Kupambana na mtu aliyechoka uonevu, aliyejitoa kufa ama kupona, anayekwenda vitani anafahamu atakufa na akifa ni sawa au akipona ni sawa, huwezi toboa, huwezi shinda. Aisee mentality waliyonayo hao Hamas tayari ni silaha, ni zaidi ya iron dome au silaha yeyote unayoifahamu.
Zamani nilifikiri kuwa na misilaha ya gharama na kutisha ndio kuwa mbabe, lakini kwa sehemu kubwa naona katika vita silaha kubwa ni mentality na morale waliyonayo askari, haya masilaha yenye majina ya kutisha sijui Lockheed Martin F22 Raptor, utasikia Lockheed Martin F-35 Lightning II ni mbwe mbwe na ni biashara za watu, silaha inapambwa kwa sifa mbalimbali ili biashara zifanyike utasikia inakimbia km 2500 kwa saa, hizo ni biashara za watu mambo ya military–industrial complex.
Ndio maana unakuta silaha yenye thamani dola milioni moja, inaharibiwa na silaha ya dola elfu moja, kama sio biashara za watu ni nini?
Inashangaza sana lakini ndio ukweli, myahudi this time around amefeli na kuaibika kwa wakati mmoja, inashangaza.