haiwezi kuwa nyepesi hivyo.
 

Nguruvi,
Kwa wakati ule mwaka 1958 Sheikh Suleiman Takadir hakueleweka.

Yeye alikuwa anawaambia Waislam kuwa vipi uhuru unakuja na Nyerere anapachika
Wakristo wenzake kwenye nafasi za uongozi?

Ukitaka kupata hili lazima sasa urudi kwenye Kura Tatu na ujue kwa nini TANU ilitaka
kugoma kushiriki.

Leo Sheikh Takadir ni shujaa katika macho ya Waislam na ndiyo hili joto tunalohisi sasa.
Nimeeleza hapa huko nyuma kuwa Nyerere heshima yake mbele ya Waislam iko chini.

Sasa tujiulize kwa nini imekuwa hivyo?
 

Nguruvi3.

Mitaa kupewa majina ya wazee wetu na wazee wako kina John Ketto siyo issue.

Jambo kubwa na endelevu ambalo litawaenzi hawa wazee wetu waliofutwa na historia ni kuwaandika kwenye vitabu.

Nakushauri hata wewe aundike kitabu kuwaenzi wazee wako kina John Ketto walivyokuwa kwenye harakati za uhuru.
 
Last edited by a moderator:
Hapana si kweli ni kwa baadhi ya waislam. Katika hao baadhi wengi wao ufahamu ni mdogo, ukiwauliza kwanini wanamchukia Nyerere hawana sababu bali kuishia kusema ni mbaya.
Wengi wamefundishwa chuki kitu kibaya sana.

Wameaminishwa tu but they don't have ground to stand.
Fanya research kidogo uone uelewa wa baadhi ya viongozi, wakalishe kitako, hazipiti dk 10 hawana jibu. Watakachosema tumeshikia, inasemwa au tumeambiwa.Hili litaonekana kama dharau lakini ni ukweli.


Kikundi kidogo kimejivika joho la waislam na hiki kinaendeleza chuki za akina Takdir.
Takdir hakuwa na la maana wakati ule na hadi leo. Huo ndio ukweli hata kama unakataliwa.

Nchi hii ni yetu sote na wala hakukuwa na uwezekano wa uhuru wa dini moja,hakuna kitu kama hicho. Na hata sasa nchi ni yetu sote na hilo litabaki hivyo
 

Nguruvi,
Hali ya nchi yetu ni mbaya.

Nafasi ya Kanisa katika kuendesha nchi sasa ni wazi na si siri tena.
Prof. Hamza Njozi alieleza tatizo hili katika kitabu chake ''Mwembecha Killings...''

Ukweli ndani ya kitabu ulitisha serikali.
Kitabu kikapigwa marufuku.

John Sivalon na yeye kaandika kitabu kuhusu nafasi ya Kanisa katika siasa za
Tanzania.

Mohamed Said akaja na historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika na mwisho wa
kitabu kaandika kuhusu njama dhidi ya Uislam.

Waislam wa kizazi kipya sasa wanajiuliza mengi.

Kubinywa kwa Waislam leo kuko wazi hata kama tunaogopa kulizungumza hili na
serikali inajifanya yote ni shwari.

Ukweli ni kuwa hali si shwari.

Baadhi ya marafiki wa Tanzania kwa pembeni wametoa ushauri kwa serikali
kutolifumbia macho tatizo hili.

Sisi si kikundi kidogo tuna umma mkubwa wa Waislam na ukitaka kupima nguvu
yetu angalia tulipowaambia Waislam wakatae kujiandikisha hadi kipengele cha
dini kimewekwa.

Zoezi halikufanikiwa.

Angalia ukipenda mfano mdogo tu.
Sikiliza mijadala humu JF.

Tunalo tatizo na halitoondoka kwa kutaka tu liondoke.
Tatizo litaondoka kwa kuukubali ukweli na kuzungumza bayana kuondoa dhulma.
 
Wickama.

Bi Aisha hana sifa hiyo usitake kumchafua kwa upuuzi wako, Bi Aisha alikuwa mwanamke mwadilifu sana Bi Aisha katajwa kuwa ndiye mwanamke bora duniani.

Weka hiyo hadith yako, imepokelewa na nani. usipende kuokota maneno mitaani na kuyaleta JF haswa maswala ya Uislam.

Tunasubiri hiyo hadithi yako.
 
Last edited by a moderator:
Teh teh teh! Eti baadhi ya Waislam halafu hao Waislam upeo wao ni mdogo.

Nadhani hapa unawaongelea Bakwata.

Nguruvi3 ukitaka kupima Waislam wanamchukuliaje Nyerere, fanya utafiti wako pita Misikitini tu halafu msifie uone kitakachokutokea.

Lakini pita katika Misikiti michache ya Bakwata Nyerere huko ni shujaa.

Nakupa mfano mdogo kama una akili pima.

Sheikh Mkuu wa BAKWATA alitangaza kuwa anawataka Waislam wote wajitokeze kujiandikisha kwenye sensa, baadae Sheikh Ponda, ambaye hana hata Msikiti akasema hakuna kujitokeza nini kilitokea.
 
Last edited by a moderator:

Pole sana Wickama,

Kuna vitu unavichanganya hapa!

Na utapata navyo tabu sana kama hutakua makini
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…