ISRAEL kuikalia palestina Milele

ISRAEL kuikalia palestina Milele

Mrengwa wa kulia

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2022
Posts
1,091
Reaction score
3,695
Wayahudi wana haki waliyopewa na Mungu kwa nchi hii. Kiongozi mmojawapo wa vyama viwili vya siasa kali za mrengo wa kulia, vinavyounga mkono walowezi, ambavyo Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu alivileta katika muungano wake wa serikali baada ya uchaguzi wa 2022.

Smotrich anahudumu kama waziri wa fedha lakini pia ana wadhifa katika wizara ya ulinzi, ambao umemruhusu kufanya mabadiliko makubwa kwa sera za Israel katika Ukingo wa Magharibi.

Amewekeza kwa kiasi kikubwa fedha za serikali katika makazi ya walowezi, ikiwa ni pamoja na barabara mpya na miundombinu. Lakini pia amechukua mamlaka kutoka kwa jeshi, ili kuharakisha ujenzi wa makazi ya walowezi.

Katika matamshi yaliyorekodiwa kwa siri akiwaambia wafuasi wake, Smotrich alijigamba kuwa anafanya kazi kubadilisha DNA ya mfumo juu ya utanuzi wa makazi, na itakuwa rahisi kueleweka katika sheria na muktadha ya kimataifa.

Wazalendo wa kidini walikuwa pembeni mwa siasa za Israel kwa miongo kadhaa. Lakini itikadi yao polepole imekuwa maarufu zaidi. Katika uchaguzi wa 2022, vyama hivi vilichukua viti 13 katika bunge la Israel lenye viti 120 na kuwa katika muungano wa mrengo wa kulia wa Netanyahu.

Wanahakikisha vita vya gaza vinachukua muda muda mrefu ili kujihakikishia kuukalia ukingo wa magharibi bila bughudha kisha Israel waweze kuichukua palestina Yote.

Source BBC
 
Wafuasi wa mkosa nyumba shida sana. Roll model wenu alilala njia panda akamuona shetan,i kwenye ndoto yake. Shetani akamuambia Yesu ni Mungu. Nyie mnaota Israel kapewa nchi na Mungu, wakati kapewa na Muingereza hamna hata aibu.
 
Wafuasi wa mkosa nyumba shida sana. Roll model wenu alilala njia panda akamuona shetan,i kwenye ndoto yake. Shetani akamuambia Yesu ni Mungu. Nyie mnaota Israel kapewa nchi na Mungu, wakati kapewa na Muingereza hamna hata aibu.
Kaka hiyo habari imeandikwa na bbc na mleta mada kaweka na source sio mawazo yake.
 
Arabs should go back to Arabian peninsula even Egyptian, Moroccan,Algelia,Sudan,Libya,Mauritania na baadhi huyo Africa ya kati.. Let Waisrael warudi kwao wakiwemo Taliban Pashtun, wale zimbabwe,Wairaqwi wa Tanzania n.k
 
Israel anafaa akatiwe kuanzia manyara mpaka kigoma ashuke mpaka kusini yote apande mpaka tabora yote...tuna land kubwa sana nzuri unproductive wakati wao wanagombania majangwa huko
 
Back
Top Bottom