Israel kuwatuma wanajeshi 50,000 wa akiba Gaza

Israel kuwatuma wanajeshi 50,000 wa akiba Gaza

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
838
Waziri wa Ulinzi wa Israel, Israel Katz, ameuidhinisha mpango wa kijeshi wa kuuteka mji wa Gaza na pia ameidhinisha hatua ya kuwashirikisha askari wa akiba katika zoezi hilo

Wizara ya Ulinzi ya Israel imethibitisha kwamba majenerali wakuu tayari wameidhinisha operesheni hiyo mpya inayolenga kuyadhibiti maeneo ya jiji la Gaza ambayo bado hayajafikiwa na jeshi la Israel, ambako inadhaniwa wapiganaji wa kundi la Hamas wapo kwa wingi na wanaendeleza shughuli za kundi hilo.

Maafisa wa kijeshi wamesema mpango huo sasa unasubiri idhini ya mwisho kabla ya kuanza kutekelezwa. Jamii ya kimataifa ina wasiwasi kuhusu raia wa kawaida kupoteza maisha yao katika eneo hilo la Gaza lenye watu wengi.

Afisa mmoja wa kijeshi aliyezungumza bila kutaka kutambulishwa amebainisha kuwa takriban askari wa akiba 50,000 wataitwa kujiunga na operesheni ya kijeshi mwezi ujao, na uwezekano wa kuongeza idadi ya askari hao wa akiba hadi takriban 120,000. Muda sahihi wa kuanza operesheni hiyo ya kijeshi katika ardhi ya Gaza bado haujawekwa wazi
 
Back
Top Bottom