Assalam Alykum warahmatullah wabarakatuh.
Akhy
gombesugu tukiwa tunasubiri response ya mzee
Mohamed Said juu ya mas'ala uliyomuuliza labda nizungumze kidogo kuhusu hilo la marehemu shekh Nurudini Hussein Annakshbandy. Huyu shekh alhamdulilah nimewahi kuwa mwanafunzi wake kipindi cha nyuma kidogo japo nilikuwa bado wa umri mdogo na alishawahi kutueleza mkasa wake uliomsibu kutoka kwa Nyerere yeye na rafiki yake sheki Hussein Albadawi ambaye yupo pale IRshadi Lushoto. Miaka ile ya uhuru unapatikana japo sijui alihusikaje nayeye katika harakati za uhuru walimfuata Nyerere na kumtaka mambo flani kadhaa na Nyerere alikataa na kuwaambia wawili hawa mnayo masaa 24 ya kuonekana Tanzania. Jambo hili walilipinga ndipo wakarudi Kilwa na kufanya ZAFFA ya hatari na kuitikisa nchi ndipo akaamuru jeshi likawakamata na kuwaweka ndani. What happens huko gerezani ni hatari ambayo Nyerere hajawahi kuiona. Wazee inavyosemekana walikuwa wanatoka bila gate kufunguliwa mida ya swala na wakimaliza wanarudi wenyewe. Taarifa zilipomfikia Nyerere ndipo alipowaambia kama watampinga tena kuondoka atawaua. Hussein Albadawi alikimbilia Lamu na shekh Nurudini Hussein akaenda kujificha Korogwe akijifanya mfanyabiashara wa mahindi. Na hapo ndio kikaanzishwa chuo cha Shaadhilia. Kwahiyo madhila na yeye kayapitia kutoka kwa mwalimu. Albadawi baadae alirudi na kwenda kuanzisha kile chuo pale Lushoto. More tusubirie kutoka kwa shekh
Mohamed Said.
Ayatollah
Chamviga,
Alayka Salaam,Al Habib
Maulana.
Wallahi,kila nikusomapo
bayana zako naburudika mno pasi kiasi na
najifunza mangi mno toka kwako...
Shukran Sheikh wangu.
Hiyo bayana yako ni
njema mno na yoote ulonena
nakubaliana nawe...maana nilishawahi kuyasikia takriban yoote toka kwa
Wazee Wetu.
Huyo
Sheikh Nurdin Hussein Al Sha'dhily,family yetu na yake ni watu wa karibu mno tangia kitambo. Pia alikua ni mtu wa karibu mno wa Marehemu
Babu yangu upande wa kuumeni.
Nawajua wanae wengi mno ambao ni marafiki zangu;basi itakuwa unawafahamu pia kina Ummy,Ma'ruuf,Hussein,na yule Prof. wa Literature na wengineo wengi mno...nilikua
Amerika miezi michache ilopita na nilikutana na yule Ma'ruuf.
Ile
Qadiriya ya
Al Shadhiliya pale kona ya Twiga na Sikukuu,napajua uzuri mno...na
Imam wa ile Masjid alikua ni
Sheikh Hashim Haji Abdallah,ambaye nae pia alipitiwa na ule
"msukosuko wa Baba wa Taifa"!
Yule mke wake wa mwisho/mdogo wa
Sheikh Nur'din, ni shogake mkubwa mno wa Bi Mkubwa wangu.
Pia majuzi nilichungulia mojawapo ya
post/s zako hapa,nikaona umetaja kule
Mgombezi!?
Lile shamba alifanziwa mpango kulipata na
Alhaj Issa Mtambo Gonera kulipata,na akenda kimbilia kule kujistiri baada ya ile misukosuko ya
Nyerere.
Lakini kumbuka yakuwa;hapo pana
network kubwa mno na ya kiundani/
extremely secretive,baina ya huyo Nyerere,Oscar Kambona,Alhaj Issa Mtambo,Alhaj Kitwana Kondo,Alhaj Ali Hassan Mwinyi,Ali Mwinyi Tambwe,Alhaj Umar Muhaj,
Mapinduzi ya Zanzibar,kukamatwa kwa
Masheikh wetu/Wazee Wetu na mangineyo mangi pita kiasi!?
Wakti ule msafara wa kwenda kumuona
Gamal Abdil Nasser,ukiongozwa na
Mufti Sheikh Hssan Bin Amir,ili kutembelea/kuzuru nchi kadhaa kuomba
misaada,ushauri/utaalamu kwa ajili ya kuendeleza
Ilm ya
Waislam hapo
East Afrika...yaani tayari
Nyerere alishapanga maangamizi na kuweka
Moles/informers wake takriban kwenye Embassies zetu kwenye nchi zile zoote ambazo ule msafara ungalipitia!? Kwi! Kwi! Kwi!
Wallahi,
Nyerere alikua
maluuni wa kutupwa...yaani alikua bingwa na alipewa kipaji cha kuwavuruga
Waislam maskini! Kwi! Kwi! Kwi!
Hatuna haja/lazim ya kuweka hapa kila kitu,itakua
si vyema...na natumai
utanifahamu ndugu yangu.
Huko
Lushoto,nakupenda mno...tuliwahi kuishi kwa miezi michache mno wakti fulani nikiwa mduchu na Mzee wangu alikuwa huko kishughuli....na nilikua sijui yakuwa
Shariff Hussein bado yupo pale maskini.
Mimi ni mwenyeji kiasi changu mno pale
Soni na miji/vijiji vingine vizungukavyo hiyo Lushoto,lakini Lushoto yenyewe, wenyeji wangu takriban woote wanaishi
D'salaam.
Insha Allah,tutakutana penye majaaliwa na nitazidi kuelimika kwa
Darsa zako.
Nafikri pia utakua unaifahamu hii njia ya kutoka
Korogwe mpaka
Mabokweni!? Kwi! Kwi! Kwi!....haya tuanze...Korogwe,Magoma,Bwiti,Mwele,Daluni,Maramba,Mabokweni!?
Sasa wale
Maramba Jkt,mimi ninapakana nao na ninajishughulisha na shughuli za kilimo kiduchu cha
Hiliki pale...ile ardhi tulikuwa nayo kitambo lakini ilikua haitumiki.
Ama kwa hakika nazipenda mno hizo sehemu maana ni
very fertile na watu wake ni waungwana mno...japo ukifika siku ya mwanzo lazim wakukaribishe na
"Zongo"!? Kwi! Kwi! Kwi!
Ahsanta.