mzee, hao sio wazungu, uzuri wenzetu wanafuata sana dini, wana vyama vya kidini nchi zote na wana utaratibu ambao hata wakae miaka mingapi hawapotezi identity. na hii ndio ilisababisha hata hitler akawaua kwa urahisi kwasababu walikuwa wanajulikana na wao wanajijua kama wao ni wayahudi. hao unaosema wazungu wanaweza kuwa wamezaliana na wazungu lakini DNA ni ile ile. sawa na wewe ukienda kuzaa na mmalawi lakini toto wako ni mtz. wapo wachache sana ambao wameasili dini, wengi wao ni wayahudi wa kuzaliwa. hata hivyo, jua kwamba wao hata mwanamke wa kiyahudi akizaa na kabila ingine, mtoto ni myahudi na ina nguvu sana tu kama ile ya baba kuzaa na kabila ingine. wapo kimakabila sana, kuna wale ashkenazi ambao ni wahayudi waliokuwa wamezaliwa kanda za urusi, ujerumani,austria,poland na ulaya mashariki. hawa walizaliana kidogo na wazungu ndio maana ni weupe sana. wapo wengine walizamia nchi za yemen na uarabuni, wana tabia na tamaduni za kiarabu kidogo, na wengi sio weupe kama wengine. wengine ni wale walioenda australia, marekani, canada, mexico, agentina etc. lakini asili yao haipotei. hivyo kuwaita wazungu ni upuuzi, hao sio wazungu ndugu. nimeshakuwa nao mara nyingi na nimeshaingia hadi kwenye sinagogi lao katika nchi fulani hivi. ninawajua vizuri sana. Mungu ibariki Israel.