Hapana si kweli ni kwa baadhi ya waislam. Katika hao baadhi wengi wao ufahamu ni mdogo, ukiwauliza kwanini wanamchukia Nyerere hawana sababu bali kuishia kusema ni mbaya.
Wengi wamefundishwa chuki kitu kibaya sana.
Wameaminishwa tu but they don't have ground to stand.
Fanya research kidogo uone uelewa wa baadhi ya viongozi, wakalishe kitako, hazipiti dk 10 hawana jibu. Watakachosema tumeshikia, inasemwa au tumeambiwa.Hili litaonekana kama dharau lakini ni ukweli.
Kikundi kidogo kimejivika joho la waislam na hiki kinaendeleza chuki za akina Takdir.
Takdir hakuwa na la maana wakati ule na hadi leo. Huo ndio ukweli hata kama unakataliwa.
Nchi hii ni yetu sote na wala hakukuwa na uwezekano wa uhuru wa dini moja,hakuna kitu kama hicho. Na hata sasa nchi ni yetu sote na hilo litabaki hivyo
Nguruvi,
Hali ya nchi yetu ni mbaya.
Nafasi ya Kanisa katika kuendesha nchi sasa ni wazi na si siri tena.
Prof. Hamza Njozi alieleza tatizo hili katika kitabu chake ''Mwembecha Killings...''
Ukweli ndani ya kitabu ulitisha serikali.
Kitabu kikapigwa marufuku.
John Sivalon na yeye kaandika kitabu kuhusu nafasi ya Kanisa katika siasa za
Tanzania.
Mohamed Said akaja na historia ya kweli ya uhuru wa Tanganyika na mwisho wa
kitabu kaandika kuhusu njama dhidi ya Uislam.
Waislam wa kizazi kipya sasa wanajiuliza mengi.
Kubinywa kwa Waislam leo kuko wazi hata kama tunaogopa kulizungumza hili na
serikali inajifanya yote ni shwari.
Ukweli ni kuwa hali si shwari.
Baadhi ya marafiki wa Tanzania kwa pembeni wametoa ushauri kwa serikali
kutolifumbia macho tatizo hili.
Sisi si kikundi kidogo tuna umma mkubwa wa Waislam na ukitaka kupima nguvu
yetu angalia tulipowaambia Waislam wakatae kujiandikisha hadi kipengele cha
dini kimewekwa.
Zoezi halikufanikiwa.
Angalia ukipenda mfano mdogo tu.
Sikiliza mijadala humu JF.
Tunalo tatizo na halitoondoka kwa kutaka tu liondoke.
Tatizo litaondoka kwa kuukubali ukweli na kuzungumza bayana kuondoa dhulma.