Islam’s role in Tanzania’s freedom struggle

Islam’s role in Tanzania’s freedom struggle

mkuu ameshaweka wazi kila kitu. implication yake ni kushabikia wapenda kuvuruga amani nchini. nampa majibu kwasababu,nataka kuweka wazi anavyoeleweka kwa kupenda kushabikia vurugu.

mkuu tanzaniaa tumeshuhudia makanisa yakichomwa moto, mchungaji akiuwawa na waislamu kule kanda ya ziwa, mapadre wakimwagiwa tindikali, shek arusha akilipuliwa na bomu, na mabinti wa uingereza wakimwagiwa tindikali, shekh ulanga akiagiza watu wauane kule mombasa kenyea. mkuu kutokana na hayo ningeomba unipe tofauti ya shetani na mungu kwa matendo yao.

Tatizo lako wewe 2013 na wagalatia wengi ni kuwa always mnachukua 1+(? ) halafu jibu mnasema ni 2.

Tukiwauliza hii (?) Ni nini.
Mnaanza stori ndeefu ya kukwepa jibu!

Wewe kwa elimu yoote uliojaaliwa no matter how small or big it is, hebu niambie je! Ulishawahi kukaa chini ukaangali uwiyano baina ya waislamu na wakristo ktk nyanja zoote Hapo Tanzania!?

Au unakwenda na mkumbo tu kama bendera inavyofuata upepo?

Kama umeshughulisha kichwa chako kidogo HUWEZI KUSEMA chuki zilizopo na zinazoendelea kuongezeka hapa zinasababishwa na shekh huyu au maalim yule! Huko ni kuropoka bila kufikiri!

Hebu jiulize kwa undani bila kuropoka yafuatayo;-

1.kwanini shekh huyu au yule alalamike?

2. Nini madai ya waislamu wa Tz kwa serikali ilioko madarakani??

3. Je haya madai yao ni kweli ? au basi tu wanapenda fujo?

4. Tumejifunza nini toka uhuru wa nchi hii kutokana na uongozi wa nyerere kuhusiana na SUALA LA UDINI?

5.Je! Yale makosa aliyo yafanya nyerere ya kuleta ubaguzi ktk DINI ni kweli yalikuwepo? Na bado yapo??

Na kama ni hivyo je! YAMEREGEBISHWA??

6. Hawa waislamu wanapiga kelele kuwa Kuna MFUMO KRISTO HAPA TZ! Ambao muanzilishi alikuwa ni yule Nyerere! Na wanadai kuwa huu ndio chanzo CHA FITNA KUBWA BAINA YETU WATZ!

JE! KWELI MFUMO HUO UPO??

Kama hujakaa ukajiuliza haya maswali machache tu!
Basi Utapiga kelele wee kama mlevi! Na atakae kusikiliza labda awe mlevi kama wewe!

Masuala ya kumwagiana tindi kali. Kuchoma nyumba za ibada. Bla..bla..blaa!

Yoote hayo NI MATOKEO YA CHUKI!!

SASA NI NINI MZIZI WA HII CHUKI??

Je! Inaingia akilini mwako kuwa Shekh asimame aamue kusema kuwa waislamu wananyanyaswa BILA KUWA na SABABU YYT??!!!

Au kitabu cha waislamu kiwaamrishe waumini wake waende wakamwagie mtu tindikali. Basi tu kwa sababu A.na.B.na C!!
Kama utafikiri hivi! Basi wewe na ile bendera inayofuata upepo Hakuna tofauti!

Unatakiwa utumie KICHWA NA FAHAMU ZAKO KUFIKIRI NA KUFANYA UPEKUZI KIDOGO!

Huenda ktk kufanya hivyo basi kama sio wewe japo wanao watakuja kupata faida ya kujua UKWELI HALISI..Na huenda ike fitna na chuki Ikamalizika!

Na SIO ZILE ELIMU ZA WAROPOKAJI TU!

Ahsantum.
 
Last edited by a moderator:
Kwanza sioni jambo la maana kuendelea kujadiliana mambo ya jarhu wala muktadha lhali kwani sio hoja ya msingi. Kama bado msimamo wako kasengenywa haya ni twende na hoja iliyo mezani. Mtama wako tuliousubiri muda mrefu tumeshauona na tumeshaupatia majibu yake. Halafu nimekuona sehemu nyingi unaniita chamvinga badala ya chamviga sijui ni makusudi? Chamvinga katika lugha yetu inaleta maana nyingine.
Kwanza nikutake radhi hakika jina ninalofahamu ni hilo kwa makosa na nitarekebisha na kuwa @Chamviga

Mtama hauna majibu kwasababu nimeuliza wazee wa matambiko wanaangukia wapi katika wapigania uhuru?
Je, matambiko yanaangukia katika Uislam.

Jibu lililoletwa ni mimi nisiwaondoe katika Uislam kwasababu ya matambiko. Nikauliza kama ni hivyo iweje watu wawaite Bwakata makafir kwasababu kumwita mtu kafir ushamuondoa katika Uislam. Nani kapewa haki ya kusema huyu Bwakwata kafir huyu Watambiko afadhali kidogo.

Hoja niliyoweka hapo kuhusu kutengwa Nyerere kwa imani aliuliza THE BIG SHOW chanzo chake.
Nilimueleza kama ilivyoandikwa na Mohamed @#918 kuwa hiwezekani mtu abaguliwe mara mbili au tatu na aendelee kutoa pass mark. Ndio chanzo cha Bakwata.

Nashangaa Ritz anamnukuu Nyerere halafu anakana maneno yale yale anayodhani ni utetezi.
Mohamed Said ameonyesha kuwa hao wazee hawakupenda ubaguzi. Ni jambo la dhahiri kuwa kikao cha 'Yuda' kinaonyesha jinsi ubaguzi ulivyoanza na hivyo kusema Nyerere alianzisha si kweli.

Hicho ndIcho tunakikataa hapa na wengine wanajribu kukiwekea mbolea.

Kuhusu kusengenya, sidhani kama Abdul au Mshume na Nyerere wangefurahi kusikia mambo yaliyohusu mboga na sigara au maisha yao binafsi.

Kwavile wasingefurahi basi hilo halipendezi na linageuka kuwa usenganyaji.
Hata mama Maria Nyerere au watoto wake wakisoma maandishi ya Mohamed kuhusu mboga na vyumba vya kulala hawajisikii vema kabisa.

Tunaona sababu zinatafutwa kwa lugha ku justify usengenyaji. Kusengenya kutabaki kuwa kusenganya hata kwa mapipa ya perfume.

Nguruvi,
Kwako wewe hapo uliposimama ndiyo nguvu yako ilipo na itakuwa tabu
kukutoa.

Ikiwa kueleza kuwa Nyerere alikaa nyumbani kwa Abdu baada ya kuacha
kazi ya ualimu ni kusengenya mengi nilosema yatakuwa ya kusengenya
hatakuwa kasegenywa Nyerere peke yake bali hata TANU yenyewe na TAA
pia kwani vyama vyote hivyo viwili Abdu kavifadhili pakuwa.

Na kwa hakika katika hilo hakuwa Abdu peke yake.

Alikuwapo mdogo wake Ally, Dossa, Rupia, Kiyate Mshume, Mwinjuma Mwinyikambi,
Jumbe Tambaza na wengine wengi hapa Dar es Salaam.

Na ukipenda hata Tanganyika yenyewe imesengenywa kwani mchango wa
akina Sykes kwa maendeleo ya nchi hii katika kuamsha watu ni mkubwa sana.

Kumbuka kuwa baba yake Abdu ni mmoja wa waasisi wa AA na alitoa fedha
nyingi katika siasa.

Mtaumiza sana nyoyo zenu kwa historia hii.
Huu ndiyo ukweli hata kama mtu atatoa majina gani.

Haya yote yalitendeka na zilikuwapo ihsani nyingi baina yao.
Mohamed Said, kusimama na kusema Nyerere alikuwa anakwenda kuomba mboga akapewa sh 200 na Mshume Kiyate sijui kulilenga nini. Sidhani kuwa katika maisha ya Nyerere kuanzia nayakati hizo hadi anafariki hakuwahi kutenda jema na iweje yeye hapiti barabarani, au watoto wake ama vijukuu wakipaza sauti kunadi michango ya mzee wao.

Mohamed unafahamu kuwa ukitoa kwa mkono wa kulia ni vema mkono wa kushoto usione(nisahihishwe kama nimekosea)
Sasa hili la kutanganza chumba alicholala Mama Maria na Mumewe achilia mboga na matunda sijui kama si kusengenya ni kitu gani. Ninajaribu sana kufahamu kama ni Muktadhal haal au ni kitu gani.

Hiawezekani matajiri kama hao wa zama hizo wawe wamesadidia Nyerere tu, hakuna mahali wao kwa wao wanasaidiana.
Bila shaka kuna mahali lakini kwa kisitiriana hilo halisemwi na njia rahisi ya kumtia Nyerere dhalili yeye na kizazi chake ni kutumia mboga, sigara na mashuka na bakuli za kulia. Hilo umefanikiwa ingawa sijui kama umefanikiwa kuondoa legacy yake kwa wenye akili na wanazozitumia.

Nikukumbushe kuwa akina Sykes walitoa sana lakini usisahau kuwa babu yake Abdul Sykes , mzee Mbuwane alikuwa DHALIM mkubwa aliyekuja kuwaumiza Watanganyika. Angalia shilingi pande zote mbili na jaribu kuondoa makengeza. Tuwape hsehima bila kuangalia dhalili walizotufanyia. Umeshahu Mbuwane alivyokuja Tanganyika.
 
Kwanza nikutake radhi hakika jina ninalofahamu ni hilo kwa makosa na nitarekebisha na kuwa @Chamviga

Mtama hauna majibu kwasababu nimeuliza wazee wa matambiko wanaangukia wapi katika wapigania uhuru?
Je, matambiko yanaangukia katika Uislam.

Jibu lililoletwa ni mimi nisiwaondoe katika Uislam kwasababu ya matambiko. Nikauliza kama ni hivyo iweje watu wawaite Bwakata makafir kwasababu kumwita mtu kafir ushamuondoa katika Uislam. Nani kapewa haki ya kusema huyu Bwakwata kafir huyu Watambiko afadhali kidogo.

Hoja niliyoweka hapo kuhusu kutengwa Nyerere kwa imani aliuliza THE BIG SHOW chanzo chake.
Nilimueleza kama ilivyoandikwa na Mohamed @#918 kuwa hiwezekani mtu abaguliwe mara mbili au tatu na aendelee kutoa pass mark. Ndio chanzo cha Bakwata.

Nashangaa Ritz anamnukuu Nyerere halafu anakana maneno yale yale anayodhani ni utetezi.
Mohamed Said ameonyesha kuwa hao wazee hawakupenda ubaguzi. Ni jambo la dhahiri kuwa kikao cha 'Yuda' kinaonyesha jinsi ubaguzi ulivyoanza na hivyo kusema Nyerere alianzisha si kweli.

Hicho ndIcho tunakikataa hapa na wengine wanajribu kukiwekea mbolea.

Kuhusu kusengenya, sidhani kama Abdul au Mshume na Nyerere wangefurahi kusikia mambo yaliyohusu mboga na sigara au maisha yao binafsi.

Kwavile wasingefurahi basi hilo halipendezi na linageuka kuwa usenganyaji.
Hata mama Maria Nyerere au watoto wake wakisoma maandishi ya Mohamed kuhusu mboga na vyumba vya kulala hawajisikii vema kabisa.

Tunaona sababu zinatafutwa kwa lugha ku justify usengenyaji. Kusengenya kutabaki kuwa kusenganya hata kwa mapipa ya perfume.

Nguruvi3.

1) Narudia tena kukujibu hao wazee waliofanya matambiko bado wanaangukia kwenye Uislam kufanya kwao matambiko hauwezi kuwafuta kwenye Uislam, achilia mbali matambiko walifanya na makosa mengine sababu ya siasa na kumpenda Nyerere.

2) Hakuna anayewafuta Bakwata kwenye Uislam, tatizo letu na Bakwata hawana sifa ya kuwa viongozi wa Waislam wanashirikiana na Makafir kuwapiga vita Waislam, Qur'an imeishaeleza. tungekuwa tumewafuta Bakwata kwenye Uislam wala tusingekuwa tunaingia kwenye misikiti ya Bakwata na kufanya ibada.

3) Nguruvi3. Mtu yeyote akishatoa shahada (Laa ilaaha illa illa) huyu ni Muislam hata akifa kwenye makosa shahada ndiyo nguzo ya kwanza ya Uislam, haya ndiyo mafundisho ya dini yetu ya Uislam.

Nasubiri mtama mwingine...
 
Last edited by a moderator:
Nguruvi3.

1) Narudia tena kukujibu hao wazee waliofanya matambiko bado wanaangukia kwenye Uislam kufanya kwao matambiko hauwezi kuwafuta kwenye Uislam, achilia mbali matambiko walifanya na makosa mengine sababu ya siasa na kumpenda Nyerere.

2) Hakuna anayewafuta Bakwata kwenye Uislam, tatizo letu na Bakwata hawana sifa za kuwa viongozi wanashirikiana na Makafir kuwapiga vita Waislam, tungekuwa tumewafuta Bakwata kwenye Uislam tusingekuwa tunaingia kwenye misikiti yao na kufanya ibada. Nasubiri mtama mwingine...
Sijui kama nitakuwa sahihi kwa hili naomba kufahamishwa. Hivi kuna kiingilio au kadi katika dini tunazozijua? Suala la kuwafuta linatoka wapi? Nani awafute na kwa mamlaka yapi!

Sina tatizo na wazee waliofanya kila waliloona lina manufaa. Tatizo langu ni kuhusu swali la kuwa hawa nao wanaangukia katika kundi la Mohamed la Waislam? Na jibu kama ni ndio vipi inatosha mtu kuitwa Othaman na kuwa mwaislam? Nisaidie kwa elimu kidogo hapa naona yangu ni hafifu.

Kuhusu Bwakata, vipi leo wameachwa kuitwa makafir wanaitwa walioshirikiana na makafir?
Huko nyuma Khataan kaeleza mtu anayetetea dhulma ni dhalimu mkubwa,sasa hawa Bakwata nitakosea nikisema ni dhalimu wakubwa? Na kama ni dhalimu je bado wanabaki katika Uislam?

Naomba msaada na kusahihishwa nilipopokosea.
 
Na declare interest zangu kwanza. Binafsi mimi ni mkristo na nimesoma History kidogo angalau kwa level ya chuo kikuu. Sioni tatizo sana kwa jinsi mleta mod alivyoi present mada. Isipokuwa ninachokiona ni ile title ya mada tu. Labda km angewataja kama watanganyika waliosahaulika katika freedom struggle badala ya kuwavika kwanza koti la dini. Kwa maoni yangu, Utanganyika ni identity zaidi ya dini zao.

However, katika historia kuna kitu kinaitwa Noble heroes na commoners. Ni jadi duniani kote ma noble heroes kubebwa sana na commoners. Nyerere ni noble heroe lakini alifikishwa hapo alipo na wengi sana wakiwemo hao anaowataja mtoa mada waliokuwa waislam na wakristo pia hata kama walikuwa si wengi kama mzee John Rupia aliyekuwa tajiri sana by then. Commoners hubaki kuwa commoners na hakuwezi kuwa na ma noble heroes zaidi ya mmoja. Ni sheria ya historia!
 
Sijui kama nitakuwa sahihi kwa hili naomba kufahamishwa. Hivi kuna kiingilio au kadi katika dini tunazozijua? Suala la kuwafuta linatoka wapi? Nani awafute na kwa mamlaka yapi!

Sina tatizo na wazee waliofanya kila waliloona lina manufaa. Tatizo langu ni kuhusu swali la kuwa hawa nao wanaangukia katika kundi la Mohamed la Waislam? Na jibu kama ni ndio vipi inatosha mtu kuitwa Othaman na kuwa mwaislam? Nisaidie kwa elimu kidogo hapa naona yangu ni hafifu.

Kuhusu Bwakata, vipi leo wameachwa kuitwa makafir wanaitwa walioshirikiana na makafir?
Huko nyuma Khataan kaeleza mtu anayetetea dhulma ni dhalimu mkubwa,sasa hawa Bakwata nitakosea nikisema ni dhalimu wakubwa? Na kama ni dhalimu je bado wanabaki katika Uislam?

Naomba msaada na kusahihishwa nilipopokosea.
Nguruvi3.

Uislam ni dini ina mwongozo wake ambao ni Qur'an na Sunna, katika mafundisho yetu majibu yote yanapatikana humo.

Shahada ndiyo kiingilio cha Uislam, yaani wasiokuwa Waislam wakiamua kuingia katika Uislam hukaribishwa na Waislam kwa kutamkishwa shahada.

Narudia tena kukujibu tumekatazwa kuwafuta au kuwatoa watu kwenye Uislam kama kaishatamka shahada, lakini tumelekezwa jinsi ya kupambana na Waislam wanafiki ambao wanashirikiana na makafiri na kama wataenda mbali zaidi kuwapiga vitu na kuwauwa Maulamaa wanapitisha futwa kwa mujibu wa sheria.
 
Last edited by a moderator:
Sijui kama nitakuwa sahihi kwa hili naomba kufahamishwa. Hivi kuna kiingilio au kadi katika dini tunazozijua? Suala la kuwafuta linatoka wapi? Nani awafute na kwa mamlaka yapi!

Sina tatizo na wazee waliofanya kila waliloona lina manufaa. Tatizo langu ni kuhusu swali la kuwa hawa nao wanaangukia katika kundi la Mohamed la Waislam? Na jibu kama ni ndio vipi inatosha mtu kuitwa Othaman na kuwa mwaislam? Nisaidie kwa elimu kidogo hapa naona yangu ni hafifu.

Kuhusu Bwakata, vipi leo wameachwa kuitwa makafir wanaitwa walioshirikiana na makafir?
Huko nyuma Khataan kaeleza mtu anayetetea dhulma ni dhalimu mkubwa,sasa hawa Bakwata nitakosea nikisema ni dhalimu wakubwa? Na kama ni dhalimu je bado wanabaki katika Uislam?

Naomba msaada na kusahihishwa nilipopokosea.

Kwanza nikupongeze kwa kufahamu kuwa huna hakika na uyasemayo!
Well done Nguruvi3.

Pili unapoongelea MUISLAMU basi ufahamu unaongelea mtu ambae aliye sarenda maisha yake kwa amri za Muumba .
Lkn haina maana wanaojiita waislamu woote ni waungwana au ni wenye kufuata sheria za Allah 100%.

Mapungufu yapo lkn mapungufu yyt ayafanyao Muislamu hayawezi kumfanya yeye akawa KAFIRI Unless akatae kwa vitendo au kwa kauli kuwa Mungu si mmoja na Muhammad s.a.w sio mtume wa Mungu! Huyu atakuwa AMETOKA KTK UISLAMU!

Sasa tukirudi ktk suala la bakwata!

Ni kweli kabisa nilisema BAKWATA NI MADHALIMU WAKUBWA! NA WANACHANGIA SANA KTK KUWAGAWA WAISLAMU.

Maana ya UKAFIRI NI KUMSHIRIKISHA MUNGU NA VIUMBE AU VITU VINGINE!!

Na chanzo cha hio bakwata kuwa hivyo ilivyo ni HUYO NYERERE NA SIASA YAKE YA MFUMO KRISTO!

Wengi ktk watendaji wa BAKWATA ni njaa tu!! Na kuwanunua ni kazi ndoogo sana.
Imani ya dini yao ni dhaifu mno. Na hili sio BAKWATA TU!

Ukiangalia takriba makanisa yote! Kinacho wapeleka wengi wao ktk kufungua ministry ni maslahi tu!

Unless MFUMO KRISTO UFE! BAKWATA ITAENDELEA KUWA SUMU KTK JAMII YA WAISLAMU!

Ahasante
 
Last edited by a moderator:
Kwanza nikutake radhi hakika jina ninalofahamu ni hilo kwa makosa na nitarekebisha na kuwa @Chamviga

Mtama hauna majibu kwasababu nimeuliza wazee wa matambiko wanaangukia wapi katika wapigania uhuru?
Je, matambiko yanaangukia katika Uislam.

Jibu lililoletwa ni mimi nisiwaondoe katika Uislam kwasababu ya matambiko. Nikauliza kama ni hivyo iweje watu wawaite Bwakata makafir kwasababu kumwita mtu kafir ushamuondoa katika Uislam. Nani kapewa haki ya kusema huyu Bwakwata kafir huyu Watambiko afadhali kidogo.

Hoja niliyoweka hapo kuhusu kutengwa Nyerere kwa imani aliuliza THE BIG SHOW chanzo chake.
Nilimueleza kama ilivyoandikwa na Mohamed @#918 kuwa hiwezekani mtu abaguliwe mara mbili au tatu na aendelee kutoa pass mark. Ndio chanzo cha Bakwata.

Nashangaa Ritz anamnukuu Nyerere halafu anakana maneno yale yale anayodhani ni utetezi.
Mohamed Said ameonyesha kuwa hao wazee hawakupenda ubaguzi. Ni jambo la dhahiri kuwa kikao cha 'Yuda' kinaonyesha jinsi ubaguzi ulivyoanza na hivyo kusema Nyerere alianzisha si kweli.

Hicho ndIcho tunakikataa hapa na wengine wanajribu kukiwekea mbolea.

Kuhusu kusengenya, sidhani kama Abdul au Mshume na Nyerere wangefurahi kusikia mambo yaliyohusu mboga na sigara au maisha yao binafsi.

Kwavile wasingefurahi basi hilo halipendezi na linageuka kuwa usenganyaji.
Hata mama Maria Nyerere au watoto wake wakisoma maandishi ya Mohamed kuhusu mboga na vyumba vya kulala hawajisikii vema kabisa.

Tunaona sababu zinatafutwa kwa lugha ku justify usengenyaji. Kusengenya kutabaki kuwa kusenganya hata kwa mapipa ya perfume.

Sina uhakika kama kuna mtu kawaita bakwata kuwa ni makafiri unless aliandika kimakosa badala kusema sio makafiri akasema ni makafiri. Ni mtu asiyeijua dini pekee ndio atawaita bakwata ni makafiri. Kuna kanuni moja katika soma la Aqidah(mising) ya dini inasema "WALA HATUSHUHUDILII KUWA FLANI NI MTU WA PEPONI AU MOTONI ISPOKUWA KWA WALE WALIOTHIBITIKA KWAO DALILI" Maana yake ni kwamba hatuwezi kumuita mtu huyu ni kafir(ataingia motoni) au muislamu(ataingia peponi) ispokuwa kwa wale waliothibitikiwa na dalili za kuwa hivyo. Mfano Mitume wote wataingia peponi kwasababu quruani imethibitisha hilo, kuna wale maswahaba kumi waliobashiliwa pepo akiwamo Abubakar r.a, Omar r.a, Uthmaan r.a, Ally r.a,Sayd ibn Zaid r.a, Sa'ad ibn Abi waqasi r.a, Abdurhman ibn Aufi r.a, Twalha ibn Abdillah r.a, Abu Ubaida bin Jaraha r.a na wengineo waliotabiliwa pepo na Mtume s.a.w ama kwa upande wa wale waliothibitikiwa kuingia motoni ni Makafir wote yaani wakristo, Mayahudi, Majusi n.k na twasema hivyo kwakuwa quruani imelisema hilo. Kumbuka wakati huo pia kuna Makafiri miongoni mwa waislamu lakini kamwe hatuweyi kuwatamkia wao ni makafiri mpaka watìbitishiwe hilo tena sio mimi wala Ritz ila na maulamaa wenye cheo cha kiulamaa. Hapa nitakupa mfano wa watu walio na identity ya kiislamu ila wamekufurishwa kutokana na maovu yao makubwa walioufanyia umma wa kiislamu ni kiongozi wa mapinduzi ya iran Ayatollah Khomein. Bila shaka kwa ufafanuzi huu umenipata kidogo.
 
Last edited by a moderator:
Sijui kama nitakuwa sahihi kwa hili naomba kufahamishwa. Hivi kuna kiingilio au kadi katika dini tunazozijua? Suala la kuwafuta linatoka wapi? Nani awafute na kwa mamlaka yapi!

Sina tatizo na wazee waliofanya kila waliloona lina manufaa. Tatizo langu ni kuhusu swali la kuwa hawa nao wanaangukia katika kundi la Mohamed la Waislam? Na jibu kama ni ndio vipi inatosha mtu kuitwa Othaman na kuwa mwaislam? Nisaidie kwa elimu kidogo hapa naona yangu ni hafifu.

Kuhusu Bwakata, vipi leo wameachwa kuitwa makafir wanaitwa walioshirikiana na makafir?
Huko nyuma Khataan kaeleza mtu anayetetea dhulma ni dhalimu mkubwa,sasa hawa Bakwata nitakosea nikisema ni dhalimu wakubwa? Na kama ni dhalimu je bado wanabaki katika Uislam?

Naomba msaada na kusahihishwa nilipopokosea.
Mkuu Nguruvi naomba nikueleze masuala kiduchu ninavyo yafahamu mimi kuhusu bakwata na kuhusu ukafiri.
Naanza na Bakwata kwanza utambue Bakwata ni taasisi kama zilivyo taasisi nyingine za kiislamu kwa mfano Islamic foundation na nyinginezo.
Tatizo lililoko ni kwamba serikali yetu imewapa mamlaka makubwa Bakwata kuwa wasemaji wakuu wa waislamu na hilo jambo Sio sawa,kwa mfano wakati wa kudai mahakama ya kadhi taasisi zote zilishiriki cha ajabu kwenye kuchagua makadhi mufti alifanya maamuzi bila kushirikisha taasisi nyingine.

Kuhusu kafiri hapo nyuma tulishakueleza kuhusu maana ya neno kafiri na al akhy chamviga,na sidhani kama kuna mtu anawaita Bakwata ni makafiri hiyo sio Sawa kwa ufahamu wangu mimi,kwasababu hatakama viongozi wa bakwata wamefanya kufru huwezi kuwaita makafiri mpaka kwanza uwalinganie.

Katika masuala ya "usul fikhi" huwezi kumuita mtu kafiri hatakama ni muislamu kafanya kufru kwanza mpaka umlinganie kwa hoja na dalili kupitia kitabu na sunna.
Ahsanta
 
Sina uhakika kama kuna mtu kawaita bakwata kuwa ni makafiri unless aliandika kimakosa badala kusema sio makafiri akasema ni makafiri. Ni mtu asiyeijua dini pekee ndio atawaita bakwata ni makafiri. Kuna kanuni moja katika soma la Aqidah(mising) ya dini inasema "WALA HATUSHUHUDILII KUWA FLANI NI MTU WA PEPONI AU MOTONI ISPOKUWA KWA WALE WALIOTHIBITIKA KWAO DALILI" Maana yake ni kwamba hatuwezi kumuita mtu huyu ni kafir(ataingia motoni) au muislamu(ataingia peponi) ispokuwa kwa wale waliothibitikiwa na dalili za kuwa hivyo. Mfano Mitume wote wataingia peponi kwasababu quruani imethibitisha hilo, kuna wale maswahaba kumi waliobashiliwa pepo akiwamo Abubakar r.a, Omar r.a, Uthmaan r.a, Ally r.a,Sayd ibn Zaid r.a, Sa'ad ibn Abi waqasi r.a, Abdurhman ibn Aufi r.a, Twalha ibn Abdillah r.a, Abu Ubaida bin Jaraha r.a na wengineo waliotabiliwa pepo na Mtume s.a.w ama kwa upande wa wale waliothibitikiwa kuingia motoni ni Makafir wote yaani wakristo, Mayahudi, Majusi n.k na twasema hivyo kwakuwa quruani imelisema hilo. Kumbuka wakati huo pia kuna Makafiri miongoni mwa waislamu lakini kamwe hatuweyi kuwatamkia wao ni makafiri mpaka watìbitishiwe hilo tena sio mimi wala Ritz ila na maulamaa wenye cheo cha kiulamaa. Hapa nitakupa mfano wa watu walio na identity ya kiislamu ila wamekufurishwa kutokana na maovu yao makubwa walioufanyia umma wa kiislamu ni kiongozi wa mapinduzi ya iran Ayatollah Khomein. Bila shaka kwa ufafanuzi huu umenipata kidogo.

Kwa mantiki hii, Mohamed Said naye ni kati ya "maulamaa" kwavile katika maandishi yake mengi amekuwa akitanabaisha kuwa kuna BAKWATA na kuna waislam, kama vile walioko ndani ya BAKWATA si waislam.
 
Last edited by a moderator:
kwa mantiki hii, mohamed said naye ni kati ya "maulamaa" kwavile katika maandishi yake mengi amekuwa akitanabaisha kuwa kuna bakwata na kuna waislam, kama vile walioko ndani ya bakwata si waislam.

sina uhakika kama tanzania kuna "maulamaa" nitaomba nirekebishe katika hili. Na

aliposema kuna bakwata na kuna waislamu katika hayo maandishi yake alikuwa alikuwa anaongelea nini?
 
Hajjat Faizafoxy,

Shukran nyingi kwa kunijuza yayo. Pia tunakusoma mno kwa bayana zako adimu na Ilm utoayo humu Jf.

Mola
takulipa kwa yoote na kukuzidishia neema Insha Allah.

Ni kweli huyo Bwana Idd Bin Khamis unamjua uzuri. Alikua pia na mwanae wa kiume,msomi mzuri akiitwa Mzee Bin Idd Khamis,huyu nafikiri alisomea Jordan na Israel kipindi fulani.

Huyo Colonel "Baruti" Ramia,namfaham uzuri mno. Tulikua tukienda kumtembelea na Bwana mkubwa/Mzee wangu mara kadhaa wakti akiwa pale JWTZ/Ngerengere.

Huyo jina lake ni Yahya Bin Ramia...lakini si unakumbuka enzi ile ya Nyerere,kuna Waislam wengi walokua wasomi/Wanataaluma,iliwalazim kubadili majina kutia nakshi za Uafrika ili kuonekana ati ndo "mzalendo" zaidi na pia usionekane unaupenda Uislam au "Uarabu"!? Kwi! Kwi! Kwi!

Huyo Colonel Ramia,nakumbuka mara ya mwisho ndo alokua MP wa Bagamoyo kabla ya Muheshimiwa Al Rais Mrisho Kikwete hajachukua ule ubunge wa pale Bagamoyo.

Huyo Bwana,alipewa jina la great-grandfather wake yaani Sheikh Yahya Mohammed Ramia...ambae mwanae Sheikh Mohammed Bin Yahya Ramia ndie aliekuammojawapo wa wanaharakati/wanasiasa wakubwa na vinara mahiri wa siasa wakti huo wa mapambano. Pia ndie aliekua mmojawapo wa wafadhili wakubwa mno wa yule Nyerere binafsi.

Hawa ndo baadhi ya waliokua marafiki wa karibu mno kutoka ile Madrasat Al Hassanain/Islamic Seminary ilokua maarufu mno hapo Mzizima na ilotoa watoto wa mjini wengi waliokua wasomi...kina Mohammed Mwita/Chief Engineer Government Hanger,Prof. mansour Hussein,Dr Muhidin Hussein,Sheikh Yahya Hussein,SSP mwanakondo Aziz Ali then Businesswoman,SACP Abdallah Gwebe Formerly Kigoma RPC,Musadique Azzan aka Zungu Bussineman former Airman/Helicopter Pilot and Mechanic now Mp for Ilala,Brigadier Ahmed Takadir,Brigadier Simba Wazir,Bakari Himidi General Manager Kilombero Sugar Company na Bukoba Sugar Company,Shaaban Mar'ejby,SSP Kitwana Luga Usalama wa Taifa then Bussineman,Colonel Dr.Keis Mtambo aliekua Personal Chief Medical Officer wa Nyerere kwa miaka kadhaa,Dr. Idris Msabaha MP/Principal Secretary Ministry of Foreign Affairs,Mohammed Azzan Bussineman,Abdallah Awadh Bussineman,Salum Hiriz Businessman,Mohammed Riyami Airforce Mechanic na wengineo wengi mno pasi!

Wengi wao maskini wamefariki vijana mno...Inna Lillahi Wa Inna Illahi Ra'juun!

Hawa woote ni nduguze Sheikh Mohamed Said,na anawatambua uzuri mno kuliko mimi!

Hiyo Madrassa ilikua chini ya Uongozi wa Al Marhum Sheikh Hussein Bin Juma wa UTP na twin Brother wake Al Marhum Sheikh Hassan Bin Juma...ambae ndie aliekua Baba yake Mzazi Sheikh Yahya Hussein.

Kwenye mnakasha ulopita niliwahi kumuomba Sheikh Mohamed Said,atuwekee japo kiduchu hizo khabar za Madrassat Al Hassanain...labda safari hii akipata fursa atakumbuka na kutuwekea!?

Kama kuna lolote/chochote hapo nimepotoka,tafadhali usisite kunielekeza Dadangu...maana sisi soote tumo hapa kuelekezana.

Ahsanta.

Cc;Maulana Dr. Kahtaan,Shariff Ritz,Al Habiby Al Tayeb,Ulamaa Boko Haram,Ayatollah Chamviga

Akhiy, gombesugu,

Wengi kati ya unaotutajia hapo juu ni watu nnaowajua fika. Ni "kaka" zangu wa Dar. La Haula... Walotutangulia Mwenyeezi Awarehem nasi tuliobaki tuwe kwenye rehma zake, Amin.

Wallahi hizi nyuzi za Akh Mohamed Said zinatukutanisha "spiritually" na wazee wetu na ndugu zetu na sisi wenyewe.

Halafu wanakuja wapuuzi kubeza haya? hivi inawauma sana waonapo aahh hawa watu wana historia iliyotukuka? najiuliza, sipati jibu, labda ndugu zangu humu jamvini mnisaidie.

Ni nini kinachowauma hawa watu mpaka walete kejeli na istihizai na kufanya kila hila kujaribu kuishusha hadhi historia ya Waislaam?
 
Kwa mantiki hii, Mohamed Said naye ni kati ya "maulamaa" kwavile katika maandishi yake mengi amekuwa akitanabaisha kuwa kuna BAKWATA na kuna waislam, kama vile walioko ndani ya BAKWATA si waislam.

Hili suali lako/"hoja"...hapa hatuna majawaba yake asilan,na wala yeye Sheikh Mohamed Said nae pia hatakujibu abadan!

Kwa msaada zaidi labda upitie kule "jukwaa la dini",yaweza akatokea kiumbe yeyote kukujibu kwalo.

Nafuatilia baadhi ya post/s zako,yaani wewe huna tafauti na yule Remote kabisaa!

Nilishaona kwenye post siku chache zilizopita,ati unamuita Sheikh Mohamed Said ni fitna/mzandiki,mchonganishi!?

Sasa kama tayari mtu huyo huyo umeshamuwekea alama hizo...yaani dhanna/conclusion,yawaje leo warejea hapa jamvini kutuuliza sisi hicho kisuali chako!?

Kwa kifupi,wewe ni miongoni ya wale wakorofi tu na wala huna credibility ya kuuliza suali la maana.

Niwie radhi kwa huo uchechefu wangu kiduchu,natumai hutakereka asilan!?

Tukumbuke yakuwa ni muhimu kuambizana kweli,khasa kwenye mijadala ya kitaaluma kama hii.

Ahsanta.
 
Akhiy, gombesugu,

Wengi kati ya unaotutajia hapo juu ni watu nnaowajua fika. Ni "kaka" zangu wa Dar. La Haula... Walotutangulia Mwenyeezi Awarehem nasi tuliobaki tuwe kwenye rehma zake, Amin.

Wallahi hizi nyuzi za Akh Mohamed Said zinatukutanisha "spiritually" na wazee wetu na ndugu zetu na sisi wenyewe.

Halafu wanakuja wapuuzi kubeza haya? hivi inawauma sana waonapo aahh hawa watu wana historia iliyotukuka? najiuliza, sipati jibu, labda ndugu zangu humu jamvini mnisaidie.

Ni nini kinachowauma hawa watu mpaka walete kejeli na istihizai na kufanya kila hila kujaribu kuishusha hadhi historia ya Waislaam?

Hajjat Faizafoxy,

Asalaam Alaykum,Shukran nawe pia.

Nimekusoma na kukufahamu kwa undani mno.

Kwa kifupi,siku alipofariki Sheikh Mohammed Ramia pale Bagamoyo...yeye Colonel Yahya Baruti Ramia na Uncle wake Abdilrahman Mohammed Ramia(alikua Usalama wa Taifa),ndio waliompigia simu "Bwana" Nyerere kumpa khabar za msiba/kifo.

Nyerere mwenyewe akawajibu yakuwa,tayari nimeshapata khabar asubuhi hii,lakini ati alikua akisubiri simu/telephone conversation na yule Terrorist wake wa Kimakonde aka Samora Machel,lakini aliahidi angehudhuria mazikoni/msibani!?

Mpaka hivi nikwambiavyo,mpaka leo hawajamuona/hawakumuona tena Nyerere,sijui kama bado wanamsuburia!? Kwi! Kwi! Kwi!

Watu wengi pale msibani walistaajabu mno,khasa ukichukulia ule ukaribu wa miaka mingi mno baina ya zile harakati za "Uhuru",TANU,Sheikh Ramia na yule Nyerere!?....huyo ndie "Baba wa Taifa"!

Shukran na nimefurahika mno kuzungumza nawe,japo kiduchu.

Ahsanta.
 
Hili suali lako/"hoja"...hapa hatuna majawaba yake asilan,na wala yeye Sheikh Mohamed Said nae pia hatakujibu abadan!

Kwa msaada zaidi labda upitie kule "jukwaa la dini",yaweza akatokea kiumbe yeyote kukujibu kwalo.

Nafuatilia baadhi ya post/s zako,yaani wewe huna tafauti na yule Remote kabisaa!

Nilishaona kwenye post siku chache zilizopita,ati unamuita Sheikh Mohamed Said ni fitna/mzandiki,mchonganishi!?

Sasa kama tayari mtu huyo huyo umeshamuwekea alama hizo...yaani dhanna/conclusion,yawaje leo warejea hapa jamvini kutuuliza sisi hicho kisuali chako!?

Kwa kifupi,wewe ni miongoni ya wale wakorofi tu na wala huna credibility ya kuuliza suali la maana.

Niwie radhi kwa huo uchechefu wangu kiduchu,natumai hutakereka asilan!?

Tukumbuke yakuwa ni muhimu kuambizana kweli,khasa kwenye mijadala ya kitaaluma kama hii.

Ahsanta.

Should I be concerned of what gombesugu thinks of me? Should I care that Moh' Said doesn't respond to my post?Think again!!

Yes, nimemuita Moh' Said ni Mfitini (na ni ukweli, anafitinisha jamii), kama wewe unavyoniita mkorofi.

Asante.
 
Last edited by a moderator:
sina uhakika kama tanzania kuna "maulamaa" nitaomba nirekebishe katika hili. Na

aliposema kuna bakwata na kuna waislamu katika hayo maandishi yake alikuwa alikuwa anaongelea nini?

Asante kwa ufafanuzi.

Nimeanza kumsoma na sometimes kubishana na Mohamed Said toka 2010. Threads zote alizozianzisha nimesoma na most of the time nimeweka some posts.
It is unfortunate kuwa siwezi kwanza kuzi-trace ili nikueleze alivyomaanisha kuhusu "waislam" na "bakwata". It is just not worth it.
Ila kwa vile wewe unapenda kusoma posts zake, nakushauri upitie threads zake zilizopo hapa JF, na utakubaliana nami. Otherwise, najua wengi waliomsoma muda mrefu, hata baadhi ya waislam, watakubaliana nami kuwa Moh amewa-classify waislam into "moslems" and BAKWATA.
 
Sina uhakika kama kuna mtu kawaita bakwata kuwa ni makafiri unless aliandika kimakosa badala kusema sio makafiri akasema ni makafiri. Ni mtu asiyeijua dini pekee ndio atawaita bakwata ni makafiri. Kuna kanuni moja katika soma la Aqidah(mising) ya dini inasema "WALA HATUSHUHUDILII KUWA FLANI NI MTU WA PEPONI AU MOTONI ISPOKUWA KWA WALE WALIOTHIBITIKA KWAO DALILI" Maana yake ni kwamba hatuwezi kumuita mtu huyu ni kafir(ataingia motoni) au muislamu(ataingia peponi) ispokuwa kwa wale waliothibitikiwa na dalili za kuwa hivyo. Mfano Mitume wote wataingia peponi kwasababu quruani imethibitisha hilo, kuna wale maswahaba kumi waliobashiliwa pepo akiwamo Abubakar r.a, Omar r.a, Uthmaan r.a, Ally r.a,Sayd ibn Zaid r.a, Sa'ad ibn Abi waqasi r.a, Abdurhman ibn Aufi r.a, Twalha ibn Abdillah r.a, Abu Ubaida bin Jaraha r.a na wengineo waliotabiliwa pepo na Mtume s.a.w ama kwa upande wa wale waliothibitikiwa kuingia motoni ni Makafir wote yaani wakristo, Mayahudi, Majusi n.k na twasema hivyo kwakuwa quruani imelisema hilo. Kumbuka wakati huo pia kuna Makafiri miongoni mwa waislamu lakini kamwe hatuweyi kuwatamkia wao ni makafiri mpaka watìbitishiwe hilo tena sio mimi wala Ritz ila na maulamaa wenye cheo cha kiulamaa. Hapa nitakupa mfano wa watu walio na identity ya kiislamu ila wamekufurishwa kutokana na maovu yao makubwa walioufanyia umma wa kiislamu ni kiongozi wa mapinduzi ya iran Ayatollah Khomein. Bila shaka kwa ufafanuzi huu umenipata kidogo.

Ayatollah Chamviga,

Asalaam Alaykum,nakusomeni sana Al Akhiy na Shukran kwenu nyoote hapa jamvini kwa kunifungua macho na kunifundisha kwa yalo mangi.

Nimesoma hiyo bayana yako kiduchu,ikanilazim kucheka...kumbe ndo maana siku ile ukanambia yakuwa huna hakika na hilo jina nilokupa la Ayatollah!? Kwi! Kwi! Kwi!

Naona Askofu Nguruvi3,kaamua kuvua majoho yake na ati sasa nae ameamua kutambaa na uchambuzi wa "Tartib Al Adab"!? Kwi! Kwi! Kwi!...Wallahi,humu Jf pana vitimbi/vituko vingi mno! Kwi! Kwi! Kwi!

Kwa kifupi,yeye Nguruvi3 afanzacho sasa ni kutumia Psychological Warfare and/or playing game. Anajitahidi mno kudodosa mle mle kwenye majawaba mumpayo na kutafuta zile loop holes za kitoto.

Jaribu kuwa mwangalifu nae kiduchu,wala sikufundi jinsi ya kumjibu,hasha!...nisemacho ni yakuwa kuwa makini/balance na majawaba yako huku uki-anticipate suali jingine toka kwake katika hayo hayo majawaba yako!? Kwi! Kwi! Kwi!

Bwana Nguruvi3,pamoja na yoote lakini yeye ni mwenzetu "kiaina"...yeye bila ya sisi "hawezi" kuishi,nasi bila ya yeye "hatuwezi" kuishi. Twende nae tu hivyo hivyo,la si hivyo tutamtupia nani!? Kwi! Kwi! Kwi!

Kuhusu ile khabar ya Ayatollah Khomein,nafikiri labda pia ni uzuri Al Akhiy,tujihadhari na kwenda nje mno ya mada yetu khasa pale tunapotoa mifano kadhaa,japo nimependa pia huo mfano ulogusia.

Hizo geopolitics,mie ndo mojawapo ya fields zangu na ninawezajinasib yakuwa kwa kiasi changu natambua mangi mno...lakini pia nakubali yakuwa pana wengi mno hapa jamvini mjuao mangine mangi mno kunizidi mara alfu!

Nakukumbusha kiduchu tu;Maulana Ayatollah Khomein, ndie mmojawapo ya Viongozi wa Kiislam duniani waliofanziwa attacks na character deformation nyingi mno pita kiasi,na wale maharamia wa Western World kwa kutumia zile mainstream media outlets zao...khasa wale CIA,State Depart. Strategists,Zionist Propagapanda machine/Movement,Saud Royal Family na mangineyo mangi mno pasi kiasi!

Na hayo mambo nafikiri unayafahamu kiundani na jinsi mpaka kesho yanavyoendelezwa humu dunia nzima!?

Kwa kifupi,huku kuchafuana baina ya Waislam kama tunakokuona leo duniani,baina ya Saud Royal family/Gulf States,Amerika na Iran kwa upande mwingine...kunaleta na kusababisha mparaganyiko na athari kubwa mno kwa sisi Waislam wenyewe popote tulipo duniani na hata pia kwa jamaa zetu wengine tunao-share nao hii dunia!?

Sijui mwenzangu unafahmu vipi "uhusiano" wa karibu mno na wa miaka mingi pita kiasi,baina ya Amerika,Saud Royal family na Israel!?

Haya mambo ni makubwa mno na ya kiundani...na madhara yake mengi yanatupata sisi nchi/watu maskini duniani hata bila ya kujali tafauti ya imani na itikadi zetu.

Nimetembelea mara kadhaa kwa shughuli za hapa kibaruani pangu,pale Tehran,Qoom,Baluchstan,Islamabad,Jeddah,Lebanon,Damascus na ile Israel miji kadhaa na pia tuna family pale...unajua Wifey wangu ni Austrian Jew.

Hao ndugu zetu wa Ki-Iran ni watu wema mno na walikua wako civilised dahri nyingi mno,hata kabla ya Mtume wetu mtukufu hajazaliwa...japo wakti huo wao walikua wakiabudu moto...Zoroastrianism! Kwi! Kwi! Kwi!

Nakumbuka haya majambo kuna wakti nilifanza mabishano "mapana" ya kimazungumzo na Bwana Rostam Aziz...mwishowe tulifikia tamati ya agree to diagree!? Kwi! Kwi! Kwi!...si unajua yeye ndugu yetu asili yake ni wale Sunni wa kule Iran.

Mimi nimeona kwa macho yangu hishma na vyeo kwenye nyanja mbalimbali wanapozopewa Jews,Atheist,Sunnis,Budhists na wengineo wengi kwenye ile Islamic Republic of Iran...kuliko hata huko kwenye hizo nchi nyingi za Western wenye kujiita ati ndo "Civilised".

Nilishawahi pia kufanza mazungumzo ya kina na Sheikh Abdillahi Nassir pale Nairobi...unajua yeye ndugu yetu ni Kiongozi/Imam mkubwa mno wa ma-Shia kwa hapo East Afrika...lakini mwishowe tukaishia kucheka na kumwambia bado hajanipata!? Kwi! Kwi! Kwi!

Si unajua yule mtu Ilm zake zoote secular/Islamic ni kubwa na pana mno...nami kwa umbumbumbu wangu ati nilijifanza kutaka kumuuliza visuali vyangu vya kitoto.

Nafikiri haya yatosha kwa leo Al Akhiy,na Insha Allah labda siku nyingine tupate wasaa kunyambua kwa undani tukiwa hapo Lushoto na Mtae!?

Shukran kwa kunisikiza,na niwie radhi Al Akhiy kama kuna lolote nimenena kwa ukosefu labda wa Ilm.

Hata hivyo nimefurahika kunijaalia fursa hii ya kuzungumza nawe.

Ahsanta.
 
Should I be concerned of what gombesugu thinks of me? Should I care that Moh' Said doesn't respond to my post?Think again!!

Yes, nimemuita Moh' Said ni Mfitini (na ni ukweli, anafitinisha jamii), kama wewe unavyoniita mkorofi.

Asante.

Mkuu Nanren,

Nisamehe tena Mkuu wangu,kama hukuipenda ile bayana yangu...nakumbuka nilikutaka radhi na kukusihi usikereke!?

Khalaf mbona pia wanichanganyia lugha Mkuu!? Si mnajua sisi Waislam "kithungu" ni taabu,yaani cha kuchapia...sasa nitakufahamu vipi!? Kwi! Kwi! Kwi!

Punguza hamaki Mkuu!

Ahsanta.
 
Akhiy, gombesugu,

Wengi kati ya unaotutajia hapo juu ni watu nnaowajua fika. Ni "kaka" zangu wa Dar. La Haula... Walotutangulia Mwenyeezi Awarehem nasi tuliobaki tuwe kwenye rehma zake, Amin.

Wallahi hizi nyuzi za Akh Mohamed Said zinatukutanisha "spiritually" na wazee wetu na ndugu zetu na sisi wenyewe.

Halafu wanakuja wapuuzi kubeza haya? hivi inawauma sana waonapo aahh hawa watu wana historia iliyotukuka? najiuliza, sipati jibu, labda ndugu zangu humu jamvini mnisaidie.

Ni nini kinachowauma hawa watu mpaka walete kejeli na istihizai na kufanya kila hila kujaribu kuishusha hadhi historia ya Waislaam?

Wallahi,

Najisikia mnyonge na huzuni mno mkiwataja mabwana hawa mmungu awawie radhi. Sheikh Mohamed Ramia na Sheikh Yahya Bin Hussein nimewasikia wakisema Dar-es-Salaam ni jiji la amani na wasomaji quran. Maskini sasa hivi wasomaji wazuri wa quran ni dhalili na maskini na hakuna hasa Dar.

Shida moja ndugu zangu wanayoipata wanatamani hii tunu walioipata waislamu waipate wao kwani ni tunu iliyopo katika kiini cha historia ya uhuru wa Tanganyika. Hakuna mtu mwenye kuishi kariakoo asiyemjua Sheikh Ramia, Sheikh Hassan Bin Ameir, Abdu sykes, Mshume Kiyate na wengineo wengi waliokuwa katika harakati za uhuru.

Ingelikuwa mmungu amewapa tunu hiyo wenzetu basi tungeliwajua hadi babu zao walikotoka but kwakuwa tunu hiyo kawanyima basi ni husda, choyo na hiyana ndio zinawasukuma mapovu kuwatoka kujaribu kudivert the truth.
 
Back
Top Bottom